Saturday, November 24, 2007

Polisi wa Brazil wachanganya madawa, msichana wa miaka 15, aona cha moto.

Bolton wavunja mwiko, Alex Ferguson aamriwa kuwa mtazamaji. London.Uingereza - Kwa mara ya kwanza, kwa kipindi kisicho pungua miaka 20. timu ya Bolton Wanders, wameweza vunja mwiko kwa kuwafunga Man United goli moja kwa bila kweye uwanja wa nyumbani. Mara ya mwisho Bolton kushinda uwanja wa nyumbani ilikuwa desembe 1978. Goli la ushindi, lili fungwa na mshambuliaji hatari Nikalas Anelka kwenye dakika ya 11 kipindi cha kwanza. Matokeo ya mchezo huu yamewaza kuipa huai timu ya Bolton,kuepuka kuwa moja ya timu zinazo elekea kushuka daraja. Kufutia hali hii, kulimfanya kocha wa timu ya Man United, bwana Alex Ferguson, kutolewa kwenye benchi la wachezaji,na kuamriwa kuwa mtazamaji, baada ya kujibishama kimaneno na mwamuzi wa mchezo huo. Pichani anaonekana kocha wa Man United, Alex Ferguson,akielekea kujiunga na watazamaji, baada ya kutolewa kwenye benchi la wachezaji.

Wakati ni mgumu kwa mshambuliaji wa Kibrazil"Aingi kambini"
Milani.Itali - Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na Inter Milan Adriano, anatarajiwa kuanza mazoezi hivi karibuni,baada ya kuwa na matatizo binafsi.
Adriano anatarajiwa kuanza mazoezi ya peke yake huku kwao, ili kuwa tayari kuingia uwanjani tena.
Mshambuliaji huyu Adriano mwenye miaka 25, amekuwa na matatizo ya kutokuwa madhubuti kiakili, kimwili,na matatizo ya kifamilia, na wakati mwingine kunywa pombe kupita kiasi.
Hata hivyo huenda asirudi kwenye klabu yake Inter Milan,kutokana na sababu zisizo julikana.
Andriano huenda akajiunga na Man City au Arsenal, hapo atakapo kuwa madhubuti kimwili na kiakili.
Merry Jones afungiwa miaka miwili, na kutakiwa kurudisha fedha zote.
Monte Calro,Monaco-Mwana riadha maarufu wa mbio fupi duniani kwa upande wa wanake, Merry Jones, amefungiwa kukumbia au kushiriki mashindano ya aina yoyote ya riadha ya shilikisho la riadha la dunia kwa kipindi cha miaka miwili na kuvuliwa ubingwa wa dunia na kunyang'anywa medali zake alizo shinda kwenya mashindano ya olyimpiki yaliyo fanyaika Sydney Australia.
Vile vile amatakiwa kurudisha fedha zipatazo US$ 700,00 alizo pewa kama tunzo.
Merry Jones, alitangaza kujiuzuru kukumbia, baada ya kukubali yakuwa alitumia madawa yakuongezea nguvu mwilini wakati wa mashindano ya olympiki ya Sydney. Pichani hapo juu ni Mery Jones, akitoa machozi,baada ya kukili makosa yake, na picha nyingine Merry Jones akiingia ndani ya koti kusikia hukumu dhidi yake.
Rais wa zamani wa Ufaransa afunguliwa kesi za uchunguzi.
Paris. Ufaransa - Mahakama nchini Ufaransa, imefunga kesi ya uchunguzi zidi ya rais wa zamani wa Ufaransa bwana Jacques Chirac.
Kesi hii inahusu, kuajiliwa watu hewa, na matumizi ya fedha za umma wakati alipo kuwa meya wa jiji la Paris.
Kesi hizi hazikuweza kufunguliwa, wakati wa urais wake, kutokana na sheria za Ufaransa za kumlinda rais wa nchi kushitakiwa akiwa madarakani.
Hapo juu pichani ni rais wazamani bwana, Jacques Shirac akihutubia taifa.
Ili kujenga nchi upya, Somalia yapata waziri mkuu mpya.
Baidoa. Somalia- Baada ya rais Abdullahi Yusuf, kumteua bwana Hassan Hussen kuwa waziri mkuu mpya wa Somalia, amepitishwa na bunge la serikali ya Somalia na kuapishwa.
Kuteuliwa kwa bwana Hassan Hussen, ni katika kujenga uhusiano wa kimakabila nchini humo, nakuleta uhusiano wa karibu na serikali ya rais Abdillahi Yusuf, ambayo inawakati mgumu wa kuijenga upya nchi ya Somalia,baada ya kuaribika kiuchumi na kimazingira kwa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenye.
Bwana Hassan Hussen au kwa jina jingine Nur Adde, anatokea kwenye koo Hawiye, moja ya koo kubwa ambazo ndizo zilizo na nguvu nchini Somalia.
Hapo juu ni picha ya waziri mkuu mpya wa Somalia bwana Nur Adde.
Wateka nyara wa FNL, wanataka madai yao yatimizwe na serikali.
Bujumbura. Burundi -Kikundi kinacho pingana na serikali ya Burundi, The Force for National Liberation (FNL) kimewateka nyara maafisa wa serikali.
Msemaji mmoja wa kundi hilo, bwana Pasteur Habimana, amedai wamewateka nyara mafisa wawili, mmoja ni afisa usalama wa jimbo la Cibitoke, na afisa wa polisi anaye shughulikia uchunguzi na usalama wa Bujumbura.
Msemaji huyu aliongeza kwa kusema, wameaua kufanya hivi, ili serikali iwapatie wanachama wao ambao wamafungwa katika majela ya serikali. Pichani hapo juu ni askari wa jeshi la serikali wakiwa kazini , na chini ni picha ya askari wa serikali akiangalia miili ya watu walio kufa, baada ya mapambano na wapinzani wa serikali wajulikanao kama The Force of National Libaration (FNL)
Serikali yarudi nyuma, walala hoi"Chingas warudi mitaani"
Dakar. Senegal -Baada ya serikali ya Senegal kujaribu kuwafukuza,wafanya biashara wadogo wadogo wanao uza mitaani, hasa ndani ya jiji la Dakar kwa kutumia nguvu zake za dola, imeamua kuruhusu tena wafanya biashara hawa kuendelea na biashara zao kama kawaida.
Kufuatia maelezo ya benki ya dunia,asilimia 95% ni wafanyakazi wadogo wadogo(Chingas),na kunapunguza uzururaji na ukosefu wa kazi nchini humo.
Pichani ni mwela wa kupambana na vurugu, wakiwa wanamalizia kazi yao ya kuwafukuza (Chingas), kabla ya kruhusiwa kurudi mitaanai kuendelea na biashara zao kama kawaida.
Polisi wa Brazil, wachanganya madawa,"Msicha wa miaka 15 aona cha moto."
Sao Paulo. Brazil -Kutokana na wingi wa uarifu, unaosababishwa na ukosefu wa kazi, kumepelekea kujaa wa watu walio fungwa jela.
Hali hii imesababisha, polisi kwenye jimbo moja la Para, wamefanya kitendo cha kushutua jamii ya wa Brazil na ulimwengu kwa ujumla, baada ya kumuweka mahabusu msichana mmoja wa miaka 15 na wafungwa wengine wa kiume wapatao 20.
Kutokana na kitendo hicho, cha polisi kumweka pamoja na wanaume kulipelekea msichana huu kubakwa na kunajisiwa na mahabusu wenzake wa kiume.
Uchunguzi wa kesi hii bado unandelea, na wote walio husika na uzembe huu watachukuliwa haua, msemaji wa polisi alisema.
Hapo juu ni picha za lupango nchini Brazil,ambazo zinasadikiwa kujaa, huduma ni duni.
Mimi na wewe mpaka milele, lakini siyo kama ilivyo. " Nchini Misri"
Cairo.Egypt - Zaidi ya ndoa 240, huwa zinavunjika,au wapendanao kuachana, hii ni kutokana na na achunguzi wa maswala ya jamii.
Hii ni kuwa kila siku, ndoa moja huvunjika kwa kipindi cha dakika sita (6), kwa kipindi cha mwaka wa kwanza wa ndoa, na kukadiriwa ya kuwa kuna idadi ya ndoa 2,5 millioni kwa mwaka huvunjika.
Wengi ya wanaodai taraka ni wanawake,au kupewa taraka na waume zao kutokana na sababu mbali mbali, hasa wanaume wengine kutaka kuongeza mke mwingine ndani ya nyumba.
Ingawaje kuvunjika kwa ndoa huchukua muda, hasa kuzingatia muda wa kufatilia uamuzi wa mahakama.
Lakini msemaji alisema ya kuwa kunandoa nyingi, ambazo huvunjika bila habari zake kujulikana. Hapo juu ni vifungo ya chuma vya maisha ambavyo wapendanao huwa wanafungana ili waishi milele, lakini mara wanakata kwa msumeno vifungo hivi...................................... mambo yaha
Australia yapata waziri mkuu mpya, je vita Iraq mashakani?
Sydney. Australia -Waziri mkuu wa Australia bwana John Howard,ameshindwa kupita kuwa tena waziri mkuu wa nchi hiyo kwa kipindi kingine.
Bwana Howard ambaye ameiongoza Australia kwa kipindi cha miaaka 11 kama waziri mkuu chini ya chama chake Liberal Part .
Matokeo ya uchaguzi huu, yamepa bwana Kevin Rudd ushindi mkubwa na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya chama chake cha Labor Part kushinda kura, kwa asilimia 53%, zidi ya chama cha cha bwana Howard ambacho kimepata asilimia zipatazo 47%.
Bwana Kevin amehaidi kuleta mabadiliko, na kuangalia upya kuhusu vita vya Iraq. Pichani ni picha mbili tofauti, picha ya juu anaonekana bwana Kevin Rudd, akiangalia kwa tabasamu baada ya mataokeo.Picha nyingine anaonekana bwana John Howard aki waaga wanachama wenzake baada ya kukubali mtokeo ya uchaguzi
Nimeishi kwa kunywa aja ndogo na majani ya pori"Mfanyakazi wa mbuga za wanyama"
Nairobi.Kenya - Mfanyakazi mmoja, anayefanayakazi kwenye mbuga za wanayama karibu na mlima Kenya uliopo km110 kaskazini mwa mji wa Nairobi, bwana Solomon Nyanjui ameponea chupuchupu baada ya kuanguka na helikopta. Bwana Solomon Kinyanjui, ambaye ni mfanya kazi wa Kenya Wildlife Service (KWS), amekuwa ana fanya kazi ya kuendesha helikopta, kwa kipindi cha miaka 27. Baada ya ajali kumkuta, bwana Solomoni Kinyanjui, alisema, aliweza kuishi porini na majeraha, na kwa kula majani na mkojo wake mwenyewe hadi hapo wanajeshi wa jeshi la Kenya walipo kuja kumuokoa. Hii ni mara ya pili bwana Kinyanjui anaponea chupuchupu,mara ya kwanza alipata na ajali kama hii 1995 wakati alipo kuwa akikagua mbuga za wanyama. Pichani, ni mmoja wa kifaru, ambaye bwana Solomon Kinyanjui na wafanayakazi wenzake huwa wanawalinda, na kuwafatilia kwa makini ili wasimalizwe kabisaa, na wawindaji haramu ambao huwaua na kuchua pembe zao tayari kwa mauzo. Zim dolla, kuchapishwa upya, Irani na Zimbabwe ushirikiano wa mzuri zaidi.
Harare. Zimbabwe - Gavana wa benki kuu ya Zimbabwe, bwana Gideon Gono, ametangaza ya kuwa serikali, imetoa noti mpya, hivi karibuni.
Hali hii inakuja, kutokana na kushuka kwa thamani ya pesa ya Zimbabwe, ijulikanayo kama Zimbabwe dollar.
Akiongea na waandishi wa habari, gavana Gideon Gono, lindelea kwa kusema kwa kuwashutumu baadhi ya wafanya biashara na wale watu wanao shikilia pesa, wanaombwa wa zibadilishe kwa haraka, kabla ya kupoteza thamani yake, na akaagiza benki ziongeze maasaa, ili kukabiliana na mabadiliko haya.
Wakati huo huo, ushirikioano wa Zimbabwe na Iran unazidi shamiri,baadaya viongozi wa nchi hizi mbili kukutana na kuongea wakati rais Robert Mugabe, alipo tembelea hvi karibuni nchin Iran. Pichani ni rais wa Iran, Mahamoud Amadinejad na rais Robert Mugabe, wakikagua gwaride rasmi lillilo andaliwa kwaajili ya rais Mugabe.

No comments: