Mwaka 2014 waanza kwa Wakenya kujeruhiwa na bomu.
Mombasa, Kenya - 02/01/2014. Mlipuko wa bomu umetokea baada ya watu walio kuwa kwenye pikipiki kurusha bomu katika hotel moja mjini Mombasa.
Akiongea kuhusu shambulizi hilo, Evans Achoki ambaye ni mkuu wa tarafa ya Kwale alisema " nilisikia mlipuko uliotokea katika hotel kwa jina Tandoori na baadaye nilipofika pale nilikuta watu wamejeruhiwa"
Kuthibitisha mlipuko huo, msemaji wa polisi Jack Ekakuro amesema " watu 10 wamejeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu na kwa sasa majeruhi wapo hospital kwa matibabu."
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu, tangu nchi hiyo ilipoamua kulisaidia jeshi la serikali ya Somalia katika harakati zake za kupambana na kund la Al Qaeda. Na kundi hilo la al Qaeda kuhaidi kufanya mashambulizi nchini Kenya.
Mwaka 2013 haukuwa mwaka wa heri kwa Wairak.
New York, Marekani - 02/01/2014. Umoja wa mataifa umetoa taarifa kuwa mwaka 2013 umekuwa mwaka ambao mauji kwa Wairak yalizidi kulinganishwa na miaka ya nyuma nchi humo.
Ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa "watu wapatao 8,868 wamepoteza maisha yao, na mauaji ya kutisha yametokea mwezi wa Desemba 2013 ambapo watu 759 ambapo 69 kati yao walikuwa ni walinzi na maafisa usalama wa taifa."
Mauaji mengi yanayo tokea nchini Irak yamekuwa ni ya kisiasa au ya kimakundi ambayo yanahusisha Washia na Wasuni, ambapo wamekuwa wakivutana katika kuongoza nchi, tangu kuangushwa kwa utawala wa Saadam Hussein na jeshi la Marekani na washiriki wake miaka 10 iliyopita.
No comments:
Post a Comment