Risasi zalipuka baada ya rais Michel Djotodia kutagaza kuachia urais.
Bangui, Afrika ya Kati - 10/01/2014. Rais wa mpito wa Afrika ya Kati ameachia madaraka baada ya serikali yake kushindwa kuhimili vishindo vya mvurugano wa kisiasa nchi humo.
Tangazo hilo la rais Michel Djotodia kuachia madaraka limetolewa, huku mkutano wa kuleta amani ukifanyika nchini Chad.
Baada ya kutangazwa kujiudhuru kwa Djotodia, milio ya risasi ilisikika katika sehemu tofauti jiji Bangui, na kambi ya wakimbizi Kikiristu 100,000 iliiingiwa na nderemo, na huku hakukuwa na hata mmoja wa wapiganaji wanaomuunga mkono Djotodia mitaani.
Kufuatia habari za kujiudhuru Michel Djotodia, waziri Ufaransa Ulinzi wa Jean-Yves le Drian amesema " tunatarajia kuwepo na uongozi mpya ambao utaiongoza Afrika ya Kati hadi kipindi cha uchaguzi na kuunda serikali itakato ongoza nchi kwa kufuata sheria."
Afrika ya Kati nchi ambayo ilikuwa koloni la Ufaransa, imekumbwa na mvurugo wa kisiasa ambao umepelekea kuleta matabaka ya kidini kati ya Waislaam na Wakristu ambayo kwa sasa makundi hayo yanapigana.
Na tangu kuanza kwa vurugu za kisiasa nchini Afrika ya Kati, maelfu ya watu wamesha poteza maisha, mali zao na hata kukimbia na kuchukua ukimbizi nje ya nchi ya Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment