Monday, July 28, 2008

Uispania na Venezuela wasuruhisha mgogoro wao, na sasa kuganga ya jayoo.

Baraka Obama, hawa kuvutio cha wengi nchi za Ulaya "Matumaini yao atachaguliwa kuwa rais".

London , Uingereza - Mgombea kiti cha urais nchini Amerika kwa kupitia cham cha Demokratiki, bwana Baraka Obama, amemaliza ziara yake ya kutembelea nchi za Ulaya na nchi za Mashariki ya Kati.
Ziara hiyo aliyoifanya alitembela nchi za, Jordani, Israel, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.
Katika ziara zake hizo bwana Obama , alisisitiza uhusiano uliopo kati ya nchi za Ulaya na Amerika ni muhimu kudumishwa, na haukuna nchi inata kayoweza kutatua matatizo ya dunia peke yake.
Kufanyika kwa ziara hii ya bwana Baraka Obama, kuliwezesha wanchi na hasa wanachama wa chama cha demokratiki waishio nchi za Ulaya, kuweza kuhudhulia kwa wingi kwenye mikutano aliyo hutubia, huku wakiwa wameshikiria mabango yaliyo andikwa Baraka Obama awe rais.
Picha ya kwanza hapo juu anaonekana bwana Baraka Obama , akiwa anajiandaa kuwapungia mkono watu walio kuja kumsalimia kabla ya kuingia kwenye ofisi kuu ya serikali ya Uingereza iliyopo kwenye mtaa wa Dawning 10.
Picha ya pili, wanaonekana wananchi waliokuja kumlaki na kumsalimia, bwana Baraka Obama wakati wa ziara yake nchini Uingereza.
Picha ya tatu, anaonekana bwana Obama alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kuongea na waziri mkuu wa Uingereza bwana, Gordon Brown.
Picha ya nne wanaonekana Baraka Obama wakiwa pamoja na waziri mku wa zamani wa Uingereza bwana Tony Brair, wakati walipo kutana wakati wa ziara hiyo ya Obama nchini Uingereza.
Picha ya tano , anaonekana,waziri mkuu wa Uingereza bwana ,Gordon Brown akimwonyesha Baraka Obama, mazingira ya yaliyo izungu ofisi yake.
Picha ya sita anaonekana, Baraka Obama akiongea na waandishi wa habari wakati alipo kuwa nchini Ufaransa, kulia ni rais wa Ufaransa, Nicolaus Sarkozi.
Picha ya sita unaonekana umati wa watu wapato 2,00,000 waliokuja kusikiliza hotuba ya Baraka Obama, wakati alipokuwa ziarani nchini Ujerumani.
Chini mwisho wanaonekana, Kansera Angela Merkel akiwa na Baraka Obama, wakati wa ziara ya Obama nchini Ujerumani.
Idadi ya watu yazidi pungua nchini Swaziland" Wakina mama ndiyo hatarini"Umoja wa mataifa .
Mbabane,Swaziland -Ofisi za Umoja wa mataifa nchini Swaziland, imesema ya kuwa ya idadi ya watu inazidi pungua nchini Swaziland kutokana ma vifo vinavyo ambatana na ugonjwa wa ukimwi.
Ripoti hii ilitolewa hivi karibuni ilisisitiziwa na bi Aisha Kamara, ambaye ni mwakikilishi wa Umoja wa mataifa,alisema ya kuwa vifo vingi vinatokea hasa kwa kina mama na watoto, kwani ofisi inayo shughulikia idadi ya watu,iliseama wanawake 500,wanafariki dunia kati ya 1000 kwa mwaka kutokana na magojwa yanayo husiana ukimwi.
Kufuatia hali hiyo serikali ya Swaziland imetenga mfuko maalumu kwa ajili ya kupambana ha hali hii, haya yaliongelewa na waziri wa uchumi ,mipango na maendeleo Absolom Dlamini
Pichani ya kwanza hapo juu, anaonekana Mfalme Mswati kushoto,akiwa anasherekea siku muhimu y kihistoria ya nchi yake.
Picha ya pili, wanaonekana , wasichana wakiungana kwa pamoja kushereheka siku ya kihistoria ya nchi yao.
Picha ya tatu, wanaonekana wazee wa Kiswazilnd wamevalia mavazi ya kiasili, wakiwa wamekaa chini, baada ya kumalizika sherehe ya kihistoria ya nchi yao .
Picha ya nne, inaonesha mandhali nzuri ya asili nchini Swaziland, ambayo inasadikiwa wakazi wake wengi wanawakati mgumu wa kupambana na gojwa hatari la Ukimwi.
Picha ya mwisho ni bendera ya ya Swaziland, nchi ambayo mfalme ni kiongozi muhimu katika jamii nzima.
Uispania na Venezuela, wasuruhisha mgogoro wao, na sasa kuganga ya jayoo.
Madrid, Uispania - Rais wa Venezuela, Hugo Charvez, amekutana na wakuu wa serikali ya Uispania na kumtembelea mfame wa Uispania, mafalme Juan Carlos.
Ziara hii ya rais Charvez, ilikuwa ya kiserikali na kuimarisha uhusiano uliotetereka miezi ya nyuma, baada ya mfalme wa Uispania kufokeana na rais Charvez wakati walipo udhulia mkutano pamoja mapema mwaka jana.
Katika ziara yake hiyo ,rais Charvez aliweza kutaniana na mfalme Juan Carlos,kwa kumkaribisha waende ufukweni mwa pwani wakatembee kwani kulikuwa na hali ya joto saana.
Picha ya juu ni ben dera ya Venezuela nchi ambayo hapo zamani ilikuwa kolono la Uispania.
Picha ya kati wanaonekana rais Hugo Charvez kushoto, na mfalme Juan Carlos kulia wakikumbatiana na kuongea kuyamaliza yaliyo pita na kuganga ya jayo.
Picha ya chini ni bendera ya Uispania, nchi ambayo ilitawala Venezuela kwa muda mrefu.
Jiji la Istanbul, lipo katika mshituko mkubwa"Magaidi watega mabumu na kuuwa na kujeruhi wengi"
Istanbul,Uturuki - Watu wapatao 27 wamefariki dunia na kujeruhi wengini 150 ,baada ya mabomu kulipuka katika nyakati tofauti kwenye kitongiji kimoj mmoja jiji Istanbul .
Kwa mujibu wa mshihidi waliona tukio hilo,alisema ya kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea na na baadaye ulifuatia mlipuko wa pili mkubwa na kusababisha vifo hivyo na majeruhi wengi.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, alisema yakuwa milipuko hiyo ilipishana kiasi cha madakika kwani inasadikiwa mabomu hayo yalikuwa yamewekwa kwenye mifuko ya taka-yakuwekea uchafu na alongeaza huenda maafa ya kaongezeka kwani kuna watu wengine bado hali zao siyo nzuri.
Kufuatia mlipuko huo, waziri mkuu wa Uturuki, bwana Tayyip Erdogan, alisema yakuwa milipuko ya mabomu ni ugaidi wa hali ya juu , nakuhaidi ya kuwa ,Waturuki, aita tetereka kwani wamekuwa wakipigana na ugaidi zaidi ya miaka 30, watapigana hadi kushinda.
Waziri huyo, pia aliongeza kwa kusema ugaidi hauna dini, hakuna dini inayo ruhusu ukaidi, na dini ya Kislaam hataruhusu Magaidi kutumia Uislamu kama njia ya kutekeleza ugaidi wao.
Picha hapo juu anaonekana, waziri mkuu wa Uturuki, bwana Tayyip Erdogan,wakati alipo tembelea maeneo ambayo mabumu yalilipuka na kusababisha maafa makubwa kwa kupoteza maisha ya watu.
Picha ya pili, wanaonekan wahudumu wa huduma ya kwanza, wakimpakiza mmoja ya watu walioumia kutokana na milipuko ya mabomu.
Picha ya tatu, wanaonekana raia wakimsaidia mmoja ya jamaa ya ambaye amelala chini huku damu zikimtoka, baada ya kujeruhiwa na mmoja ya milipuko ya mabomu yaliyo tokea katika kitongiji cha jiji la Istanbul.
Abiria wa tua salama"Tanki la gesi la Oksigeni ndiyo chanzo?"Uchunguzi bado unaendelea.
Manila, Phillipienzi - Ndege ya shilika la ndege Qantas, boeing 747, imeponea chupu chupu na kutua salama baada sehemu moja ya ndege hiyo kubomoka na kudondoka wakati ndege hiyo ilipo kuwa hewani kuelekea Australia.
Kufuatia tukio hilo, ndege hiyo ilibidi itue kwa dharula mjini Manila.
Hata hivyo wachunguzi wa maswala ya ndege wamesema, bado wanachunguza ni kwanini tukio hili lilitokea kwa kusababishwa na tanki dogo lenye hewa ya Oksigeni ambalo linasadikiwa lilidondoka wakati ndege hiyo ikiwa hewani.
Picha hapo juu ni picha ya ndege,ambayo inaonekana ikiwa na tundu kubwa ambalo lina onekana kwa chini ya ndege.
Picha ya chini wanaoneka wapendanao amabo walikuwa moja wa abiria waliokuwemo kwenye ndege boeing 747, ambayo ilitua kwa dharula mjini Manila, baada ya kumegeka katika moja ya sehemu ya ndege hiyo.
Chama cha Labour chapoteza kiti kingine"Waziri mkuu Gordon Brown anawakati mgumu".
London,Uingereza - Waziri mkuu wa Uingereza bwana, Gordon Brown amekuwa katika hali ngumu kisiasa nchini Uingereza baada ya chama chake cha Labour kushindwa vibaya katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Glasgow Mashariki.
Kufuatia kushindwa kwa chama cha Labour ,mjini Glasgow kunaongezea idadi ya kuzidi kushindwa kwa chama hiki Labour kumekuwa ni mara ya tatu katika kwenye jimbo ka Scotland.
Hata hivyo chama cha Labour, kimekanusha yakuwa hakitaitisha uchaguzi wala kubadili uongozi wa juu wa kiserikali ambao unaongozwa na bwana Gordon Brown, na kufutilia mbali maoni na madai ya chama cha upinzani kinachoongozwa na bwana , David Camerron .
Kushindwa kwa chama cha Labour, kuna mweka waziri mkuu bwana, Gordon Brown kuwa na wakati mgumu kisiasa.
Picha hapo juu anaonekana akihutubia hivi karibuni katika moja ya mikutano nchini Uingereza.
Picha ya chini anaonekana, waziri mkuu wa Uingereza bwana, Gordon Brown akiwa anasikiliza moja ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

No comments: