Thursday, April 9, 2009

Swala la nguvu za nyuklia ni kitendawili kwa Iran, Amerika na washiriki wake.

Kim Jong Il, achaguliwa kuwa rais wa Korea Kaskazini tena.

Pyongyang,Korea ya Kusini - 09/04/09.Kiongozi wa Korea ya Kaskazini,Kim Jong Il, amechaguliwa tena kuwa kiongozi na rais na bunge la nchi hiyo.
Kim Jong Il, alikuwa anashikilia madaraka yaliyo achwa na baba yake Kim Il Sung alifaliki dunia 1994, alikuwa ka rais wa mpito.
Kwa kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, atakuwa ni kiongozi wa jeshi la Korea ya kaskazini.
Picha hapo juu, anaonekana akikagua jeshi, ambalo kwa sasa litakuwa chini yake.
Picha ya pili, wanaonekana, baadi ya wanchi wakiwa katika moja ya sherehe za kitaifa nchini Korea ya Kusini.
Swala la mguvu za nyuklia ni kitendawili kwa Iran, Amerika na washiriki wake.
Isfahan,Iran 09/04/09 - Rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad, amefungua rasmi mtambo kutengenezea nguvu za kinyuklia, katika mji wa Isfahan.
Katika sherehe ya ufunguzi wa mtambo huo, rais wa Iran, alisema mazungumzo ni lazima yawe ya faida kwa pande zote mbili na siyo kwa faida ya upande mmoja tu
.
Rais, Mahmoud Ahamadinajad, alisema hayo,kuonyesha ya kuwa, maelezo yaliyo tolewa na rais wa Amerika , Baraka Obama hivi karibuni,hayakuwa kizuizi cha Iran kuendelea kiteknolojia katika nyanja za matumizi ya nguvu za nyuklia.
Huku akisisitiza, rais ,wa Iran , alisema, mazungumzo kati ya Amerika na Iran katika swala la nyuklia, yanatakiwa yawe ya kisheria za kimsingi, na siyo Amerika nchi ye nye nguvu kutumia,chombo cha kutathmini nguvu kusimamisha maendeleo ya Iran kiteknolojia.
Hata hivyo , rais wa Amerika, alionya ikiwa Iran, inatakakuwa na uhusiano mzuri na Amerika na jumuia ya kimataifa ni lazima isimamishe mpango wake wa kuendeleza kuzalisha nguvu za kinyuklia.
Picha ya hapo juu, anaonekna rais, wa Amerika , Baraka Obama, akiongea katika moja ya mkutano na wandishi wa habari, wakati wa ziara yake ya kwanza katika bara la Ulaya tangu kuwa rais wa Amerika.
Picha ya pili , ni ya rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, akiongea mara baada ya kufungua mtambo mpya wa kuendeshea nguvu za kinyuklia katika mjin wa Isfahan.
Utata wa kisiasa nchini Georgia, waleta mshaka kwa rais.
Tiblisi, Geogria -09/04/09 - Hali ya kisiaasa nchini Georgia imeendela kuwa ya utata , baada ya mamia ya fuasi wa vyama vya upinzani na viongozi wao wameaaandamana hadi kwenya maeneo ya bunge kwa madai razima rais Mikheil Saakashvili, ajiudhulu kutaka madarakani kwa kushindwa kutekeleza ahadi alizo zihaidi kabla ya uchaguzi nakuwa na ukilitimba wa madaraka.
Akiongea hayo wakati wa maandamano hayo,Levan Gachechiladze, ambaye alikuwa mgombea mpizani wa kiti cha urais wa Georgia, alisema watakaa mbele ya bunge mpaka hapo, rais atakapo sikiliza hoja za wananchi.
Hata hivyo wakati viongozi wa vyama vya upinzani wanafanya maandamano , rais Mikheil Saakashvili alikuwa akiwahutubia wanchi wa Georgia kwa kusisitiza umoja kwa wanchi wa Geogria,katika kumbukumbu za kuazimisha tangu, Georgia ilipo kwa moja ya nchi za umoja wa shirikisho za nchi za Kirashia.
Picha hapo juu , ni ya rais wa Georgia, Mikheili Saakshvili, anaye daiwa ajiudhulu toka madarakani na vyama vya upinzani.
Picha pili, wanaonekana wanchi wa vyama vya upinzani wakiandamana kuelekea kwenya ukumbi wa bunge kwa madai ya kuwa ni razima rais ajiudhulu.
Picha ya tatu , wanaonekana mamia ya waandamanaji wakiwa mbele ya bunge la Georgia, wakidai rais ajiudhulu,ndipo watatoka katika eneo hilo.
Wafuasi wa Al Sadr,wataka majeshi ya kigeni yaondoke.
Baghdad,Irak - 09/04/09 - Maelfu ya watu wameaandamana ,kwa madai ya kuwa jeshi la Amerika na washirika wake waondoke nchini humo.
Wafuasi na mwadau wa kiongozi wa Shia Murtada al Sadr, ambaye anajulikana kupinga kuwepo kwa majeshi ya kigeni, walionekana wakiwa wameshikilia mabango ya picha ya kiongozi huyo na huku wakidai ni lazima majeshi hayo ya kigeni yaondoke.
Waandamanaji hao wakikusanyika katika mnara wa aliyekuwa rais wa Irak , hayati Saddam Hussein, ambapo mnara huo, uling'olewa na jeshi la Amerika,mara baada ya kufanikiwa kuianguha serikali ya rais Saddam Hussein.
Irak,imekuwa chini ya majeshi ya kigeni kwa kipindi cha miaaka sita, tangu kuuangushwa kwa aliyekuwa rais wa Irak, Saddam Hussein na jeshi la Amerika na washirika wake.
Picha hapo juu wanaonekana waandamanaji wakiwa wameshikilia mabango na bendera katika moja ya mtaa mjini Baghadad.

No comments: