Tuesday, February 3, 2009

Muungano wa nchi za Afrika wamchagua rais wa Libya kuwa Mwenyekiti.

Muungano wa nchi za Afrika wamchagua rais wa Libya kuwa Mwenyekiti.

Adis Ababa,Ethiopia - 03/02/09 - Muungano wa nchi za Afrika, umemchagua rais wa Libya Muammar Gadafi kuwa mwenyekiti wa muungano huo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia februari 2- 2009.
Rais Muamaar Gadafi,ambaye amekuwa akisisitiza kuungana kwa nchi za Afrika ndiyo njia pekee ya itakayo iponya Afrika na kutaweka heshima ya Afrika.
Katika ufunguzi wa mkutano huo, muungano wa nchi za Afrika, zilitaka vikwazo vilivyowekwa zidi ya Zimbabwe viondolewe, kwani viongozi wa nchi hiyo wamekubali kufanya kazi kwa pamoja ili kujenga Zimbabwe.
Picha hapo juu, anaonekna rais wa Tanzania Jakaya . M. Kikwete,ambaye muda wake wakuwa mwenyekiti wa wa muungano wa nchi za Afrika umekwisha akihutubia katika moja ya mikuta ya kuwakaribisha viongozi wa Afrika walipo tembelea nchi yake.
Picha ya pili,ni ya rais wa Libya, Muammar Gadafi,ambaye ndiye mwenyekiti aliyechukua kiti cha uwenyekiti wa muungano wa nchi za Afrika kutoka kwa rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akisikiliza kwa makini wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ulio fanyaka Adis Ababa Ethiopia.
Kundi la FARC nchini Kolombia, la achia mateka wengine.
Bogota, Kolombia - 03/02/09. Kundi linalo pingana na serikali ya Kolombia, FARC, limewaachia mateka wanne lililo kuwa likiwashikilia kwa muda mrefu.
Baadhi ya watu waliochiwa huru ni gavana wa zamani, Aran Jara, mwenye umri wa miaka 51, aliyetekwa nyara mwaka 2001.
Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la la msalaba mwekundu,Yves Heller,alisema Alan Jara, aliachiliwa huru, katika eneo lililopo kusini mwa Kolombia kwenye jimbo la Guaviere.
Picha hapo juu , wanaonekana wapiganaji wa FARC, wakiwa wanafanya doria, katika maeneo yao. Picha ya pili, anaonekana mmoja ya mateka walioachiwa na kundi la FARC, akiwasalimia ndugu na jamaa na marafiki waliokuja kumlaki.
Urusi na Belarus kudumisha ulinzi kati ya nchi zao.
Moscow,Urusi - 03/02/09. Serilikali ya Belarus na serikali ya Urusi, zimetiliana mkataba wa makubaliano ya kiulinzi, ili kudumisha ubola wa ulinzi kati ya nchi hizi mbili.
Makubaliano hayo yalifanyika nchini Urusi wakati rais wa Belarus, Alexander Lukashenko na mwenyeji wake, rais wa Urusi,Dmitry Medvedev.
Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mazungumzo yaliyo chukua muda mrefu kati ya nchi hizi mbili.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Urusi, Dmitry Medvedev, akimkaribisha mgeni wake rais wa Belarus, rais Alexander Lukashenko, alipo wasili nchini kwa ziara ya kiserikali.
Picha ya pili, wanaonekana viongozi wa nchi zote mbili, Urusi na Belarus, wakiongea katika mkutano mara baada ya kutiliana sahii mkataba wa makubaliano ya kiulinzi mjini Moscow.
Picha ya tatu, anaoneka rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, akisalimiana na waziri mkuu wa Urusi, Vladimir Putin, wakati alipo wasili nchini Urusi kwa ziara ya kiserikali.
Al-Shabab ya ahaidi kupigana na Majeshi ya Muungano wa Afrika.
Mogadishu,Somalia - 03/02/09.Kundi la Al-Shabab,linalo pingana na serikali ya Somalia, limesema ya kuwa litaanza kupigana namajeshi ya (AU African Union) majeshi ya Muungano wa Afrika. Akiongea hayo, mkuu wa kundi la Al-Shabab,Sheik Mukhtar Robow, alisema ya kuwa watawaimiza wananchi wote wa Somalia, kujiunga no kupigana na jeshi hilo, kwani wanauwa wanchi Wasomalia.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, watu wapatao 18, wali uwawa, baada ya basi walilo kuwa wame panda kushambuliwa na jeshi la muungano wa Afrika, inakuja baada ya jeshi hilo kushambuliwa na bomu lililo kuwa limetegwa barabarani kusini mwa Mogadishu.
Picha hapo juu wanaonekana wapiganaji wa kundi la Al-Shabab wakiwa wanafanya mazoezi ya kulenga kwa kutumia siraha.
Picha ya pili,anaonekana mmoja wa kina mama akilia kuonyesha kuomba msaada, kwani hali ya usalama nchini Somalia imekuwa ni ya kutisha.
Iran yarusha chombo Angani"Nimafanikio makubwa kwa Wairani"Asema rais wa Iran".
Tehran,Iran - 03/02/09. Iran imezindua na kurusha rasmi chombo cha kwenda angani.
Uzinduzi huo na urushwaji wa chombo hicho, kilichopewa jina Omid au Matumaini,ulishuhudiwa na rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad.
Akiongea mara ya chombo hicho kuruka angani, rais, Mohmoud Ahmadinejad, alisema hii ni mafanikio makubwa kwa Wairan wote.
Chombo hicho Omid, kitakaa angani kwa muda wa miezi mitatu, na madhumuni yake ni kuimarisha mawasiliano na kuangalia matukio ya asili.
Picha ya hapo juu wanaonekana Wanasayansi wa Kiirani wakiwa karibu na roketi iliyo tumika kurushia Omid.
Picha ya pili anaonekana rais wa Iran, Mohmoud Ahmadinejad,akipokea maelezo toka kwa mwana sayansi, wakati alipo tembelea eneo hilo kabla ya Omid kwenda angani.

No comments: