Areal Sharon alazwa nyumba yake ya milele.
Mazishi ya waziri Areal Sharon yalifanyika katika shamba leke kwenye eneo la jangwa la Negev.
Waziri mkuu wa sasa wa Izrael Benyamin Netanyahu ambaye aliongoza mazishi kwa niaba ya serikali, alisema " Sharon ni moja ya komanda wa Kiizrael ambao watakumbukwa kwa kuitete Izrael na Wajuishi "

Mazishi ya Areal Sharon yameudhuliwa na makamu wa rais wa Mareakani Joe Biden, waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergi Levrov, aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Brair na viongozi wengi kutoka sehemu tofauti duniani kasoro viongozi kutoka Afrika na Amerika ya Kusini.
Areal Sharon 85, alifariki kutokana na kuugua kwa baadhi ya viongo vyake vya ndani ya mwili, na hii ilitokana hapo mwanzo wa mwaka 2006 kupata ugonjwa wa kiaharusi ambao ulimsababishia kulazwa kwa muda wa miaka saba.
No comments:
Post a Comment