Wednesday, July 30, 2008

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa ukimwi duniani wapungua"Umoja wa mataifa"

Mkutano wa Kiuchumi wavunjika Geneva"Pigo kwa uchumi wa dunia OXFAM " Doa yawa ndoto"

Geneva , Uswis - 30/07/08. Mazungumzo ya kuletaunafuu katika biashara na kilimo yaliyo kuwa yakifanyika Geneva yamevunjika baada ya nchi za, Amerika, China na India kutofikia maafikiano na kuzika mandhumuni ya mkutano wa Doa,Katar,liofanyika miaka saba iliyo pita.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa WTO - World Trade Organisation, bwana Pascal Lamy, alisema nchi hizi zimeshindwa kufikia maafikano na hivyo kusababisha mkutano kuvunjika bila kuwa na mafanikio.
Hata hivyo, bwana Pascal Lemy, alisema kuvunjika kwa mkutano huo, siyo kusikatishe tamaa, kwani bado kuna matumaini ya hapo baadaye nchi hizi zikifafika makubaliano.
Kufuatia kuvunjika kwa mkutano huo, kamishna wa biashara wa jumuia ya Ulaya, bwana Peter Mendelson, amesema kuvunjika kwa mkutano huu kumeleta uchungu,na hasa katika kuinua uchumi wa dunia.
Naye mkurugenzi wa OXFAM International, bwana Jeremy Hobbs, alisema hii ni pigo kwa dunia na inasikitisha kwani, kuvunjika kwa mkutano huu , kumekuja wakati chakula na mafuta vinazidi kupanda bei na italeta hali mbaya ya kiuchumi duniani.
Kuvunjika kwa mkutano huu, kumeonyesha ni jinsi gani nchi tajiri na masikini duniani, zinavyo vutana katika maswala ya kimaslahi, alisema mmoja wa wajumbe walioudhulia mkutano huu.
Picha hapo juu anaonekana mkurugenzi mkuu wa WTO,bwana,Pascal Lamy akiwa ahamini yakuwa mkutano umevunjika bila kuleta mafanikio ya kiuchimi kwa dunia.
Chini ni picha ya anaonekan mmoja ya wakulima wa nchi za dunia ya tatu, akilima kishamba chake, tayari kuuza mazo ili apate pesa, lakini kudumu kwa kilimo chake kunategemea saana mikutano kama huu ulio vunjika,ambapo angepata nafuu ya pembejeo na soko la kuuza bidhaa zake.
Picha ya mwisho mwanaonekan majumbe, walioudhulia mkutano mjini Geneva, wengine wamesimama na wengine wamekaa , na kuashiria ya kuwa hali katika mkutano huu , mambo yalikuwa ya vuta ni kuvute.
Idadi ya vifo vinavyo sababishwa na ugonjwa wa ukimwi duniani wapungua"Umoja wamataifa ".
Umoja wa mataifa, New York - 30/07/08. Umoja wa mataifa umesema vifo vinavyo sababishwa na ugonjwa wa ukimwi vimekuwa vichache kulinganisha miaka ishirini iliyo pita.
Ripoti hii ilitolewa katika mkutano wake wa mwaka, ambao ulikuwa ukitathmini hali halisi ya ugonjwa huu wa ukimwi, na jinsi ya kuukabilina nao tangu ulipo anzaa kuongezeka mapema miaaka ya 1990.
Hata hivyo, Umoja wamatifa , umeziagiza serikali kuzidi kupupambana na ugojwa huu kwa kuwekwa fungu la fedha za kutosha ili kuokoa maisha ya watu wengi.
Ofisi zinazo shughulika kupambana na ugonjwa wa ukimwi, zilizopo nchini Uswis -Geneva, zimesema yakuwa idadi ya vifo vya wagonjwa wa ukimwi vimepungua hadi kupunga kwa kiasi cha 200,000, kulnganisha miaka mitatu iliyo pita.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa (NAids), Peter Piot,alisema yakuwa hadi hivi sasa kuna watu wapatao million 33 duniani ambao wanaishi na virusi ya ukimwi.
Akiongezea kusema , mkurugenzi huyu Piet Pot, alisema yakuwa tangu 2007 , watu wapatao million 3 wanatumia vidonge , kulinganisha na mwaka 2003, na hii inatokana na madawa kwa rais kupatikana na kuuzwa kwa bei nafuu.
Picha hapo juu ni picha ya virus vya ukimwi ambavyo uhathili aafya ya mtu,pindipo vinapo ingia ndani ya mwili na hasa ukiwa huja pata matibabu au kuanza kutumia madawa na kula lishe bora.
Picha ya pili ni picha alama ya Ukimwi (AIDS) ikiwa imechorwa katika moja ya ofisi zinazo shughulika Ugonjwa huu.
Hali ya usalama nchini Irak bado ya kusuasua" Wengi wajeruhiwa ".
Bagdad, Irak -28/07/08. Watu wapao 28 wamepoteza maisha yao na wengine 92 kijeruhiwa vibaya, wakati wanawake watatu walipo jilipua katika kadamnasi ya watu waliokuja kuhiji kushereheka siku ya kidini ya watu wenye madhehebu ya Kishia.
Kwa mujibu wa masemaji wa serikali alisema yakuwa wanawake hawa walikuwa katika kundi la mahujaji na walipo jililipua walisabisha maafa makubwa ya watu kupoteza maisha na kujeruhi watu wengi.
Picha hapo juu, anaonekan mmoj wa wanajeshi wa Amerika akiwa kazini kulinda usalama wa raia wa Irak.
Picha yapili anaonekana mzee wa Kiirak, akiangalia kwa uchungu miili ya watoto wadogo, waliopoteza maisha yao, baada ya mabomu kulipuka na kisababisha maafa makubwa katika jamii ya Wairak.
Picha ya tatu anaonekana raia mmoja wa Irak , akiwa anaondoka kwenye eneo ambalo limetoke mlipuko huku akiwa anamajeruha kwenye uso wake na damu zikimtoka wakati akitembea.
Polisi wa Irak, wanaonekana wakijaribu kuashiria kuomba msaada kuzimisha moto ambao umesababishwa na mlipuko wa wabomu.
Uchimbaji wa mafuta Niger Delta hali ni ngumu"MEND wadai watendelea na uharibifu".
Niger Delta , Nigeria - 28/07/08. Kukundi kinajulikana kam( MEND au Movement for Emancipation of the Niger Delta), kimedai yakuwa kimeharibu mitambo na mabomba ya kupitishia mafuta ya nayo milikiwa na kampuni ya Shell.
Kikundi hicho kilitoa maelezo hayo kwa kupitia barua pepe na kudai kitaendelea na mashambulizi yake ikiwa akitapatiwa mahitaji yake kutoke serikalini.
Kampuni ya shell, ilianza kuchimba na kusafirisha mafuta katika kitongoji cha Bonga mwaka 2205, hadi kufikia 2007 zaidim ya mapipa million 100 yalikuwa yamesha safilishwa kutoka eneo hili, ambali lipo km 120 kwenye maeneo ya ufukwe wa bahari.
Pia eneo hili lina gasi lenye ulefu wa kubic 150 millioni.
Pichani hapo juu ni wapiganaji wa kikundi cha MEND wakiwa ndani ya boti huku wakizunguka maeneo ambayo yana mafuta.
Picha pili ni ya boti inayo tumiwa na MEND.
Hatimaye bwana Radovan Karadzic awasili mjini Hague tayari kukabiliana na mashitaka yanayo amkabili" Hataki kuwakilishwa na mwana sheria".
Hague, Uhollanzi - 30/07/08. Aliyekuwa kiongozi wa Bosnia - Serbia, bwana Radovan Karadzic, amewasilishwa leo nchini Uhollanzi tayari kwa kukabiliana na mashitaka yanayo mkabili dhidi yake.
Mashitaka hayo ambayo yanamkabili bwana,Radovan Karadzic, ni ya yale yanayoambatanishwa na vita vilivyotokea Bosnia mwaka 1992 - 1995, na ni kwanza tangu kumalizika vita vya pili ya dunia katika bara la Ulaya.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa mahakama ya kimataifa ya mjini Hague,alisema yakuwa bwana, Radovana Karadizdic atafikishwa mahakamani hivi karibuni,ili kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Mashitaka yanayo mkabili bwana Radovan Karadzic, ni ya mauaji ya ya zaidi ya watu 8,000 waumini wa dini ya Kiislaam katika kitongoji cha Srebrenika.
Hata hivyo, kwamujibu wamsemaji wa bwana, Radovan Karadzic,alisema yakuwa bwana Karadizic atajitetea peke yake na hataki kuwawakilishwa na mwana sheria yoyote katika kujibu mashitaka yake.
Pichani hapo juu anaonekana bwana Radovan Karadzic, enzi hizo alipo kuwa kiongozi wa Serbia , akiongea na baadhi ya viongozi wenzake.
Picha ya pili ni chumba ambacho, inasadikiwa bwana,Radovana Karadzic atakuwa anaishi wakati kesi yake ikiwa inaendelea.
Picha ya tatu wanaonekana polisi wakipambana na baadhi ya wananchi wa wapenzi mjini Bergedi, Yugoslavia wakiandamana kupinga kukamatwa na kupelekwa kwa bwana, Radovan Karadzic mjini Hague, tayari kusikiliza kesi zinazo mkabili dhidi yake.
Picha ya tatu, inaonekana helkopta iliyombebe bwana Radovan Karadzic ikitua ndani ya gereza mjini Hague,kwenye gereza hili ndimo bwana, Radovan Karadzic, atakaa kwa kipindi chote atakapo kuwa akisikiliza kesi yake.
Pichani anaonekana kaka ya bwana, Radovan Karadzic, akijitahidi bila mafanikio kuwasialiana na wanasheria na wana ndugu, iliwajaribu kuzuia kupelekwa kwa kaka yake nchini Uhollanzi kujibu mashitaka.

No comments: