Homa ya zidi panda 2010, dunia itakubali Afrika ina uwezo"Soka la dunia"
Pretoria. Maandalizi ya kombe mpira wa miguu la dunia yatakayo fanyika nchini Afrika ya Kusini 2010, yamekadiliwa kuighalimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kuliko kilivyo kadilikiwa hapo awali.
Kiasi hicho huenda kikapanda hadi kufikia Us$ million 500, ni sawa na asilimia 20% la ongezeko, toka mashindano ya takapo anza na kumalizika.
Akiongea, waziri mdogo wa fedha wa Afrika ya Kusini bwana Jabu Moleketi,alisema hii inatokana na kuwepo mabadiliko ya bei na mahitaji ya vifaa vitakavyo kamilisha uandaaji huu mkubwa katika historia ya soka barani Afrika.
Alihaidi dunia nzima itakubali kuwa, Afrika tunao uwezo wa kuandaa mashindano haya.
Hapo juu ni picha ya nembo au alama itakayo tumika wakati wa mashindano ya kombe la soka au kandanda la dunia nchini Afrika ya Kusini 2010.
2million paundi kama kiinua mgongo, kiti moto cha timu ya taifa ya Uingereza kikowazi.
London. Uingereza. Kufuatia kushindwa kuingia kwenye mashindano ya kugombea kikombe cha ubingwa Ulaya, kocha mkuu wa Uingereza kibarua chake kiliota majani.
Kocha huyo bwana Steve MacClaren,ametimuliwa na chama champira cha nchi ya Uingereza yeye pamoja na jopo lake la walimu.
McClaren, tangu achukue timu ya taifa ya Uingereza miezi 18 iliyo pita, alisema kuondoka kwangu kama kocha wa timu ya taifa ni uchungu mkubwa katika maisha yake, na kuongezea ya kuwa amejifunza mengi kwa kipindi alicho kuwa kocha wa Uingereza.
Bwana McClaren, ameondoka na kitita cha paundi million 2 kama kiinua mgongo.
Hata hivyo kuondoka kwa bwana McClaren kumeleta, kufunguka milango kwa makocha kadhaa, maarufu duniani, akiwemo, kocha wa zamani wa Real Madrid, bwana Fabiano Capello, kocha wa zamani wa Chelsea bwana Jose Mourinho .
Lakini , bwana Mourinho, amesema hawezi kuwa kocha au kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza.
Pichani hapo juu, anaonekana aliyekuwa kocha bwana Steve McClaren na mke wake bibi Kathryn wakitokea ndani baada ya kuongea na waandisi wa habari, "huuu" kuachana na kiti moto cha timu ya taifa ya Uingereza.
Waziri mkuu wa Rhodesia afariki dunia,ubaguzi ulikwisha alipotoka madarakani.
Johannesburg. Afrika ya Kusini. Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Zimbabwe bwana Ian Smith, amefarika dunia hivi karibuni.
Chanzo cha kifo chake hakijajulikana,lakini watu wake wakaribu walisema bwana Smith alikuwa anaugua kwa muda mrefu.
Ian Smith, aliongoza kufukuzwa kwa Uingereza nchini Zimbabwe 1965, na kuongoza serikali ya wazungu wachache na kuwakandamiza wana wa Afrika waliowengi nchini Zimbabwe enzi ikijulikana kama Rhodesia.
Pichani hapo juu, anaonekana Ian Smith akiongea na waandishi wa habari, wakati wa enzi zake kama waziri mkuu wa Rhodesia.
Wasichana wa Uingereza kuonja lupango nchini Ghana.
Accra. Ghana, wasichana wawili raia wa Uingereza waliokamatwa na polisi julai, 2/07,wakati wakijaribu kupenyesha 6kg ya madawa ya kulevya ili kuyapeleka Uingereza kupitia kiwanja cha ndege cha Acrra wamekuta na hatia.
Wasichana hawa,Yasmine Vatansever na menzake Yatunde Diya wamekutwa na makosa na wanaweza kufungwa kwa kipindi cha miaka mitatu au zaidi kufuatia sheria za kuwafunga vijana wasio timia miaka 18 nchini Ghana.
Hukumu ya kesi yao inatarajiwa kutolewa desemba 5/07.
Kukamatwa kwa wasichana hawa, kunakuja kuokana na ushirikiano kati ya polisi wa Ghana na Uingereza, ili kuzuia biashara hii ambayo imeshamiri saana kupitia nchi za Afrika ya magharibi na kuingizwa nchini Uingereza.
Pichani ni mmoja wa wasichana na uchungi kichwani,akielekea kwenye ndinga lamwela kurudi mung'aanda kungojea kazi ya muheshimiwa bwana Pilato,ambaye hawajui atawapa mvua ngapi.
Hali ya usalama, na ushindani wa kibiashara barani Afrika"Shell kuachia ngazi?"
River Delta. Kutokana na kuokuwa na hali ya usalama, na mashindano ya biashara kataika uchimbaji wa mafuta eneo la mto Delta nchini Nigeria,kampuni kubwa dunia ni ya uchimbaji na uuzaji wa mafuta na gasi Shell imetangaza huenda ikauza baadhi ya hisa zake kwa kampuni moja ya kichina.
Habari zilizo patikana, zimesema yakuwa,kutokuwepo usalama katika eneo hili la Delta ni chanzo kikubwa cha kudhohofisha uzalishaji wa mafuta na gesi, na hivyo kupelekea shell kufikilia kuuza hisa zake zilizopo eneo hilo.
Hali yakuto kuwa na usalam, inakuja baada ya wakazi kutoona faida ya uwekezaji huu, hasa kwa kukosekana mahitaji muhimu kama, maji safi , shule, hospitali na barabara.
Hata hivyo, sababu nyingine ni makampu ya kichina yamekuwa yanaleta ushindani mkubwa katika kuwekeza hisa, na kusababisha bei kupanda.
Lakini ata hivyo msemaji wa shell, alikataa kuongea chochote kutokana na habari hii.
Hapo juu pichani, ni makaazi mmoja wa eneo la Delta, akiangalia kwa makini jinsi uchimbuzi wa mafuta na gasi unavyo endelea.


No comments:
Post a Comment