Saturday, November 10, 2007

Nchi wanachama kukubaliana kupinga adhabu za vifo?" UN"

Nani kama Ruud Gullit? Acholile kachola, soka bado ya muhitaji.

Mwana soka bora wa Ulaya 1987, Ruud Gullit na amechaguliwa kuwa kocha wa timu maarufu nchini Amerika Los Angeles Galaxy. Gullit ambaye amesha kuwa kocha mkuu wa timu, kama Chelsea, Newcastle United,na Feyenoord ametambulishwa mbele ya viongozi na wapenzi wa timu hiyo hivi karibuni. Kuchaguliwa kwa Gullit, kunaongeza umaarufu wa timu hii, ambayo tiali ina mchezaji maarufu na kaptaini wazamani wa timu ya Uingrereza David Beckham ambaye alijiunga na timu hii kwa mkataba wa miaaka mitano. Pichani hapo juu ni kocha Gullit, alipo tambulishwa mbele ya wapenzi na wanachama wa timu ya Los Angels Galaxy.
Bado nipo gado, upepo hautashinda mwili wangu nguvu "Haile"
Mwana riadha bingwa wa dunia wa mbio ndefu Haile Gebrselassie mwenye miaka 34, amesema bado mwili wake una mruhusu kushiriki mashindano ya riadha.
Akiongea na waandishi wa habari, aliongezea ya kuwa kiafya na kimwili bado nipo gado, na nitashiriki mashindano ya riadha kwa ajili ya nchi yangu Ethiopia na kuwa karibu wa wananchi wenzangu.
Gebrselassie, alisema mtu aliyempa moyo ni Miruts Yifter aliyeshinda mbio za olimpiki Moscow.
1992, Haile Gabrselassie, alishinda kwa mara ya kwanza mbio za dunia za vijana na hapo ndiyo mwanzo wa kuwa bingwa wa dunia hadi hi leo ya pata miaka kumi na sita. Hapo juu Haile Gabrselassie akiwa kazini kuwani kuvunja rekodi yake ya dunia ya mita 5000.
Nchi wana chama kukubaliana kupinga adhabu za kifo? " UN"
New York, Umoja wa Mataifa, unatarajiwa kupiga kura kupinga dhabu ya kifo zinazo pitishwa na nchi wanachama wa Umoja huu.
Inaamiika ya kuwa nchi kati ya themanini na mmoja kati ya nchi mia mmoja tisini na mbili, ambazo ni wanachama wa UN, zina kubaliana na mswada huu wa kupinga adhabu hii ya kifo kutolewa na nchi wanachama.
Na mswada huu utapigwa kura hivi karibuni wakati nchi wanachama UN watakapo kaa kujadiri swala hili.
Nchi mia moja na thelathini zimesha futa adhabu hii ya kifo, na ni nchi ishirini na tano tu ndizo zilizo nyonga watu mwaka jana. Pichani hapo juu ni ndani ya UN, ambapo miswada hupitishwa kurekebisha dunia na watu wake.
Sasa siyo soka tu kwa Brazil, bali wamepata kiungo cha dunia, nani wa kuwazuia?
Wakati dunia ikiwa inatafakari jinsi gani kudhibiti utumiaji wa mafuta yanayo tumika katika kuendeshea mitambo na magari.
Nchini Brazil kumekuwa na furaha na chereko nyingi, baada ya wataalamu wa madini wa nchini humo kugundua eneo lenye mafuta mengi, yatakayo ongezea ongezeko la mafuta yatakayo sadia katika matumizi ya kuendesha mitambo na magari.
Msemaji wa kampuni ya mafuta ya Brazil, Petrobras amesema mafuta hayo yamepatikina karibu na ufukwe wa bahari wa Tupi, ujazo wake ni kiasi cha magaloni billion 5 na billion 8, na mafuta haya hayatahitaji kuchujwa saana kwani yananekana kutokuwa na matope mengi.
Kufuatia kugunduika huko Brazil, itakuwa mmoja ya nchi zitoazo mafuta kwa wingi duniani kuzifutia nchi za Venezuela,na Saudi Arabia. Pichani, katikati ni rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, akionyesha vidole vya gumba, kuonyesha ya uwa mambo yamekuwa swafi saana kwa uchumi wa Brazil, huku amezungukwa na wataalamu wa madini baada ya ugunduzi huo.
Uzembe na kutokuwa makini ni chanzo cha kupoteza maisha ya Mbrazil"IPCC"
Polisi wa jiji la London, wakutwa na makosa ya uzembe ambayo yangewza kuepukwa kama wangekuwa makini, na wasinge kupoteza maisha, kwa kumpiga risasi raia wa Brazil kwa jina Jean Charles de Menezes aliye kuwa mkazi wa jiji London kwa kudhaniwa ni mmoja wauji wa kujitolea muhanga. .
Kufuatia ripori iliyo tolewa na (IPCC) Independent Police Complaints Commision , imesema amri ya kushuti na kuuwa ambayo walipewa polisi ndiyo chanzo cha kifo cha Menezes
Pia kulipitishwa tako la kutaka mkuu wa polisi wa Metropolitan bwana Ian Blair ajiudhuru kwa kufanya uchunguzi wa kesi hii ,kuwa mgumu.
Lakini bwana Blair alikataa tamko hili la kutaka ajihudhuru.
Pichani hapo juu ni marehemu Jean Charles de Menezes aliye uwawa na polisi jiji London
Tunaomba ajihudhuru kwa kuatarisha amani ya dunia" Israel"
Makamu wa waziri mkuu wa Israel bwana Shaul Mofaz, ameomba mkurugenzi wa maswala ya kuchunguza Nyuklia, bwana Mohamed Elbaradei ajiudhuru kwa kudharau amani ya dunia.
Aliyaongea hayo alipokuwa mjini Washington, alisisitiza kwa kusema bwana Alberadei, amekuwa akiongele ya kuwa Iran siyo tishio kama inavyo daiwa na jumuia ya kimataifa, bali Iran inajenga mitambo ya nyuklia kwa ajili ya matumizi ya nguvu za umeme wala siyo bomu.
Israel ni mwanchama wa IAEA( International Atomic Enegy Agency), lakini siyo mwana chama wa kuzuia kusambazwa nguvu za kinyuklia. Pichani viongozi wa Israel wakiwa kwenye mkutano kujadili hali halisi ya kiusalama.
Hali hii ni mbaya kwa wana nchi wa Zimbabwe" Yar Adua"
Rais wa Nigeria, bwana Amuru Musa Yar Adua, amekemea matendo ambayo yanaokea nchini Zimbabwe, na kuomba inabidi hali hii iliyopo Zimbabwe ibadilike. Aliyaongea hayo alipo kuwa akiongea na viongozi wa Ujerumani wakiongozwa na rais Horst Kohler.
Pichani rais Yar Adua, akiongea na waandishi wa habari, wakati aliopo tembelea Ujerumani.
Kichwa bado kinawauma NATO, Taribani na wenzake waongezeka?
Wanajeshi sita wa Amerika ambao wapo chini ya NATO na wanajeshi watatu Afghanistani , wamefariki dunia, baada ya kuvamiwa na na wanamgambo wa Talibani wa kishirikana na Alkaida.
Wanajeshi hawa walivamiwa walipokuwa wanafanya doria mashariki mwa Afghanistani.
Msemaji wa NATO, alisema mmoja wa wanamgambo hawa aliuwawa, baada ya wanajeshi wa NATO, kujibu mashambulizi hayo.
Inasadikiwa mpaka sasa askari wapatao 100 wa Amerika, toka mwaka 2007 uanze.
Hapo juu pichani ni mwanjeshi wa NATO kila doria huku akiwa ndani ya helkopta hivi karibuni.
Kama UN, inashindwa nani wa kula mfupa huu wa Kisomalia?
Dunia, ikiwa imeshkwa na butwaa, na kutokujua nini la kufanya , ili kuleta amani nchini Somalia, hali imezidi kuwa mbaya, baada ya wanchi wa Somalia kushuhudia miili ya askari wa Ethiopia, ikiburuzwa miitani. na kukumbushia hali kama hii iliyo tokea 1993,baada ya majeshi ya Amerika kujitolea kuleta amani, lakini kukutana na upinzani mkubwa, ambao ulipelekea kuangushwa kwa helkopta, na maaskari wa Amrika kuuwawa na baadayekuburuzwa mitaani.
Miili ya askari hawa marehemu ambao walifarika baada ya mapigano makali kati ya majeshi yanayo pinga serikali ya mpito ya Somali, na yale ya serikali yanayo ongozwa kwa usaidizi wa majeshi ya Ethiopia.
Akiongea hivi karibun katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki Moon." Hali ya nchi ya Somalia, imekuwa ngumu ki amani, na nivigumu kwa nchi yoyote kujitolea kupeleka jeshi au wafanyakazi wa kutoa misaada nchini Somalia".
Picha apo juu ni wana nchi wa Somalia wakionyesha hasira zao mitaani baada ya majeshi ya Ethiopia kuuwa watu ambao siyo wapinzani wa serikali, baada ya kitendo cha askari wenzao kuburuzwa mitaani.
Mkutano wa, Annapolis Maryland kuwa matumaini ya taifa la Wapalestina " Rice".
Waziri wa mashauri ya nchi wa Amerika, bi, Condoleezza Rice, amesema ya kuwa, Taifa la wana Wapaestina lita kuwa huru, muda si mrefu.
Aliyaongea hayo mbele ya waandishi wa habari, baada ya kumaliza mazungumzo na rais wa baraza la Wapalestina bwana Mohmoud Abbas.
Aliongeza kwa kusisitiza ya kuwa mkutano wa Annapolis Maryland, uakuwa ndiyo msingi wa kuanzishwa kwa taifa la Wapalestina, ambao wataishi kama majirani wa taifa la Israeli.
Pichani hapo juu ni bi, Condeleezza Rice, na rais Mahmoud Abbas walipo piga picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu hali livyo kwa Wapalestina.

No comments: