Tuesday, July 8, 2008

Rais, Paul Kagame aionya Ufaransa"Rwanda sasa ni miaka 13 imepita.

Uwanja wa Nelson Mandela hautakuwa tayari kwa mashindano ya mabingwa wa soka wa mabara sita"Yasema kamati"

Port Elizabeth, Afrika ya Kusini - Uwezekano wa kuwa tayari moja ya uwanja utakao tumika kutimula daruga na gozi la ngombe lililo la mviringo ili kutafuta bingwa wa mabara yote sita ya dunia kwa upandea wasoka upo mashakani.
Mashindano haya yalianzishwa mwaka 1992 hadi 1995, kama mashindano ya kugombea kikombe cha Mfalme Fahd,ambapo zilialikwatimu kutoka nchi tofauti kupambana timu ya taifa ya Saudi Arabia.
Ndipo mwaka 1997, ndipo FIFA, shirikisho la soka duniani kulitambua rasmi na kuanza kugombaniwa na mataifa mabingwa wa mabara yote sitakabla ya kuanza kwa fainali za kugombea kombe la dunia..
Kwamujibu wa mwenyeki bwana, Ivin Khoza, na kamati inayo simamia ubora wa viwanja hivi nchini Afrika ya Kusini, amesema huenda uwanja wa Nelson Mandela ulipo mjini Port Elizabeth hautatayari kwa kuchezea mashindano hayo.
Hata hivyo huwanja huo utakuwa umekamilika ifikapo 2010, tayari kwa mashindano ya kugombea bingwa wa soka wa Dunia.
Picha hapo juu anaonekana bwana Danny Jordan, ambaye alipigania kwa kila hali hadi Afrika na Afrika ya Kusini kuweza kupewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa kombe la dunia kwa mara ya kwanza.
Picha ya pili inaonyesha pilika za ujenzi wa kiwanja vinaendelea, hapo nimoja ya kiwanja kikiwa kinajengwa tayari kwa soka la dunia.
Chini ni picha ya bwana Ivin Khoza, ambaye ni mmoja ya wajumbe na viongozi wanao simamia ujenzi na maandalizi ya viwanja vitakavyo cheze wa soka ili kupata bingwa wa soka 2010 nchini Afrika ya Kusini.
Rais, Paul Kagame aionya Ufaransa" Rwanda sasa ni miaka 13 imepita".
Kigali, Rwanda - Rais wa Rwanda Paul Kagame, amesema yakuwa huenda ikaishitaki serikali ya Ufaransa kwa kuhusika kwake katika mauaji ya yaliyo tokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Rais Kagame alisema yakuwa, ikiwa serikali ya Ufaransa aitafutilia mbali madai ya kuwashitaki baadhi ya viongozi wa serikali ya Rwanda katika mahakama za Ulaya.
Rais, Kagame alisisitiza kwa kusema yakuwa , uchunguzi uliofanywa umeonyesha ya kuwa Ufaransa ilihusika katika vita vilivyotokea nchini Rwanda vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jamii ya watu wa kihutu na wakitutsi, na kusababisha maisha ya watu wasiopungua 800,000 kupoteza maisha yao wengi wao wakiwa watu kutoka jamii ya Kitusti.
Picha hapo juu anaonekana rais, Paul Kagame wa kwanza kushoto,akielekea kwenye mnara wa kumbukumbu ya mauaji ya mwaka 1994 ulipopo Murambi, huu ni mwaka wa kumi natatu tangu mauaji haya kutokea.
Picha ya pili wanaonekana rais, Paul Kagame na mke wake mama Jannette Kagame wakiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya mauaji ya yaliyo tokea nchini Rwanda mwaka 1994.
Picha ya tatu anaonekan rais, Paul Kagame, akihutubia wananchi waliokuja kuadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu ya mauaji ya watu wasiopungua 800,000, wananchi wa Rwanda.
Mugabe bado hawa shubiri kwa jumuia ya kimataifa"Afrika haya nia ya Wazimbabwe wenyewe."
Hakaido Toyako, Japan - Kundi la nchi tajiri zijulikanazo kama, G8 zimekubaliana kwa pamoja kwa kulaani hali ya kisiasa nchini Zimbabwe, na kuhaidi kuweka vikwazo kwa viongozi na wale watu wote walio usika katika kuleta mgogoro wa kisiasa nchini Zimbabwe.
Hata hivyo viongozi wa Afrika walio udhulia mkutano huu, walipinga na kusema swala la kuiwekea vikwazo Zimbabwe hakutasaidia kubadilisha matokea ya uongozi nchini Zimbabwe.
Viongozi hao wa Afrika, wakiongozwa na na mwenyekiti wa Muungano wa nchi za Afrika (AU), rais wa Tanzania bwana Jakaya Kikwete, walisema yakuwa swala la Zimbabwe waachiwe Wazimbwe wenyewe.
Hata hivyo,msemaji wa serikali ya serikali ya Zimbabwe,alisema ya kuwa kuwa uamuzi wa (G8) nchi tajiri duniani ni wakibaguzi, kwani serikali ya Zimbabwe imefanya ilichokuwa ikipigania tangu hapo mwanzo kurudisha ardhi kwa wananchi Wazimbabwe.
Picha hapo juu ni picha ya rais wa Zimbabwe bwana Robert Mugabe, ambaye amekuwa shubiri katika jumia ya kimataifa hasa bara la Ulaya na Amerika.
Chini ni picha ya viongozi wa nchi tajiri duniani walioudhulia kikao kilicho fanyika nchini Japan 2008.
Haini afungwa miaka 34,"Adhabu kali ndiyo mfano kwa wale wenye mawazo kama haya".
Malabo, Guinea Ikweta - Mtuhumiwa ambaye anahusika katika njama za kutaka kupindua serikali ya Guinea Ikweta bwana Simon Mann, amehukumiwa kwenda jela miaka 34 na miezi minne, baada ya kukutwa na hatia.
Hukumu hiyo ilitolewa siku ya tarehe 7/july/2007, bwana Simon Mann, alisema yakuwa yeye mwenyewe alikuwa siyo muhusika mkuu, bali kulikuwa na wakubwa wake , hata hivyo mahakama ya mjini Malabo haikujali malalamiko yake na kumpa adhabu kali kuwa mfano kwa wengine wenye mawazo hayo, alisikika akisema mmoja wa wasemaji wa serikali.
Guinea Ikweta, ni nchi moja wapo katika bara la Afrika, ambayo ni nchi iliyo na utajiri wa mali ya asili kama mafuta na gasi ambazo huuzwa katika nchi za Ulaya na Amerika.
Picha hapo juu ni picha ya rais wa, Guinea Ikweta bwana Teodoro Obiang Nguemo,amabye serikali yake ilitaka kupinduliwa na kundi la bwan Simon Mann.
Chini wanaonekana bwana, Simon Mann kushoto akiwa na mwenzake ambao walihusika katika jaribio la kutaka kupindua serikali, siya kwanza walipo kuwa wanaenda mahakamani kusikiliza kesi yao ya uhaini.
Jean Piera Bemba, asikiliza kesi yake kwa mara ya kwanza" Hati ya kukamatwa kwake ilikuwa siri".
Hague, Uhollanzi - Mahakama kuu inayo shughulikia makosa ya nayotokana na kukiuka haki za binadamu na makosa ya jamii iliyopo nchi Huollanzi hivi karibuni ilianza kusikiliza kesi ya bwana, Jeans Piere Bemba ambaye pia ni makamu wa rais wa Jamuhuri ya Kongo.
Kukamatwa kwa bwana, Jean Piere Bemba, kumekuja mara baada ya kuingia nchini Ubeligiji kutembelea ndugu zake, na hapo alikamatwa na polisi na kupelekwa nchini Uholanzi kujibu mashitaka dhidi yake.
Kwa mujibu wa msemaji mmoja wa mahakama ICC ya Hague, waraka wa kukamatwa kwa bwana, Jean Piere Bemba ilikuwepo toka zamani na ilikuwa imefanywa siri tangu kupitishwa kwake.
Juu ni picha ya bendera ya Umoja wa Mataifa ambayo ndiyo mama wa kila nchi.
Picha ya kati anaonekana bwana, Jean Piere Bemba aalipo kuwa mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake.
Picha ya tatu ni moja ya alama inayo onyesha jinsi gani mahama ya Hague, ilivyo zingirwa na kazi kubwa ya kutafuta haki kwa wale waasilika na matukio ya tofauti ya dunia.
Uturuki ni nchi muhimu kwa ulinzi na usalama wa Ulaya"Mkurugenzi wa NATO"
Brussels,Ubeligiji - Mkurugenzi mkuu wa Shirikisho la Ulinzi la nchi za Ulaya NATO, bwana Jaap Hoop Scheffer,amesema hipo haja ya umoja huo kufanya kila njia kushirikaiana na serikali ya Uturuki ili kuimarisha ushirikiano zaidi.
Bwana, Jaap Hoop Scheffer, alisema yakuwa ipo haj kubwa sana ya kuialika Uturuki katikajumuia ya ulinzi na usalama wa Ulaya.
Na mkurugenzi wa NATO alisema hii itaimarisha kuimarika kwa jumuia hiyo.
Picha hapo juu ni picha ya bendera ya Uturuki nchi ambayo ina itajika kwa kila hali katika swala la ulinzi wa Ulaya.
Kati ni alama ya NATO.
Chini anaonekana mkurugenzi mkuu wa NATO bwana Jaap Hoop Scheffer akiongea hivi karibuni kataika moja ya mikutano ya NATO.
Amerika yatiliana mkataba na Cezch kujenga mitambo ya ulinzi.
Prague, Czech - Serikali ya Amerika na Serikali ya Czech zimetiliana mkataba wa kujenga rada kwa ajili ya matumizi ya kijeshi na ulinzi.
Makubaliano haya ni moj ya mipango ya serikali ya Amerika kuweza kujenga mitambo ya kulinda ulinzi katika maeneo ya Ulaya na maeneo mengine.
Hata hivyo serikali ya Amerika imekuwa ikisisitiza ya kuwa kuwekwa kwa mitambo hii kutasaidia kulinda pindipo nchi za Ulaya zikishambuliwa na nchi kama Iran, ikiwa nchi ya Iran itaweza kutengeneza mizinga/siraha ifikapo mwaka 2015.
Picha hapo juu anaonekana bi, Condeleeze Rice anaye shughulikia maswaya ya mambo ya nje ya nchi akitia saini mkataba wa kuwekwa kwa mitambo ya kijeshi nchini Cezch.
Picha chini wanaonekan bi Condeleeze Rice na waziri mkuu wa Cezch bwana, Mirek Topolanek wakionyesha vitabu ambavyo wamaetilana ambavyo mkataba wa kujengwa kwa mitambo ya kijeshi nchini Cezch.

No comments: