Wednesday, July 16, 2008

Uchunguzi wa kifo cha bi,Benazir Bhutto kuanza "Umoja wa matifa"

Wachezaji lazima watimize makubaliano na timu zao "Pele"

London,Uingereza - Mfalme wa soka duniani Pele,amesema hivi karibuni yakuwa ni lazima wachezaji watimize na kutekeleza mikataba ambayo wamekubaliana na timu zao.
Pele,aliongezea kwa kusema yakuwa kauli ya kiongozi wa shirikisho la soka bwana, Sepp Blatter ya kuwa wachezaji wanakuwa kama watumwa ni kauli isiyo kuwa ya makini.
Picha hapo juu anaonekana mfalme Pele, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni.
Chini anaonekana Pele, akiwa ameshikilia moja ya nishani ambazo amekuwa akitunikiwa kutokana na umaili wake kwenye soka miaka ya nyuma.
Picha ya pili anaonekana, mfalme wa soka duniani, Pele akishangilia baada ya kufunga moja ya magoli ambalo liliifanya Brazil kuwa bingwa wa soka duniani mara ya tatu wakati wa enzi zake.
Chavez na Uribe wakutana mjini Caracas"Uhusiano utaimarika tena wasema marais hawa".
Caracas, Venazuela - Rais wa Venezuela bwana Hugo Chavez amekutana na rais wa Kolombia bwana, Alvaro Uribe.
Katika mkutano huu viongozi hawa walizungumzia ni jinsi gani wataweza kujenga na kudumisha uhusiano wao upya ambao ulikuwa si mzuri kwa kipindi kilefu.
Kwa upande wake rais Uribe , alisema yakuwa mkutano huu na rais Chavez,umefungua upya uhusiano wa nchi hizi mbili.
Hapo juu wanaonekana rais wa Kolombia bwana,Uribe akipunga mkono na rais Charvez akiwa amesima karibu, wakati rais,Uribe alipo wasili nchini Venezuela.
Chini wanaonekana rais Chavez , akiongea kitu fulani kwa rais wa Kolombia Alvaro Uribe.
Uchunguzi wa kifo cha bi,Benazir Bhutto kuanza"Umoja wa mataifa".
Islamabad, Pakistan - Umaoja wa mataifa umesema ya kuwa uchunguzi wa mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Pakistani, bi Benazir Bhutto.
Kukubalika kwa uchunguzi huo, kumekuja baada ya katibu mkuu wa umoja wa Mataifa bwana Ban Ki - Moon kukutana na waziri wa mabao ya nchi za nje wa Pakistan bwana ,Shah Mahamood Qureshi.
Kwa kusisitiza swala hili , bwana Shah Qureshi , alisema ya kuwa serikali ya Pakistani itatoa kila msaada katika kukamilisha uchunguzi huu wa mauaji ya bi Benazir Bhutto.
Picha ya kwanza , anaonekana bi Benazir Bhutto akiwa kwenye gari wakati wa kampeni ya kuimarisha chama chake, siku chache kabla ya mauaji yake. Picha ya pili, anaonekana bi,Benazir Bhutto na mumewe,wakati walipo kutana na rais wa zamani wa Palestina,hayati Yasir Arafat.
Picha ya tatu anaonekana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, akiandika rambi rambi za serikali ya Amerika baada ya kifo cha bi Benazir Bhutto.
Chini picha ya mwisho, wanaonekana baadhi ya wapenzi na ndugu wa hayati bi Benazir Bhutto, wakiomboleza baada ya kifo cha bi Benazir Bhutto.
Amani ya Mashariki ya Kati ipo karibu "Asema waziri mkuu"
Paris, Ufaransa - Rais wa Ufaransa bwana, Nicholas Sarkozy amezungumza na viongozi wa Izrael na Palestina wakati wa kufunguliwa kwa mikutano ushirikiano wa nchi za ukanda wa Mediteranian uliofanyika katika jiji la Parisi.
Katika mkutano huo, viongozi hawa aliongea kwa pamoja ni amani tu, itakayo leta uelewano na ujirani mwema kati ya Israel na Palestina.
Akisisitiza hayo waziri mkuu wa Izrael kwa kusema ya kuwa hii inaonyesha yakuwa amani ya mashariki ya kati ipo karibu, na hasa kati ya Waizrael na Wapalestina.
Pichani hapo juu ni wanaonekana viongozi wa Israel kulia bwana Ehud Olmert , kati ni rais wa Ufaransa Nicholas Sarkozy na rais wa Parestina bwana Mohmoud Abbas, wakati walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Picha ya pili anaonekana rais Nicholas Sarkozy, akipita na gari wakati wa sherehe ya kitaifa iliyo hudhuliwa na viongozi wa jumuia ya mwakanda wa Mediteraniani.
Kanisa Katoliki kuomba radhi tena kwa matukio yaliyofanywa kutumia jina la kanisa.
Sydeney, Australia - Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedict, amewasili nchini Australia siku ya tarehe 13/07/2008 tayari kunza ziara yake ya kidini.
Katika ziara hiyo Baba Mtakatifu, amesema yakuwa atawaomba radhi wale wote waliotendewa vibaya na baadhi ya wafanyaka au naviongozi wa dini wa dhehebu la katoliki.
Akiongea hayo , Baba Mtakatifu, alisema ni muhimu kwa Kanisa kukubali na yakuwa kuna mambo mabaya yalitendeka kwa kutumia jina la Kanisa Katoliki na hivyo ni lazima kanisa lifanye kila njia kuweka sawa na kuendelea kutangaza na kufanya kazi yake kama kanisa na kutangaza neno la Mungu.
Pichani hapo juu anaonekana, Baba Mtakatifu,anaonekana akiwabariki waumini waliokuja kuhudhulia misa.
Picha ya pili anaonekana , Baba Mtakatifu akifunga mikono kukubali kukaribishwa kwake katika ziara yake nchi Australia.
China na Urusi zakataa na kuonyesha misuri yake ndani ya Umoja wa Mataifa.
New York, Amerika - China na Urusi zimepinga hatua yoyote ya kuiwekea vikwazo serikali ya Zimbabwe inayo ongozwa na rais Robert Mugabe.
Akiongea haya waziri wa mambo ya nchi za njee wa Urusi, alisema itakuwa ni wahatari na kitendo cha kamati ya ulinzi ya umoja wa mataifa kuingilia maswala ya nchi hasa hasa katika maswala ya kisiasa.
Hata hivyo,waziri wa mambo ya njee wa Urusi aliongezea kwa kusema ya kuwa serikali ya Urusi, inapinga kitendo chochote cha kukandamiza haki za binadamu popote duniani na kulaani matukio yote yaliyotokea nchini Zimbabwe.
Picha hapo juu ni picha ya bendera ya Urusi na bendera ya China, nchi ambazo zimepinga kuwekewa vikwazo kwa serikali ya Zimbabwe.

No comments: