Vladmir Putin ashinda uchaguzi wa urais.
Vladmir Putin ameshinda uchaguzi huuo kwa zaidi ya asilimia 60% na anayemfuata kwa ushindi amepata 17%.
Huku machozi yakimtoka mbele ya wanachama na watu wapatao 100,000 walio kuwepo kwenye makao makuu ya chama United Russia Vladmir Putin alisema "tumeshinda kama tulivyo haidi na ni ushindi kwa wale wote waitakiayo Urusi mema."
Vladmir Putin alihutubia mkutano huo baada ya mtokeo ya uchaguzi kuonyesha ya kuwa ameshinda uchaguzzi huo kwa asilimia kubwa.
Baraka Obama ataoa onyo kwa serikali ya Iran.
Washington, Marekani - 04/02/2012. Rais wa Marekani ameoinya Iran kuachana na mpango wake kinyuklia au hatasita kutumia nguvu za kijeshi.
Rais Baraka Obama alisema "viongozi wa Iran lazima watambue hili, itabidi kutumia nguvu za kijeshi ikiwa mbinu zote za kisiasa kuisimamisha Iran kuendelea na mpango wake wa kinyuklia.
Ningeomba Izrael wawe na subira ili jitihada za kidilpomasia kufanya kazi yake, ikiwemo vikwazo vya kiuchumi ambavyo nafikiria vitafanikiwa na swaala la mazungumzo ya kivita tusiliongelee kwa sasa."
Hata hivyo serikali ya Iran imekuwa ikipinga ya kuwa haina nia ya kutengeneza siraha za kinyuklia na kuonya ya kuwa ikiwa kuna shambulizi lolote litafanyika nchini humo , basi Iran itajibu mashambulizi hayo kwa nguvu zote.
Izrael ianuwezo wake wa kujiamualia kuhusu Iran.
Tel Aviv, Izrael - 04/03/2012. Waziri wa mambo ya nje wa Izrael amehaidi yakuwa Izrael itamua niwakati gani kufanya mashambulizi nchi Iran bila kujali washiriki wake.
Avigdor Lieberman akiongea alisema "kweli Marekani ni nchi yenye nguvu kijeshi na mshiriki wetu mkuu wa karibu lakini Izrael ni nchi iliyo huru na inauamuzi wake yenyewe.
"Na uamuzi juu ya mpango wa kuisimamisha Iran isiendele na nguvu za kinyuklia ni uamuzi utakao faywa na Izrael."
Waziri Lieberman aliyasema hayo wakati wakati waziri mkuu wa Izrael Benyamin Netanyahu akiwa njiani kwenda kuonana na rais wa Marekani Baraka Obama, na swala la nyuklia Iran litakuwa na kipao mbele.
China kuongeza matumizi ya kijeshi.
Beijing, China - 04/03/2012. Serikali ya China imetangaza kuongeza matumizi ya kijeshi ili kuweza kupata uwezo sawa katika kujenga uchumi na ulinzi.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema " serikali ya China imesha panga kuongeza matumizi ya kijeshi kufikia asilimia 11.2%."
China imehaidi kuweka swala la ulinzi mbele na halitaharibu mipango mingine ya kiuchumi kwani fedha
hizo zitatumika kati mafunzo hya kijeshi kwa ajili ya wanajeshi wa China.
1 comment:
WANAJESHI WANATAKIWA KUJITAHIDI SANA KULINDA NCHI YAO MAANA VITA VINGI VYA JITOKEZA NCHI MBALIMBALI
Post a Comment