Sunday, November 4, 2007

Pembeni mwa Afrika yawa moto wa mchanga, nani wakukanyaga?

Martina Hingis, na miadharati ( Kilevi) yakata kipaji chake.

Bingwa wa zamani wa tenisi kwa wanawake Martina Hingis amegundulika kutumia mihadarati aina ya kokeini.
Martina Hingis alijulikana kama ni mtumiji wa madawa ya kokeni, wakati alipo tolewa damu kwa vipimo ziidi, kwenye wa mashindano ya Wembley cup yaliyo fanyika mwaka huu 2007 nchini Uingereza.
Kutokana na kashfa hii, Martina Hingis amejitoa katika mashindano ya aina yoyote ta tenisi duniani.
Hapo juu pichani, ni Martina Hingis, alipo kuwa akiongealea hali hii.
Picha nyingine, Martina Hingis, kulia akionyesha kikombe alicho shinda na mwan tenis akimsaidia kunyanyua kikombe juu wakati wa enzi zake nchini Australia wake.
Pembeni mwa Afrika yawa moto kwaDunia nzima.
Wanajeshi wa Ethiopia na pamoja na washirika wao wa somalia, wamepoteza maisha ya baadhi ya maaskari wao, wakati walipo pambana na wapinzani wa serikali ya Somalia hivi karibuni. Mapambano haya yalitokea karibu na uwanja wa mpira wa mjini Mogadishu.
Kwa mujibu wa watu waliona mapambano haya, wamesema waliona miili ya maaskari ikiwa ime zagaa karibu na eneo hilo la mapambano hayo.
Vita hivi vimeleta hali kutokuwa nzuri nchini Somalia, watu wasio pungua mamia kukimbia maeneo yao ya hasili.
Pichani ni askari wa Ethiopia, wakielekea vitani kupamabana wa wapinzani wa serikali ya Somalia hivi karibuni.
Mafia wachangia kiasi kikubwa kuinua bishara katika makampuni.
Wachunguzi wa mambo ya kiuchumi wamedai ya kuwa kundi la mamafia, linachangia kwa kiasi katika kuongeza biashara nchini Itali.
Wachunguzi hawa wamedai ya kuwa inachangia kiasi kiasi cha $120billion kwa mwaka. Na wamedai ya kuwa halii ina kuwa hasa upande wa kusini mwa Itali.
Hapo juu ni picha ya baadhi ya maeneo ambayo ni makazi ya wafanya biashara wa kimafya nchini Itali.
Mipira ya kufanyia mapenzi(kondom), haifai kiviwango.
Serikali ya Afrika ya Kusini, imeamua kukusanya mipira ya kunginga magonjwa na mimba, ijulikanayo kama kondom, baada ya kushindwa kufikia kiwango cha kimaatifa.
Hali hii imefikiwa, baada ya wachunguzi wa afya kugundua ya kuwa kiwanda kinacho tengeneza bidhaa hizi, kutoa rushwa kwa wafanyakazi wa shirika la viwango, kupitisha kiviwango kutumika kwa kondom hizi zipatazo mamilioni.
Hali hii inarudisha nyuma, vita zidi ya ugonjwa wa ukimwi, ambao huna poteza maisha ya watu wasiopungua 900. Pichani hapo juu,ni mwa mama akionyesha kondomo ambazo walizani ni salama kumbe hazifai, na hivyo kuamua kuandama kuiomba serikali iwasaidie.
Jeshi madarakani demokrasi kulegeza maafande.
Hali ya hatari imetangazwa nchini Pakistani na baraza la wanasheria kusimamishwa pamoja na jaji mkuu wa nchi.
Na na baadhi ya wapinzani wa kisiasa wape fungwa kifungo cha ndani kwa muda usio julikana.
Akitangaza rasmi, rais wa Pakistani bwana, Gen, Pervez Musharraf, alisema hii ni kwaa jili ya usalama wa nchi ya Pakistani, na akaendelea kusema yakuwa wapo kwenjia ya kujenga demokrasi ambayo itaifaa nchi ya Pakistani.
Hata hivyo, wapizani wake wakuu wa kisiasa nchini Pakistani, wa kiongozwa na bi Benazir Bhutto,wamesema, hii ni njia ya kiditekta na haifai katika kujenga kataiak kujenga Pakistani.
Hapo juu pichani ni hali, siyo shwali kwa wana nchi wa Pakistani,mmoja ya raia akishikilia kichwa kwa kuinama chini, baada karandinga la wazee kupita na kumwachia vumbi.
Rais wa Ufaransa afuatialia kuweka mambo sawa.
Rais wa Ufaransa bwana Nicholas Sarkoz, ameeleke nchini Chad,katika harakati za kutatua mgogoro uliopo kati ya Ufaransa na Chad, kuhusu kukamatwa kwa wafanyakazi wa shirika moja la kusaidia watoto litokalo Ufaransa lijulikanalo kama Zoe's Ark.
Shirika hilo na wafanyakazi wake wan shutumiwa kwa kutaka kutorosha watoto wapatao 103, kuwapeleka nchini Ufaransa kuwatafutia familia mpya.
Pichani ni kiongozi wa Zoe's Ark,bwana Eric Breteau, akiwa mukashoo, na anaonekana ameshikilia sigara kwa kujipoza na joto ja jiwe ya mukashoo.
Libya yatakiwa kukaa chonjo kuanzia sasa , aonya kiongozi wa chama Alqaeda .
Kiongozi mwandamizi wa chama Alqaeda, ameitahadhalisha Libya ijiandae, kwa mashambulizi ya aina yoyote.
Hii ina tokana na nchi ya Libya kukubali kushirikiana na nchi ya Amrika na Ulaya magharibi "alisema kiongizi hiyo"
Akisisitiza kwa makini, alitamka rasmi ya kuwa chama cha waislamu wenye siasa kali cha kilichopo Libya pia kimejiunga na Alqaeda, na hii ni baraka kwa mtandao wa Alqaeda katika kupinga mambo yanayo fanywa na Amerika.
Vilevile a kiongozi wa kundi hili litokalo Libya bwana Abu Laith al Libi, aliyathibitisha hayo maneno kwa kusema ya kuwa rais Gaddafi ya kuwa anaipeleka nchi ya Libya kusiko.
Pichani hapo juu ni mwandamizi wa kiongozi wa Alqaeda akiongea kupitia runinga As Sahab.

No comments: