Wednesday, November 14, 2007

Yupo chini ya ulinzi kwa kuwa shushu wa serikali "Wapinzani"

Mamilioni ya toka mapenzi yanapo kwisha" Malipo ya vunja rekodi"

Chicago. Nyota wa Mchezo wa vikapu (basket ball) Michael Jordan, inasadikiwa itabidi amlipe mke wake Juanita, kiasi cha million 168. Malipo haya yana kuja baada ya Michael Jordan kutangazwa kuachana na mkewe ambaye wameishi pamoja kwa kipindi cha miaka kumi na saba (17) kama mke na mume. Pichani hapo juu ni Michael Jordani akiangalia kwa makini hali halisi baada ya msuko suko.

Mama alikuwa kila kitu kwangu, kuondoka kwake ni pigo kwangu " Kanye West'

Mwana muziki wa iana ya ngonjera, au fokafoka, Kanye West, ameshikwa na mshituko mkubwa, baada ya kuondokewa na mama yake mzazi. Dr, Dondo West mwenye miaka 58, mama ya mwanamuziki Kanye West, alifariki dunia, kutokana na operesheni ya mwili. Kifo hiki kimetokea wakati Kanye West yupo safarini Ulaya kisaniii. Pichani hapo juu ni Kanye West na mama yake Dr Dondo Kanye, wakati Kanye West alipo shinda zawadi kutokana umairi wa muziki wake ambao umetokea kupendwa duniani hasa kwa vijana. Uzawa na kutambuana kwa kitaifa, waleta kizaazaa kwenye Umoja wa Ulaya "EU"

Brussels.Wabunge watano wa Romania , wamedai kuwa watajitoa ikiwa katika bunge la Ulaya, ikiwa matamshi yaliyotolewa na Mrs Mussolini ya kuwa watu wenye asili ya kiromania ni Sugu. Matamshi haya yalitamkwa na mrs Mussolini, baada ya raia mmoja wa Itali kuuwawa na inasadikika raia romania ndiye aliye msababishia kifo hiki. Utata wa uzawa wa asili na kutambuana, kulizuka baada ya kujiunga kwa Romania na Bulgaria kwenye jumuia hii ya n Ulaya na kuleta mgawanyiko kwa kiasi fulani, kuhusu uzawa wa asili na kutambuana. Pichani ni watu wakiandamana kupinga hivi karibuni . Yupo chini ya ulinzi kwa kuwa msaliti "asema kiongozi wa LRA"
Uganda ya Kaskazini. Kiongozi wa majeshi ya upinzani yaliyopo nchini Uganda, bwana Joseph Koni, amedai ya kuwa makamu wake bwana Vicent Otti bado ni mzima. Akiongea na msuruhishi wa mgogoro huu, bwana Norbet Mao, bwana Koni alidai ya kuwa bwana Otti ni mzima, na siyo kweli kama ilvyo daiwa na ya kuwa ameuwawa na wanajeshi wake wa LRA. Na kwa sasa yupo chini ya ulinzi kwa madai ya kuwa ni shushuu wa serikali ya Uganda. Bwana Koni na bwana Otti wanatafutwa na mahakama ya kutetea haki za binadamu, nainaaminika wapo wamejificha mashariki ya misitu ya Kongo. Pichani hapo juu ni bwana, Vicent Otti kama kamanda enzi hizo. Tumemwachia shushuu, kwa manufaa ya taifa" Mwana sheria mkuu" Lagos. Serikali ya Nigeria, imemuachia huru, mmoja wa raia wa Amerika, ambaye alikamatwa kwa madai ya kuwa shushu, "mpelelezi". Bi Judith Burdini Asuni, alishitakiwa kwa kosa la kuhatarisha salama wa nchi, kwa kuwasaidia wajerumani kupata mikanda ya video- runinga, inayao onyesha shughuli za maeneo ya Niger Delta. Wakili mkuu wa serikali ya Nigeria, alisema kuachiwa kwa bi Judith, ni kwa sababu za manufaa ya kitaifa. Bi, Judith Burdin Asuni, mzaliwa wa Nigeria, ambaye anauraia wa kiamerika, aliachiwa pamoja na wenzake wajerumani ambao walikuwa wanafanya kazi pamoja. Hapo juu pichani. ni bi Judith Burdin Asuni, alipo kuwa kizimbani kusikia shitaka linalo mkabili kushoto pembeni ni kachero. Afrika ya Kusini, moto wa nani zaidi kuwaka tena." Zuma Mashakani"
Johannesburg. Wakati uchaguzi wa kumchagua nani atakuwa kiingozi wa chama tawala, (ANC) African national Congress, nchini Afrika ya Kusini ukipamba moto. Mmoja ya wagombea wa kiti hicho, aliye kuwa makamu wa rais bwana Jacob Zuma amekutwa na wakati mgumu, baada ya mahakama kuu, kuruhusu kuendela kwa uchunguzi wa kesi ya rushwa, iliyo kuwa ikimkabili miaka mitano liyo pita. Mawakili wa serikali wamefurahishwa na wamelikaribisha uamuzi wa mahakama kuendelea na uchunguzi huu. Bwana, Zuma ali simamishwa kazi ya umakamu wa rais miaka, kutokana na kesi hii inayo husisha maswala ya bishara siraha, Bwana, Jacob Zuma kwa sasa ni makamu wa chama tawala cha ANC. Pichani hapo juu ni bwana Jacob Zuma akiongea kwenye mmoja ya mikutano ya ANC hivi karibuni.
Mwanajeshi awa majalala kwa kipindi kisicho pungua miongo miwili.
Washingtone . Inasadikika ya kuwa mmoja ya kati wanajeshi wanne waliopigana zamani wakati vita, ana ishi maisha ya omba omba , na kulala nje na kukusa matibabu na bima ya maisha.
Kutokana na mmoja wa wanajeshi hawa bwana Ben Israel mwenye miaka 51, alisema, ameishi maisha ya kuangaika na bila nyumba, tangu akiwa na umri wa miaaka 30 . Aliongezea kusema yakuwa wapiganji, wengine wameishi na wanishi maisha ya kuhangaika hapa na pale na bila kuwa na makazi maharumu, au nyumba za kulala, ingawaje wapiganaji hawa idadi yao ni kiasi cha asilimia 11% ya watu wazima waliopo nchini Amerika.
Hata hivyo msemaji mwingine amesema ya kuwa swala hili linashughulikiwa, kuna baadhi ya wapiganaji wamesha patiwa makazi mapya. Na mmoja wao ni bwana Ben
Kila jamii ina amri kumi, kama za Mtume Moses, alizo shushiwa kule jangwani.
Itali. Polisi nchini Itali hivi karibuni wamefanikiwa kumkamata kiongozi wa kndi la mamafia nchin humo.
Kiongozi kwa jina Anajulikana kama Salvatore Lo Piccolo, amabaye inasadikika ndiye anaye ngoza kundi maarufu la mamafa wenye makazi katika mji wa Sisilia.
Kitu chakushangaza ni hapo polisi walipokuta amri ambazo, ni msingi mkubwa wa mamafia. au kwa kitishi "Ten Commandments" Amri kumi za kimsingi za mamafia.
Amri hizi ni
1. Usijitokeze, au kuwa na kimbelembele, "Show off". Acha mtu mwingine wa tatu ashughulike.
2. Heshimu mke wa mwanachama mwenzio au wake wa wanchama wenzako.
3. Kaa mbali na vyombo vya sheria.
4. Usijihusishe na starehe za kijinga, kama kwenda baa au kwenye vilabu kunywa.
5. Ikiwa mtoto kazaliwa, ni wajibu wa mama kumtunza, kwani mwana chama muda wowote yupo kazini "COSA NOSTRA", hii ata kama mke wako anataka kujifungua.
6." Ahadi" Kutimiza ahadi ni wajibu wa kila mwana chama "Lazima"
7. Wake na wakina mama waheshimiwe kwa kila namna.
8. Kuwa mkweli kila unapo toa habari au kujibu swali.
9. "Pesa", Deni, au dhuruma ya aina yeyote kwa mtu au familia ni marufuku, hasa kwa Wana chama".
10. Cosa Nostra, hairuhusiwi kuwa mwana chama kama mmoja wa ndugu zako ni askari kanzu "Shushuu au polisi ama kuwa na uhusiano wowote na polisi..
Haya yoye waliwashangaza watu wa vyombo vya dola na kupigwa na mshangao mkubwa.
Hapo juu ni picha ya polisi, wakiwa na kiongozi wa mamafia ambaye aliwakimbia kwa kuda wa miongo miwili.

4 comments:

Anonymous said...

wohin die Welt gerollt wird? cialis viagra preisg?nstig [url=http//t7-isis.org]viagra generika erfahrungen[/url]

Anonymous said...

Felicito, que palabras..., el pensamiento magnГ­fico [url=http://csalamanca.com/category/viagra/ ]viagra sin receta buenos aires [/url] Como es curioso.:) comprar viagra online

Anonymous said...

Time and tide wait for no man.

Anonymous said...

tantric masѕage salmon in avocado pear beyond quaԁ and clock timе.

Mіkao Usui іnicia ѕeus trabalhos com a Energia tantric massаge Ap�s redеscobrіг о tantгiс maѕsagе e
seus one is a сleaг dіagrammatiс impressiоn.
The gеomеtric dеsignѕ aгe dіfferent for diverѕe aspects of my wаtch eаrliеr I take іt off and it's 1 AM and so. But, something has happened; this country would be ideal.

my webpage homepage
my web page -