Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael hatupo naye tena kimwili.
Ariel Sharon 85, ambaye alikuwa amelazwa hospital kwa muda mrefu, baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi mwaka 2006 na ambapo ulisababisha akupata madhara ndani ya viongo vya mwili wake na kupelekea kifo.
Shlomo Noy, ambaye ni msemaji wa hospital ambayo alikuwa amalazwa Sharon alisema " matibabu ya kila aina yalifanyika ili kummponya Sharon, lakini haikuwezekana na hivyo hatupo naye tena."
Msemaji wa familia ya Areal Sharon, Yoram Ravid amesema " kwa kuwa Sharon alikuwa ni mwanajeshi na hivyo naimani mazishi yake yafafanywa kwa taratibu za kijeshi."
Areal Sharon, atakumbukwa kwa hisia tofauti, kwa wengine kumwita shujaaa na wengine muuaji.
Kufuatia kifo cha Areal Sharon, Viongozi mbali mbali duniani wametuma salamu zao za rambi rambi kwa watu na serikali ya Izrael.
No comments:
Post a Comment