Tuesday, July 22, 2008

Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini atolewa katika majina ya magaidi" Yupo huru kuingia Amerika"

Makelele asema sasa Uingereza basi"Arudi nyumbani".

Paris, Ufaransa - Mchezaji mairi na nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa Claude Makelele, ametia saini mkataba wa kuchezea timu ya Paris ST Germain siku ya jumatatu 21/07/2008.
Hata hivyo makubaliano ya mkataba huo hayakuelezwa na vingozi wa timu PSG.
Hata hivyo kwa muujibu wa meneja wa Makelele, alisema nia ya Claude ni kucheza maika mingine miwili zaidi kabla ya kutundika madaruga juu.
Akiongea, Makelele alisema ya kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuweza kufanya kazi yake kama alivyo siku zote awapo kazini - Uwanjani.
Makelele mwenye miak 35, ambaye amechezea timu kubwa na maarufu duniani kama, Rael Madrid na Chelsea , alisema ni furaha kubwa kuja kuchezea timu ya Pars St Germain.
Picha ya hapo juu anaonekana Claude Makelele awapo kazini hana masihara, hata mkija wangapi ata shinda tu.
Picha ya pili anaonekana Makelele, akikokota kandanda huku mmoja ya wa chezaji wa timu ya Arsenal akijaribu bila mafaniko kumnyanganya kandanda hio .
Chini anaonekan Claude Makelele akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni wakati timu ya taifa ya Ufaransa ilipo kuwa ikijianda na kombe la mabingwa wa Ulaya.
Mmoja wa mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya alaiki akamatwa.
Serbia, Bosnia - Mmoja wa viongozi walioshukiwa kuhusika na mauaji ya watu wa Sarajevo na Serbia, ambaye alikuwa ni rais, wa Bosnia Radovan Karadzic amekamatwa siku ya 18/07/2008 ijumaa wiki ikiyo pita, kwa mujibu wa msemaji wa serikali.
Karadzic mwenye miaka 63, ashutumiwa kwa kutoa amri ya mauaji ya watu wasiopungua 8000, waumini wa dini ya kislaam katika kitongoji cha Srebrenica.
Kukamatwa kwa bwana Radovan Karadzic, kulitokea mnamo majira ya tatu na nusu usiku 21:30.
Hata hivyo bwana Radovan Karadzic, anatarajiwa kufikishwa mahakamani na baadaye huenda akapelekwa mjini Hague Uholanzi kujibu mashitaka ya nayao mkabili ya kivita na kuhusika na mauaji.
Pichani hapo juu anaonekana bwana, Radovan Karadzic wakati alipo kuwa raisi wa Bosnia, akionyesha maeneo fulani kwenywe ramani.
Picha ya pili wanaonekana baadhi ya wakaazi wa Sarajevo wakishangilia kukamatwa kwa bwana Radovan Karadzic.
Picha ya mwisho anaonekana, Radovan Karadzic kulia akiwa amefuga ndevu ambazo zilimsaidia kutojulikana kwa muda mrefu hadi alipo kamtwa hivi karibuni na picha ya kushoto anaonekana Radovan Karadzic kabla ya kufuga ndevu wakati huo alipo kuwa kiongozi wanchi..
Biashara ya umalaya yaleta kitendawili ''Viongozi wavutana"Afrika ya Kusini
Durban, Afrika ya Kusini -Serikali ya Afrika ya Kusini huenda ikaidhinisha biaashara ya umalaya wakati wa mashindano ya kugombania kutafuta bingwa wa soka wa kombe la dunia litakalo fanyka 2010 chini Afrika ya Kusini.
Kwa mujibu wa msemaji wa hamashauri ya jiji la Durban, alisema yakuwa wanajdili na serikali ni jinsi gani watashrikiana, hasa katika majumba ya starehe na maeneo mengine ya jiji la Durban.
Hata hivyo viongozi wa kidini jijini humo, wanapinga mpango huu kwani unakwenda kinyume na maadili ya dini na huenda ukawa wakudumu.
Picha hapo juu ni za baadhi ya watu ambao huwa wanafanya bishara ya umalaya nchini Afrika ya Kusini.
Raia wa Kipalestina aendesha gari aina ya katapilla na kujeruhi wengi.
Jerusalemu, Izrael - Dereva mmoja wa katapilla ambaye ana asili ya kiarabu ameuawawa na polisi nchini Izrael kwa kuliendesha gari aina ya katapilla kwa kwa fujo na kuanza kugonga magari na basi siku ya jumanne 22/07/208.
Dereva huyo amesababisha ajali kwa watu wasiopungua 20.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, tukio kama hili ni la pili kutokea katika mazingira tofauti.
Polisi wamesema ya kuwa dereva huyo, ambaye alijulikana kama Ghassan Abu Teir, ambaye ni raia wa kipalestina ambaye alikuwa anaishi mjini Jerusalem.
Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini atolewa katika majina ya magaidi."Yupo huru kuingia Amerika".
Washington, Amerika - Rais, George Bush hivi karibuni ametia sahii ya kutaka rais wazamani wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela kufutwa na kuondolewa katika majina ya watu wanajulikana kama magaidi.
Kufutwa kwa rais wazamani wa Afrika ya Kusini katika majina ya watu wanaojulikana kama magaidi kutamwezesha bwana, Nelson Mandela kutembelea Amerika bila kupata ruhusa ya ofisi kutoka ofisi ya mambo ya nje ya nchi ya Amerika.
Kuwekwa kwa jina la rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, kulikuja baada ya chama cha kutete haki za wengi nchini Afrika ya Kusini ANC, wakati wanachama na viongozi wa chama hiki walipokuwa wanapinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini dhidi ya makaburu.
Picha ya hapo juu wanonekana rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela na mke
wake bi Winnie wakati Nelson Mandela alipokuwa anawasalimia wanchi kwa mara ya kwanza mara baada ya kuachiwa huru kutoka jela, ambapo alitumikia kifungo cha miaka 27 kwa ajil;i ya kupinga ubaguzi warangi nchini Afrika ya Kusini.
Picha ya chini anaonekana rais George Bush akiwa anaongea na waandishi wa habari.
Waachiwa baada ya kutumikia kifungo kwa kosa la kuwa na madawa ya kulevya.
Akkra, Ghana - Wasichana wawili raia wa Uingereza waliachiwa huru, baada ya kutumika kifungo cha miezi tisa kwa kosa la kutaka kupitisha madawa ya kulevya nchini Ghana kwa kutumia kichakato au (kompyuta) ndogo. Msemaji wa serikali, bwana John Allotey alisema yakuwa wasichana hawa waliachiwa huru na hakuweza kueleza kwa undani zaidi.
Wasichana hawa wakikamatwa kwenye kiwanja cha ndege cha jijini Akkra julai 2007 wakiwa na madawa aina ya kokeini kilo 6 ndani ya (michakato)- kompyuta zao.
Picha hapo juu ni picha ya moja ya madawa ya kulevya ambayo yamekuwa yakisadikiwa kupitia nchi nyingi za Afrika hasa nchi za Afrika ya Magharibi.
Washukiwa wa ugaidi uliyo fanyika nchini Uispania waachiwa huru.
Madrid,Spain - Mahakama kuu ya Uispainia imewachia huru hivi karibuni watu walioshukiwa kuhusika na ulipuaji wa kigaidi uliofanyaka nchini Uispania mwaka 2004, ambapo zaid ya watu wasiopungua 191 walipoteza maisha.
Watu hawa wanne, ni kati ya watu 21 ambao wakikamatwa kwa kushukiwa kuhusika na ugaidi huo.
Kuachiwa kwa watu hao kuliambatana na kuachiwa kwa Rabie Osman Sayed Ahmed ambaye alikuwa anashukiwa kuhusika na katika kusaidia ugaidi ambo ulipoteza maisha ya watu na kujeruhi watu wasiopungua 1,800.
Pichani hapo juu anaonekana bwana Ahamed wakati alipo kuwa ndani ya mahabusu ya mahaka kabla kusikia kesi yake.

No comments: