Friday, July 18, 2008

Rolihlahla Nelson Mandela Madiba, atimiza miaka 90 tangu kuzaliwa"Leo pia watimiza miaka 10 ya ndoa"

Rolihlahla,Mandela Madiba atimiza miaka 90 tangu luzaliwa"Leo pia watimiza miaka 10 ya ndoa".

Eastern Cape - Afrika ya Kusini - Mtetezi wa haki za binadamu,kiongozi, mwanamapinduzi na aliyekuwa rais wa kwanza mzawa wa Kiafrika (Mweusi) Nelson Rolilhahla Mandela (Madiba) ametimiza miaka 90, leo 18/07/08.
Bwna, Nelson Mandela alichaguliwa kuwa rais wa Afrika ya Kusini mwaka 1994 baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi uliyo usisha vyama vingi nchini humo.
Katika kuadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwake miaka 90. ameagiza ya kuwa wale wote walio kuwa na mali na matajili waanze kuwasaidi wale watu masikini ambao hawana uwezo wa kimaisha.
Akiongezea agizo lake, Nelson Mandela , alisema mtu akiwa masikini nivigumu kuishi maiaka mingi.
Rais huyo wazamani wa Afrika ya Kusini, alishukuru kwa kusema nanafuraha ya kuwa bado yupo hai hadi sasa.
Nawakati huo huo, leo siku ya ijumaa 18/08, Nelson Mandela anasherehekea miaka kumi ya ndoa yake na bi Gracel Machel.
Mwana mapinduzi Nelson Mandela, alijiudhulu katika kazi za kisiasa ya jamii mwaka 2004.
Picha ya kwanza anaonekan Nelson Mandela wakati alipokuwa na miaka 42.
Picha ya pili anaonekan bwana Nelson Mandela kushoto akiwa na bi Winnie Mandela wakiwasalimi watu waliokuja kuwalaki wakati, wakuachiwa kwake kutoka gerezani mwaka 1990.
Picha ya tatu anaonekana rais, mstahafu, Nelson Mandela katikati na kushaoto kwake anaonekan waziri mkuu wa Uingereza bwana, Gordon Brown akipiga makofi wakati wwalipo kutana hivi karibuni mjini London, na kulia ni bi Gracel Macheli.
Picha ya tatu anaonekan,rais mstahafu Nelson Mandela, akipigwa kisi na mmoja wa wageni waliokwenda kumtembelea hivi karibuni.
Picha ya nne , anaonekan Nelson Mandela kabla ya kutimiza miaka 18.
Picha ya tano ,anaonekana rais mstahafu, Nelson Mamdela akifanya mazoezi ya ngumi,mchezo wa ngumi ulikuwa ndiyo mchezo aliokuwa akiupenda wakati wa ujamna wake.
Picha ya sita, anaonekana mwanamapinduzi, Nelson Mandela alipo kwenda kutembela gereza lililopo kwenye kisiwa cha Robin, ambapo alitumika kifungo cha wakati alipokuwa anatetea haki za wengi nchini Afrika ya Kusini.
Picha ya mwisho, anaonekana ,rais mastahafu ,mwanamapinduzi na mtetezi wa haki za binadamu Nelson Mandela akitabasamu kwa furaha baada ya kyadhimisha miaka 90 tangu kuzaliwa kwake. "Long live Nelson Rolihlahla Mandela'' Mungu akubariki na Mungu atubariki" Amin.
Mwanariadha akatishwa ndoto yake ya Olimpiki nchini China .
London,Uingereza - Mkimbiaji wa mbio fupi duniani, Dwain Chamber amekataliwa kushiriki katika mashindano ya Olimpiki 2008 nchini China.
Kwamujibu wa semaji wa wa mwanamichezo huyo, alisema mahakama imekataa kumrusu Dwain Chamber kushiriki mashindano hayo ya Olimpiki 2008 nchini China, kwa kutaaa kutengua kifungo ambacho, Dwain Chamber alipewa kushiriki katika mbio za kimataifa, baada ya kukutwa na kashfa ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini. Picha hapo juu ni picha ya Dwain Chamber, akitoka ndani ya mahakama kusikiliza kesi yake iliaruhusiwe kushiriki mashindano ya Olimpiki nchini 2008 nchini China.
Picha ya pili anaonekana Dwain Chamber akimaliza mbio za majaribio aliyoshiriki hivi karibuni nchini Uingereza.
Kanisa la Anglikana lawa na mvutano mkubwa"Askofu azuiliwa kuhushulia mkutano".
London,Uingereza - Askofu Gene Robinson, ambaye alikubali ya kuwa yeye ni shoga,amezuiliwa kuhudhulia mkutano wa wakuu wa kanisa la kikristu la Anglikani unaoendela nchi Uingereza.
Mgogoro katika kanisa la Anglikani, ulianza wakati askofu Gene Robinson alipo tangaza ya kuwa yeye ni shoga.
Kuzuiliwa kwake, kulifahamika baada ya askofu mkuu wa kanisa la Anglikani Askofu, Rowan Williams kutomwalika katika mkutano huu ambao hufanyika kila baada ya miaka kumi. Mkutano huu ambo umeanza usiku wa kuamkia tarehe 15/07/08, utazungumzia mswala ya kiimani na kujadili ikiwa wanawake wataruhusiwa kuwa wachungaji na maaskofu.
Picha ya askofu mkuu wa Kanisa la Anglikani, Rowan Douglas Williams, ambaye kanisa la Anglikana lenye waumini million 77, kote duniani, lina mwangalia kwa macho yote kutatua mgogoro ulipo katika kanisa hilo.
Picha pili ni ya kanisa kuu la Anglikana lililopo nchi Uingereza, lijulikanalo kama" St Paul's Cathedral".
Picha ya tatu ni ya Askofu,,Gene Robinson, ambaye amekuwa gumzo na chanzo cha mvutano katika kanisa la Anglikana , baada ya kueleza adhalani ya kuwa yeye ni shoga.
Nchi za Ulaya kuzidi kukaza nati kwa serikali ya Zimbabwe"Vikwazo kuongezeka".
Brussels, Belgium - Muungano wa nchi za Ulaya umezidi kuiwekea vikwazo zaidi serikali ay Zimbabwe inayo ongozwa na rais Robert Mugabe na washirika wake.
Kimsingi vikwazo hivyo vimekwisha kubalika baada mabalozi wa wa nchi hizi za jumuia ya Ulaya kukubaliana siku ya jumanne15/07/08,"Alisema mmoja wa viongozi aliyeudhulia kikao hicho".
Hata hivyo msemaji huyu alisema yakuwa uamuzi huu, uatakubalika na kupitishwa wakati wa kikao cha mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa jumuia hii ya Ulaya.
Picha ya hapo juu ni ya bendera ya Umoja wa nchi Ulaya, ambazo zimekubaliana kimsingi kuwekewa vikwazo serikali ya Zimbabwe.
Picha pili ni ya rais, Robert Mugabe ambaye serikali yake ipo katika hali ya kususasua kwenye jumuia ya kimataifa.
Picha ya tatu, wanaonekana kushoto, aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza bwana, Tony Brair wakati walipokutana miaka ya nyuma wakati nchi hizi mbili zilipo kuwa marafiki wa damu.
Picha ya mwisho ni ya bendera ya Zimbabwe, nchi ambayo serikali yake ina vutana na nchi nyingi za jumuia ya Ulaya.

Afrika ya Kati kuwa na amani tena,"Sudan na Chad kurudisha uhusiano".
Dakar,Senegal - Serikali ya Senegal chini ya uongozi wa rais Abdoulaye Wade, umeweza kuondoa mgogoro ambao ulikuwa unaleta matatizo kati ya Chad na Sudan.
Kufuatia mazungumzo yaliyo chukua siku kadhaa na kufila makubaliano siku ya alkhamisi 17/07/08, wiki hii.
Rais wa Sudana bwana, Omar Al Bashir alihaidi mgogoro huu umefika mwisho baada ya serikali za Sudani na Chad kufungua ofisi zao za kibalozi, ili kuendeleza mausiano yaliyo dholota, kutokana na kila upande kulaumu ya kuwa zinasaidiana na wapinzani wa serikali kuleta mchafuko katika nchi zao.
Picha ya hapo juu ni picha ya rais Omar Al Bashir, ambaye serikali yake ilikuwa na matatizo na seriikali ya Chad.
Picha ya pili na ya tatu, wanaonekan baadhi ya wapiganaji wa pande zote, ambao walikuwa wanashambuliana wakati wa mzozo ambao umekwisha.
Picha ya chini ni ya rais Idris Deby, ambaye alikuwa na hali ngumu kiusiano na rais wa Sudan bwana Omar Al Bashir.
Picha za kuchorwa hazita tiliwa maanani kwa watu wenye kuelewa"Mgombea urais wa Amerika - Baraka Obama"
New York, Amerika - Mgobani pekee wa urais, kupitia chama cha Demokrati cha Amerika, bwana, Baraka Obama amesema ya kuwa, kuchorwa kwake kwenye moja ya gazeti la mjini New York , niyakutotiliwa maaanani na watu wanao elewa hawatafuatilia na hakuna kigeni.
Katika michoro hiyo, wameonekana bwana, Baraka Obama naakiwa amevaa kama Osama Bin Laden na mkewe bi Michelle akiwa ameba bunduki na wote wana gongeana mikono.
Pichani hapo juu anonekana akihutubia katika moja ya mikutano yake hivi karibuni.
Picha ya pili anaonekana, bwana na bibi Obama wakiwa na watoto wa katika moja ya kampeni za awali ili kuweza kuwakilicha chama cha Demokrati katika kuwani kuwa mgombea pekee wa uraisi kupitia chama hicho.
Picha ya tatu ,anaonekana bi, Michelle Obama akisalimia, kabla ya kuanza kuhutubia moja ya mikutano hivi karibuni.
Picha ya chini ni picha ya kuchorwa ambayo imechorwa katika gazeti moja mjini New York.
Waasimu wawili kukutana anakwaana?"Inawezekana asema waziri wa mambo ya nje"
Ankara,Uturuki - Mazungumzo kati ya Iran na Amerika huenda yakawezekana kwa viongozi wa serikali hizi mbili kuzungumza anakwaana.
Akizungumza haya alipo kuwa ziarani Uturuki siku ya ijumaa, waziri wa mambo ya nje ya Iran, alisema yakuwa serikali ya Iran inaelewa haya kupitia vyombo vya habari, kama srikali ya Amerika itakuwa tayari basi tunaweza kukaa na kuongea.
Kufuati wasemaji wa serikali wa pande zote mbili, wanasema huenda kukawepo na mawasiliano hivi karibuni.
Kuzorota kwa Amerika na Iran , kulianza baada ya mapinduzi yaliyo ongozwa na viongozi wa dini mwaka 1979.
Picha hapo juu ni picha ya bendera ya Iran ambayo serikali ya nchi ya Iran haikubaliani na serikali ya Amerika, hasa katika swala la nyuklia.
Hapo katikati, anaonekana waziri wa mambo ya nje wa serikali ya Iran bwana Monauchehr Mottaki.
Picha ya tatu, nipicha ya bendera ya Amerika, nchi ambayo imekuwa ikivutana na na serikali ya Iran, tangu mapinduzi ya mwaka 1979.

1 comment:

Anonymous said...

Good post.