Wednesday, July 16, 2008

Hezbollah na Israel zatimiziana ahadi" Wabadilishana wafungwa na miili ya wapiganaji wao".

Brad na Angelina wawa baba na mama mapacha au (mapasa) "Picha za watoto kughalimu mamillioni".

Nice, Ufaransa - Mcheza sinema , balozi wa umoja wa mataifa kwa upande wa UNICEF na nyota maarufu duniani bi Angelina Jolie amejifungua watoto mapasa(Mapacha) wakiki na wakiume katika Hospitali ya French Riviera.
Watoto hao mapacha ambao walipishana dakika moja walizaliwa siku ya jumamosi 12/07/2008, jioni walikuwa na paundi 5 kila mmoja.
Watoto hao walioitwa Knox Leon na Vivienne Maecheline
Inatarajiwa picha zao za kwanza huenda zikauzwa kwa bei ya juu zaidi kufika kiasi cha $ 20 million,alisema mmoja wa mpiga picha bwana, Darryn Lyons, anayemiliki gazeti la Big Pictures la London.
Akiongea hay mganga aliyesaidia kuzaliwa kwa watoto hawa mapacha,alisema Brad Pitt alikuwa pembeni wakati Angelina anajifungua.
Pichani wanaonekana Brad na Angelina wakati walipo kuwa katika moja ya sherehe, kwa sasa wanitwa baba na mama MAPASA.
Picha ya pili wanaonekana Brad na Angelina, walipo udhulia pamoja katika maonyesho ya manyota wa dunia kabla ya Angela kujifungua.
Picha ya tatu, anaonekana Angelina akiwa amesimama wakati alipo kuwa mja mzito wa watotomapasa.
Hezbollah na Israel zatimiziana ahadi"Wabadilishana wafungwa na miili ya wapiganaji wao".
Beiruti,Labanoni - Wafungwa watano ambao walikuwa wanashikiliwa na serikali ya Israel kama wauwaji na magaidi leo 16/07/2008, wameachiwa huru na kurudishwa nchini Lebanon na miili ya wanajeshi wa jeshi la Israel kurudishwa nchini Israel, ikiwa ni moja ya makubaliano kati ya serikali ya Israel na kundi la Hezbollah.
Kwa upande wa Labanon ilikuwa ni sherehe na nderemo kwa kuachiwa kwa wapiganaji wao na kwa upande wa Israel ilikuwa ni masikitiko makubwa alisikika msemaji mmoja wa serikali akisema haya.
Miili ya wanajeshi, Ehud Goldwasser na Eldad Regev ambao waliuwawa wakati wa mapambano na Hezbolah.
Hata hivyo kuachiwa kwa wafungwa hao watano,kuliambatana na kutolewa kwa miili ya wapiganaji wa Hezbollah na Palestina ambao waliuwawa wakati wamapigano kwa kipindi tofauti na jeshi la Israel.
Pichani hapo juu anaonekana viongozi wa Hezbollah wakiwa na wanachama wao wakishangilia kuachiwa kwa wapiganaji wao.
Picha ya pili ni moja ya jeneza lililo beba mwili wa mmoja wa wapiganaji wa Hezbollh akitolewa ili kukabidhiwa kwa uongozi wa Hezbollah.
Picha ya tatu, wanaonekana badhi ya ndugu wa wanajeshi wa Israel wakilia kwa uchungu, mara baada ya kukabidhiwa miili ya wapiganaji wao.
Wazambia na chama cha upinzani wataka kujua kiundani kuhusu afya ya rais"Wapinzani"
Lusaka, Zambia - Chama kikuu cha upinzani nchini Zambia Patriotic Front(PF) kimetaka uwepo uwazi wa maelezo ya afya ya rais Levy Mwanawaswa kama bado kama anauwezo wa kuongoza nchi.
Akiongea haya, kiongozi wa wa chama hicho bwana, Michel Sata,amesema hawaamini taarifa ya serikali inayo sema hali ya afya inaendelea vizuri.
Rais, Levy Mwanawaswa mwenye miaka 59,amelazwa katika hospitali mjini Paris baada ya kupata ugonjwa wa kiarusi wakati alipo udhulia mkutano wa umoja wa Afrika nchini Misri. Picha ya hapo juu ni anaonekana rais Levy Mwanawasa, alipokuwa akihutubia balaza kuu la umoja wa mataifa.
Picha ya chini anaonekana rais,Levy Mwanawaswa, akikagua mradi wa maji safi hivi karibuni kabla ya kwenda kwenye mkutano nchini Misri.
Kampuni na serikali bado kuvutana" Waadhulika walitakakupewa malipo madogo".
Kano,Nigeria - Kampuni ya madawa ijulikanayo kama Pfizer imetangaza yakuwa mazungumzo kati ya srikali ya Nigeria umevunjika hivi karibuni.
Akiongea haya, wakili wa kampuni hii ya madawa Pfizer, alisema mkutano huu ulioudhuliwa na waziri wa sheria wa Nigeria na wakili mkuu bwana, Michel Andoakaa ,na mwakilishi wa wadhulika bwana, Alhaji Maisikeli.
Mwakilishi wa wadhulika alisema, mkutano huu haukufikia makubaliano,kwani kampuni ya Pfizer likuwa imetoa malipo ya kiasi cha $21million kwa maswala ya sheria na waathirika 200 kupata jumla ya $10million, na ni jambo ambalo haliwezekani, kwani watu waliotumia dawa hii aina ya "Trovan" kama majaribio mwaka 1996,walidhulika na wengine kupoteza maisha.
Picha ya picha ya bendera ya Nigeria.
Picha ya pili ni picha ya baadhi ya na dawa amabyo hutumiwa na binadamu karibu kila siku.
Afrika yawa na njia mbili kuhusu kukamatwa kwa rais wa Sudani.
Addis Ababa - Ethiopia - Umoja wa Afrika umeonya vikali yakuwa kitendo cha kumshitaki rais wa Sudan bwana, Omar Al-Bashir, kunaweza kuatarisha hali halisi ya usalama nchini Sudan hasa kwenye eneo la Darfur.
Na Umoja huu wa Afrika, umesema pia kushitakiwa huku kwa rais, Omar Bashir kunaweza kuwa ni njia moja ya kuanza kuwatishia viongozi wa Afrika kwa kutimika nguvu za mahakama pasipo kihalali hasa panapo kuwepo na swala la kisiasa.
Kushitakiwa kwa rais Bashir,kulitamkwa rasmi na wakili wa mahakama ya Hague bwana, Luis Moremo Ocampo, (ICC) wakati alipo kuwa akieleza mashitaka yanayo mkabili rais, Omar Al Bashir.
Mashitaka hayo yanayo muhusu rais Omar Al Bashir, ni kukiuka kwa haki za kibinadamu kwa serikali yake na vita vilivyo leta mauaji mauaji katika eneo la Darfur.
Hata hivyo Umoja huu wa Afrika , unapinga kukika kwa haki za binadamu katika nchi wanachama wake.
Juu ni picha ya alama ya mahakama, ambayo hutumika kutafutia haki kwa wale wanao onewa.
Picha ya pili anaonekana rais, Omar Al-Bashir akiwapungia mikono baadhi ya watu waliokuja kumuunga mkono kwa kupinga kushitakiwa kwake na mahakama ya mjini Hague.
Picha ya tatu wanaonekana baadhi ya watu wapatao maelfu ambao wanaathirika na kupata taabu kutokana na mgogoro unao kabiri eneo la Darfur.

No comments: