Wednesday, May 14, 2014

Umoja wa mataifa waingia doa na mapambano ya Ukraine.

Jaji aamuru mwanariadha akapimwe akili.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 14/05/2014. Jaji  anayesikiliza kesi ya mauaji nayo mkabili mkiambiaji Oscar Pistorius, ametoa amri ya kuchunguzwa akili kwa mwanariadha huyo ili kuweza kupata kufahamu uwezo wake wa akili na ufahamu.

Akitoa amri hiyo Jaji Thokozile Masipa alisema " mshitakiwa anatakiwa kuangaliwa kiakili kwani, itasaidia mahaka kujua ni kwa kiasi gani haya makosa yalifanyika, kwa maana hali ya kutambua akili na ufahamu wa mtu si kazi ya mahakama."

"Matatizo ya akili yanatakiwa kuangaliwa na siyo jambo la kulifumbia macho." Aliongezea Jaji Masipa.

Uamuzi huo wa Jaji Masipa wa kutaka Oscar Pistorius kuchunguzwa akili umekuja baada ya kusikiliaza mwenendo mzima wa kesi na pia kwa upande wa utetezi kutaka uchunguzi huo ufanyike kwa kutokana na historia ya maisha ya mshitakiwa.

Oscar Pistorius, ambaye ni mwanariadha wa kwanza kushiriki katika mbio za Olimpiki jumla za mwaka 2012 London akitumia miguu bandia, alikili kumwua bila kukusudia mpenzi wake Reeva  Steenkamp katika siku ya wapendanao dunia.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael ahukumiwa kwenda jela.


Jerusalem, Izrael - 14/05/2014. Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael amehukumiwa kwenda jela kwa muda wa miaka sita na kutakiwa kulipa faini ya Euro 210,000.

Ehud Olmert ambaye alikuwa waziri mkuu mwaka 2006, alikutwa na hatia ya kuhusika katika kula  rushwa wakati alipo kuwa meya wa jiji la Jerusalem.

Akitoa hukumu, Jaji David Rosen alisema, " kuwa kiongozi anaye ongoza jamii na kukabidhiwa dhamana ya wananchi ni lazima awemfano bora kwa jamii, na kitendo cha kukubali kula rushwa lazima kikomeshwe kwa kiongozi yoyote aliyehusika kwa kuadhibiwa vikali."

"Makosa aliyokutwa nayo Olmert yalikuwa kukubali kula mlungura katika harakati za kuandaa mipango mji, na pia pesa nyingi kutumika kiholera katika kutangaza baadhi ya miradi na vilevile kutoa unafuu wa kodi kinyume na sheria na hata kushinikiza baadhi ya sheria kuundwa ili kutoa ubukheri kwa wahusika katika ujenzi wa  jiji la Jerusalem."

Kesi ya Ehud Ormert imechukua zaidi ya miaka miwili,na uchunguzi  ulianza rasmi kufanyaki mwaka 2010 na baadaye kuonekana  Olmert alikuwa muhusika mkuu katika suala zima la matumizi mabaya ya pesa wakati wa utawala wake kama meya wa jiji la Jerusalem na kumfanya alijiudhuru 2008 uwadhifa wake wa uwaziri mkuu, baada ya polisi kuanza matayarisho ya kumfungulia kesi.

Umoja wa mataifa waingia doa na mapambano ya Ukraine.

New York, Marekani - 14/05/2014. Umoja wa Mataifa umekutwa na wakati mgumu wa kujibu maswali baada ya helikopta yenye nembo ya UN kuonekana kutumika katika mashambulizi nchi Ukraini.

Habari kutoka katika ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon zimesema, " nikinyume na sheria kutumia vifaa au helikopta ya umoja wa mataifa katika mapambano yoyote na hii inaleta sura potofu kwa jamii nzima ya kimataifa kuhusu ufanisi wa umoja wa Mataifa."

"Vifaa, ndege na helikopta za Umoja wa Mataifa huwa vinatumika katika kusaidia na kuokoa watu walio katika hali ya hatari na maafa, hivyo serikali ya Kiev imevunja sheria na kwenda kinyume na mkataba wa umoja wa amataifa na tunalaani itendo cha kutumia vifaa vya Umoja wa Mataifa katika mapambano ya kivita."

Hata hivyo waziri wa ulinzi wa  Ukraine imekanusha kutumia helikopta ya umoja wa mataifa katika mapambano yake na wapinzani ambao wanataka kujitenga na serikali ya Kiev, na alipo ulizwa kuhusu helikopta yenye nembo ya UN kuonekana kufanya mashabulizi akili kataa kulizungumzia swala hilo tena.

Helikopta yenye rangi nyeupe Mil Mi-24 imeonekana ikitumika katika mashambuzi ya kuwashambulia wapinzani wa serikali  ya Ukraine, ambo wanapinga uhalali wa serikali ya sasa ambayo iliingia madarakani baada ya mapinduzi yaliyo mng'oa rais Victor Yanukovych  Februari mwaka huu 2014.

Mapambano ambayo yanaendelea nchi Ukraine yamekuwa baada ya majimbo ya Donetsk na Lugansky kupiga kura ya maoni ya kujitenga na serikali ya Kiev, jambo ambalo Kiev inalipinga.

1 comment:

Unknown said...

http://kalajaduu.blogspot.com/