Thursday, April 2, 2009

Viongozi wa dunia wakubaliana kuikomboa dunia kiuchumi.

Viongozi wa dunia wakubaliana kuikomboa dunia kiuchumi.

London,Uingereza - 02/03/09.Viongozi wa nchi G20 (nchi tajiri na zili zilizoendelea kiuuchumi) zilizo udhulia mkutano ili kujadili kuokoa dunia kuanguka kiuchumi, kwa kuamua kwa pamoja kuwekeza fadha kiasi cha $ 1trillion kwa ajili ya IMF (Internationl Monetary Fund),na benk ya dunia, ili ziweze kuzisaidia nchi ambazo zimeasilika vibaya na mporomoko wa uchumi ambao umeikumba dunia.
Kikao hicho ambacho kimewafanya viongozi wa dunia, wakutane baada ya dunia kukumbwa na mporomoko wa kiuchumi tangu miaka 1930s.
Akifunga kikao,hicho cha G20, waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, ambaye ndiye aliyekuwamwenyeji na mwandalizi wa kutano huu, alisema, zimekubaliana kwa pamoja yakuwa zitachapisha majina ya maeneo ambayo kodi huwa hazilipwi na wawekezaji, na kuhakikisha ya kuwa , hali hii haitarudia tena, kutakuwa na vikwazo kwa wale wote watakao kiuka makubaliano haya.
Vilevile, usili na uficho wa mabenki umefikia mwisho,na lazima uachwe kabisa na wale wote wanaofikilia kuendelea basi wajue jumuia ya kimataifa hatawaachia.
Picha hapo juu , wanaonekana viongozi wa G20,walioudhulia mkutano London 02/04/09, wa kuikwamua dunia kiuchumi wakiwa pamoja kabla ya kuagana baada ya kumaliza mkutano.
Picha ya pili, anaonekna waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, akielekea kwenye jukwa ili kufunga mkutano wa G20.

No comments: