Wednesday, July 9, 2014

Wakuu wa nchi za BRICS kuanzisha benki ya unafuu.

Wakuu wa nchi za BRICS kuanzisha benki ya unafuu.

Moscow, Urusi - 09/07/2014. Nchi  wanachama wanao julikana kama BRICS zinakaribia kuunda benki yake ili kuepukana mvutano wa kifedha na benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa-IMF katika utoaji wa mikopo na riba.

Benki hiyo itajulikana kama Benki mpya ya Maendeleo ambayo imeundwa kwa nia ya kuwa  na kazi ya kutoa mikopo nafuu na kuunda miradi mbali mbali ya kukuza uchumi kwa nchi masikini.

Akiongea kuhusu kuundwa kwa benki hiyo, waziri wa fedha wa Urusi, Anton Siluanov amesema "Benki itaanzishwa kwa mtaji wa billioni 10 kifedha na 40 billion zitakuwepo kwa dharula, na kila mwanachama wa nchi za BRICS atachangia kiasi sawa kifedha."

"Urusi itachangia 2 billion katika kuimarisha benki hiyo kwa muda wa miaka saba ijayo na benki hii itaanza kazi rasmi ifikapo mwaka 2016."Aliongezea waziri Siluanov.

Mazungumzo ya kuanzishwa kwa benki hii mpya ya nchi za BRICS yamekuja kabla ya kikao cha wakuu wa nchi za BRICS kinacho tarajiwa kufanyika nchini Brazil Julai 15-16.

Nchi za BRICS ni Brazilm India, China na Afrika ya Kusini.

Benki hii pia itaruhusu nchi wanachama wa umoja wa Mataifa kujiunga na hazitaruhusiwa kuwekeza zaidi ya asilimia 45

Kuanzishwa kwa benki ya nchi wanachama wa BRICS, kunatoa changa moto kubwa kwa IMF na benki ya dunia, ambapo zimekuwa zikilaumiwa kwa kuwa hazipo kwa aajili ya nchi masikini na zimekuwa zikiweka masharti magumu kwa nchi inayo taka mkopo toka kwa mashirika hayo ya kifedha. 

Nchini Irak siraha za sumu zaangukia mikononi mwa ISIS.
 
Baghdad, Irak - 09/07/2014. Serikali ya Irak, imetoa taarifa kwa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa kuwa eneo lenye siraha za sumu limetekwa na kundi la ISIS linalo pingana na serikali ya waziri mkuu Nour al Malik.


Ujumbe huo wa serikali ya Irak kwa umoja wa mataifa ulikabidhiwa kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon na balozi wa Irak wa umoja wa mataifa Mohamed Al Alkhakim wenye kuandikwa " eneo lenye kuhifadhi siraha zenye sumu la Muthanna limekuwa chini ya kundi la ISIS tangi Juni 11 mwaka huu."

Siraha hizo zenye sumu, ambazo zilitengenezwa  kabla ya vita vya Gulf vya mwaka 1991 na zinasadikiwa kuwa ni roketi 2,500 ambazo zina sumu aina ya sarin na tani 180 za aina tofauti za siraha za sumu ambazo zikitumika zinaweza kuuwa mamia ya watu kwa kuwa na uwezo wa kuharibu misuri ya ufahamu katika mwili wa binadamu.

Naye aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza  Tony Brair aliyeongoza vita vya kuondoa serikali ya Irak iliyokuwa chini ya rais Saadam Husseini, amemtaka waziri mkuu wa Irak Nour al Maliki kubadili mwenendo wake wa uongozi ama kama hawezi ajiudhuru.

Waziri mkuu wa Irak Nour al Maliki amekuwa akilaumiwa kwa kuwa kinara katika kuongoza mgawanyiko wa Wairak, hasa kimakundi ya kidini ya Shia na Suni.


 


No comments: