Wednesday, November 7, 2007

Hatu waachi peke yenu tupo bega kwa bega.

Maombi yangu Mungu ameyasikia sasa nipo kwenye kitabu" Christine Ohuruogu" . Christine Ohuruogu, amechaguliwa kuwa mwanariadha bora wa Uingereza wa mwaka 2007. Christine miaka 23 ambaye alishindambio za mita 400 na kupata medali ya dhahabu jijini Osaka Japani, alitunukiwa - GB vest- kwa jitihada ya zake za kujituma hasa wakati wa mashindano yote aliyo shiriki.

Pichani hapo juu ni bi Christine Ohuruogu akionyesha medali yake ya dhahabu aliyo shinda hivi karibuni.
Nivigumu kueleawa nchi za Ulaya zinatofautiana kwa watu waliopo mbali na Ulaya" Pele".
Uingereza imependekezwa kuwa muandazi wa kombe la dunia2018, na mwanasoka mashuhuri dunia Pele.
Pele ambaye amealikwa nchini Uingereza kuadhimasha miaka 150 toka kuanzishwa Sheffield FC.
Sheffield ni moja ya timu ya zamani nchin Ungereza.
Pele aliogeza kwa kusema Uingereza lazima ijiandae kikamilifu, kuandaa mashindano haya.
Kwani watu huwa wanafikilia Ulaya zote zina fanana, lakini ukwali ni kwamba azifanani, na kwa kuzingatia Ujerumani na Ufaransa zinakaribiana, na wamesha andaa kombe la dunia.
Hili hii uwapa watu maswali mengi, na nivigumu kwa watu kuelewa ya kuwa nchi hizi zinatofautiana kwa kiasi kikubwa ki mila na kimazingira.
Usiponipenda wewe, wenzio wanitafuta " Wahenga walisema".
Mwana muziki maarufu dunia Poul McMartney,ambaye hivi karibuni alichana na mke wake, ameonekana na mwana mama mwingine bi Nancy Shevell.
Mwana mziki huyu ambaye kuachana na mkewe kurimgarimu karibu kiasi cha maelfu ya paundi za Uingera, alionekana akimpiga kisi mwana mama huyu.
Pichani hapo kulia ni bwana Poul MacCartney akitabasamu.
Maisha ya watu wapatao 500, yamepotea na nani wa kufika kizimbani?"Shirika la haki za Binadamu".
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Kenye, limeomba uchunguzi ufanyike kuhusu mauji ya watu wasiopungua 500, ambao inasadikiwa walikuwa wanachama wa kundi la mungiki.
Kutokana na msemaji wa shilika la utetezi wa binadamu nchini humo, amesema watu hao wali uwawa kwa kupiga risasi, na hii inatokana na ripoti za waganga waliochunguza marehemu hao. Msemaji huyu aliongezea kusema wanaomba wachunguziwa kesi hii watoke kutoka nchi kama Afrika ya kusini,Rwanda, na Ghana, kwani polisi wa Kenya wameshindwa kuendelea na kesi hii.
Lakini msemaji wa polisi, amesema polisi bado wanachunguza na kulifuatialia swala hili kiundani. Pichani hapo juu ni wakati polisi wakiwa katika harakati za kusaka wanachama wa mungikina watu wakiwa wamelazwa chini kungoja kuojiwa.
Picha ya pili chini ni baadhi ya mabaki ya watu waliosadikiwa kuuwawa bila kujulikana nani muaji.
Matembezi ya mfalme wa Uispania, kwa leta wasiwasi " Morokko".
Mfalme wa Morokko, bwana Mohammed VI, kitendo cha mfalme wa Uispana bwana Juana Carlos, kutembelea miji ya Ceuta na Melila ni kuleta mgongano kati ya nchi hizi mbili, na kuzidisha utata wa uhusianao uliopo kati ya Wamorokko na Waispania.
Mfalme Mohmmed VI aliongeza kusema, kutembelea kwa mfalme wa Uispania kumezidi kunyong'onyesha uhusianao uliopo kati ya Morokko na Uispania.
Maeneo haya yamekuwa kiini cha mgogoro wa muda mrefu kati ya Wamorokko na Waispania, kwani kila nchi imekuwa ikidai maeneo haya ni yake.
Hapo juu pichani ni wana nchi wa Morokko wa kijiandaa kuandamana, kupinga kitendo cha mfalme wa Uispania kutembelea miji ya Ceuta na Melilla.
Historia ya waafrika kigezo chake ni kuthamini mababu zetu waliopita.
Historia ya Mwafrika ni nguzo ya kujivunia, haya yalithibitishwa na wana historia wa Misri(EGYPT), walipo uonyesha kwa jamii kwa mara ya kwanza, mwili wa mfalme kijana,ambaye alifahamika kama mfalme Tutankhamun.
Maoneshao haya, yalifanyika kwe kaburi lake la kifalme ambalo lipo Luxor's Valley.
Haya yalitokea wakati wana historia walipokuwa wana uweka mwili wa mfalme Tutankhumun sehemu ambayo ni bora zaidi
Mfalme huyu alitawala miaka 3000 iliyo pita, na naaminika alikuwa n nguvu nyingi za kiutawala.
Pichani hapo juu ni picha za mfalme Tutankhamun, ya kwanza kulia ni kichwa chake kabla ya kutengezezwa, pili kushoto ni kabla ya kutengezwa.
Chini ni mwili wa mfalme Tutankhamun akiwa amelazwa sehemu mpya kwenye maonyesho hivi karibuni.
Biashara ya sigara ni madhara kwa Afrika " Serikali ya Nigeria".
Serikari ya Nigeria, imelifungulia mashitaka, shirika moja la kuzalisha na kuuza sigareti BAT ambalo lipo nchini humo.
Serikali ya Nigeria inadai $million 40. kama fidia.Na vilevile kuomba vyombo vya sheria kupiga marufuku matangazo ya sigara nchini humo kwani hazionyi jamii kuhusu madhara ya sigara.
Akisisitiza, msemaji wa serikali alisema, matangazo ya sigara yamekuwa ya kipigwa marufuku kwenye nchi zinazo endelea, na sasa wanajaribu kutangaza biashara zao barani Afrika, amabako nchi nyingi bado hajizifanya uchunguzi wa madhara ya sigara.
Hatua hii imekuja baada ya kugundulika ya kuwa kampuni hii inatumia saana kutangaza bidha aina ya sigareti kupita kiasi, na kufanya mpaka watoto wadogo waanze kuvutiwa na matangazo hayo na kuanza kuvuta sigara.
Pichai hapo juu ni mmoja wa watoto wadogo wakitoa alama ya kuvuta sigara, huku mwenzake akiabasamu.
Hatutawacha peke yenu,tupo bega kwa bega"rais Nicolaus Sarkoz"
Rais wa Ufaransa bwana, Nicolaus Sarkozy, ameliambia bunge la Kongresi la Amerika, yakuwa Ufaransa, itakuwa bega kwa bega na Amerika katika kuijenga Afganistani, na Ufaransa aitaiacha pekee Amerika katika vita nchini humo.
Rais, Sarkoz, aliongeza kwa kusema ya kuwa Afganistani ni nchi muhimu kwa Umoja wa NATO na Atlantiki kwa ujumla.
Vile vile aliongeza, ya kuwa hakubaliani na, Irani kuwa na uwezo wa nguvu za kinyuklia.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Ufaransa bwana Sarkoz, akihutubia bunge la Kongresi hivi karibuni.
Kazi ya kujenga Upya Liberia,yatambulikana kote duniani"WalaLiberia"
Rais wa Liberia, bi elen Johnson, ametunukiwa medali ya Uhuru, serikali ya Amerika kwa jitihada zake za kuijenga Liberia.
Liberia nchi ambayo kwa kipindi kisichopungua miaka zaidi ya kumi ilikuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Amani nchini Libria ilirudi, baada ya ais wake wa zamani bwana Charles Tylor, kukubali kutoka madarakani, kuokana na shinikizo la kimataifa.
Na ndipo bi, Ellen alipochaguliwa kuwa rais wa Liberia, na kwa kipindi hiki chote tangu aw rais bi Ellen amejitaihidi kusawazisha, na kuweka sawa hali za wananchi wa Liberia kwa kiasi fulani, hasa kiuchumi na kijamii.
Pichani hapo juu rais, wa Liberial bi Ellen akipongezwa na rais wa Amerika bwana George Bush ,baada ya kumaliza kumtunukia nishani hii ua Uhuru.

No comments: