Sunday, April 19, 2009

Makampuni yaliyo shiriki katika ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini yanaweza kushitakiwa.

Ukame wa waanza kusogelea Afrika ya Magharibi. Akkra, Ghana - 19/04/09.Wataalamu wa sayansi ya mazingira nchini Ghana wamesema huenda ikawa na hali ya ukame zaidi hapo mbeleni, kwa kufuatia uchunguzi wa kisayansi uliofanywa kwa kulinganisha karne ya 20 na karne tuliyo nayo sasa. Kwa mujibu wa kituo kimoja cha sayansi kilichopo nchini humu(Ghana) kinasema hii ni kutokana na utafiti uliofanywa katika ziwa Bosumtwi lililopo nchini Ghana. zimeonyasha tofauti kubwa kulingana na za karne za nyuma. Hata hivyo, wanasayansi walisema yakuwa,bado itachukua muda hali kuwa mbaya zaidi kwa kuzingatia mvua na maeneo ya kijiografia yaliopo katika nchi hizi. Picha hapo, juu ni ya ramani ya Afria ya Magharibi, eneo ambalo wanasayansi wanasema hali ya ukame inalinyemelea kwa mbali.

Mmoja ya washukiwa wa ulipuliwaji wa Msikiti mkubwa aachiwa kwa dhamana Pakistan.
Islamabad,Pakistan - 19/04/09.Mahakama nchini Pakistan, imemkubalia dhamana, kiongozi mmoja wa mlango wa kushoto wa kundi la Taliban, Maulana Abdul Aziz,baada ya kuwekwa jela kwa kipindi kisicho pungua miaka miwili,baada ya kushukiwa kuhusika na mauaji ya ulipuaji wa msikiti mkubwa uliokuwepo Red Square mwaka 2007.
Maulana Abdul Aziz,ambaye ni mmoja ya viongozi ambaye anapendelea kuwepo na sheria za kidini nchini Pakistan na kupinga kwa kuwepo kwa majeshi ya kigeni hasa ya Amerika na washiriki wake katika maeneo hayo.
Hata hivyo , baada ya kutoka jela, Maulana Abdul Aziz alihutubia mamia katika eneo la msikiti uliolipuliwa wa Red Square, alisema, atakubali tena vita vya kuwa lipua Waislaam wenzake, lakini vita bado vitakuwa vya amanim, kwani mapambano bado yanaendelea.
Picha hapo juu anaonekana, Maulana Abdul Aziz, akitoka jela ambapo alikaa kwa muda wa miaka miwili.
Picha ya pili,wanaonekna baadhi ya waumini wa kiswali huku wamelizunguka gari, lililo tobolewa kwa risasi, wakati wa mashambulizi ya mwaka 2007 ya ulipuliwajiwa msikiti wa Red Square.
Katibu mkuu mpya wa NATO, anawakati mgumu bele yake.
Kabul, Afghanistan - 19/04/09. Kundi la Taliban, lililopo nchini Afghanistan, kimesema ya kuwa katibu mkuu mpya wa NATO,Anders Fogh Rasmussen, ni adui wa Waislaam, baada ya kushindwa kuchukua hatua yoyote kwa wale wote walio husika na uchoraji wa katooni za kumkashifu Mtume Mohammed nchini mwake, akiwa kama kiongozi wa serikali.
Hata hivyo, Anders Fogh Rasmussen, ambaye alisema ya kuwa katiba haimruhusu yeye kuingilia maoni ya mtu, kwani atakuwa amekiuka haki inayo mruhusu mtu kuongea anachotaka kwani ni uhuru wa mtu kuongea anavyotaka kwa kutokana na katiba inavyosema.
Picha hapo juu, anaonekana , Anders Fogh Rasmussen, ambaye amechaguliwa kuwa katibu mkuu mpya wa NATO hivi karibuni.
Sudan yakubali kurejea kwa baadhi ya mashirika ya kigeni,"Asema , Seneta John Kerry".
Khartoum,Sudan - 19/04/09.Serikali ya Amerika imetuma ujumbe wake wa juu kabisa nchini Sudan, li kutathmini hali halisi ya nchi hiyo hasa katika eneo la Darfur.
Ujumbe huo, unao ongozwa na, Seneta, John Kerry, ulizungumza na viongozi wa serikali ya Sudan kwa undani zaidi,ili kuweza kutatua hali halisi ya mvutano kati ya serikali ya Sudan na mahakama ya kimataifa inayo shughulikia kesi za kivita na haki za binadamu iliyopo nchini Nederland kutoa hati ya kukamatwa kwa rais, wa Sudan, Omar Al Bashir na kufukuzwa kwa mashirika ya kigeni ambayo yalikuwa yanatoa misaada kwa wakazi wa eneo la Darfur.
Picha hapo juum anaonekana, Seneta, John Kerry, akiongea na makamu wa rais, wa Sudan, Ali Osman Mohammed Taha, wakati walipo kutana hivi karibuni mjini Khartuom kwa mazungumzo.
Makampuni yaliyo shiriki katika ubaguzi wa rangi nchini Afrika ya Kusini yanaweza kushitakiwa.
New York, Amerika - 19/04/09.Mahakama ya Amerika, imekubali ya kuwa watu wote walio athirika wakati wa utawala wa kibaguzi wa serikali ya Afrika ya kusini, wanaweza kuishitaki kampuni za General Motors, BMI na nyingine zilizo husika katika kushiriki kukiuka haki za kibinadamu.
Mahakama hiyo iliyopo New York, ilisema ya kuwa, General Motors ilikuwa inajua fika ya kuwa magari yake yalikuwa yanatumika wakati wa utawala wa kibaguzi nchini Afrika ya Kusini, kuwakandamiza watu waliowengi.
Vilevile mahakama ilisema ya kuwa IBM, ilikuwa inajua yakuwa mitambo yake ya mtandao, ilikuwa inatumika katika kubagua na kutenganisha weusi na weupe kwa kuweka repoti.
Uamuzi huo umekuja, baada ya mahakama kuona ya kuwa makampuni hayo yanaweza kushitakiwa, kwa kufuatia sheria ambayo inaruhusu makampuni ya Amerika kushitakiwa nje ya Amerika, ikiwa kesi hizo zitaletwa katika mahakama ya Amerika.
Picha hapo juu, ni bendera mpya Afrika ya Kusini, nchi ambayo wananchi wake wamekandamizwa na kunyanyaswa kwa muda mrefu na serikali ya kibaguzi wa Wazungu wachache , kwa kupitia au kutumia teknolojia zilizo tolewa na baadhi ya makampuni ya kimataifa zikiwemo IBM na General Motors na mengine mengi.
Rais wa Paraguay, Fedrinando Lugo, akubali yaliyosemwa na redio.
San Pedro, Paraguay - 19/04/09.Rais wa Paraguay, Ferdinando Lugo, amekili ya kuwa yeye ndiye baba ya watoto wawili,ambapo hapo mwanzo alikanusha baada ya redio moja kutangaza ya kuwa alikuwa rais Ferdinando Lugo, anawatoto wawili ambao amezaa na mwanake mwenye miaka 26,Viviana Rosalith.
Rais , Ferdinando Lugo, ambaye , hapo mwanzo alikuwa ni Askofu wa kanisa Katoliki katika jimbo la San Pedro,kwa kipindi cha miaka kumi, kabla ya kuamua kuacha kazi ya ukasisi na kuingia katika siasa.
Kwa mujibu wa redio, hiyo ilisema ya kuwa, rais Ferdinando Lugo ,alizaa na Viviana Rosalith wakati bado akiwa kama askofu wa jimbo la San Pedro.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Paraguay, Ferdinando Lugo, akitoa heshima katika moja ya sherehe za kitaifa hivi karibuni.
Picha ya pili anaoneka, Ferdinando Lugo, akionekana kukusalimia, baada ya kumaliza kuapishwa kuwa rais wa Paraguay, mwezi wa nne mwaka jana.
Rais wa Bolivia, asimamisha mgomo wa kula.
La Paz, Bolivia - 19/04/09.Rasi wa Bolivia, Evo Morales,amesimamisha mgomo wake wakukataa kula hivi karibuni, baada ya bunge kupitisha sheria ya kumruhusu kugombea tena kiti cha urais unao tarajiwa kufanyika mwisho wa mwaka huu 2009.
Hata hivyo viongozi wa vyama vya upinzani walijitahidi kupinga mswada huo, kwa madai ungempa rais, Morales, nafasi nyingine ya kuiongoza nchi hivyo.
Picha hapo, juu anaonekana , rais Evo Morales, akiwa amekaa mara baada ya bunge kupitisha mswada wa kumruhusu rais, kuweza kugombea urais kwa mihula miwili.
Picha ya pili, aneonekna ,rais Evo Morales, kulia akiwa amelelala chini na baadhi ya wanchama wenzake kwenye chumba
, wakati walipo fanya mgomo wa kula chakula,ili bunge kupitisha sheria mpya ya urais.
Hatuna mpango wa kuleta machafuko au mashambulizi nchini Misri.
Beiruti,Lebanoni - 19/04/09. Kiongozi wa kundi la HezbollahHassan Nasrallah, lililopo nchini Lebanoni. amekanusha ya kuwa kundi lake halina mpango wa kuleta machafuko au mashambulizi nchini Misri.
Alikuwa akiyaongea hay hivi karibununi , baada ya serikali ya Misri kudai ya kuwa kundi la Hezbollah, lina mpango wa kushambulia nchini Misri, baada ya kuwakamata watu 49, na mmoja wao inasemekana ni wanachama wa kundi la Hezbollah
Picha hapo juu, anaonekana kiongozi wa kundi la Hezbollah,akiongea kupitia lunginga, kukanusha habari ya kuwa kundi lake lina mpango wa kuleta machafuko nchini Misri.

No comments: