Waziri wa ulinzi wa Uingereza hausishwa na mateso ya wafungwa Irak.
Likiataja shirika hilo limesema "Geoff Hoon ambaye alikuwa waziri wa ulinzi na katibu mkuu Adam Ingram kuwa walihusika kwanjia moja au nyingine katika mateso na mantendo yaliyo kuwa yanakuiuka haki za binadamu kati ya mwaka 2003 na 2008 na kuvunja sheria ya Geneva ya kulinda wafungwa wa kivita."
Hata hivyo watu hao ambao wanashukiwa kufanya makosa hayo wamekana kuhusika na makosa hayo.
Kesi hiyo ambayo ina kurasa 250, ilikabidhiwa kwa ICC, huku ikiwa na makosa 85 ambayo inasemekana yamevunjwa na viongozi hao, na hivyo kuomba wachunguzwe.
Wakati wa vita vya Irak, wanajeshi wa Uingereza walishutumiwa kwa kuhusika katika kutesa wafungwa wa kivita, ambapo Geof Hoon alikuwa ndiye mkuu wa wizara ya ulinzi ya nchi ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment