Wednesday, April 8, 2009

Rais wa zamani wa Peru aongezewa miaka 25 zaidi kukaa jela.

Tetemeko la ardhi la leta maafa nchini Itali.

Rome Itali - 08/04/09.Idadi ya watu waliokufa kutokana na maafa ya tetemoko la ardhi lililo tokea katika mji wa L'Aquila mji uliopo karibu na Rome wamefikia 260.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu, kunaidadi ya watu 30,000, ambao wamepoteza makazi yao kutokana ma tetemeko hilo lililo kuwa na nguvu ya 5.6 magnitude.
Meya wa L'Aquila, alisema tetemeko hilo lilitokea usiku wa manane wakati watu wakiwa wa melala.
Picha hapo juu, yanaonekana matenti ambayo yanatoa huduma ya kwanza kwa watu walio kutwa na maafa.
Picha ya pili anaonekana, mmoja ya wahudumi wa huduma ya kwanza akijaribu kumtuliza mmoja mkazi aliyekumbwa na maafa.
Rais wa zamani wa Peru, aongezewa miaka 25 zaidi kukaa jela.
Lima,Peru - 08/04/09.Mahakama nchini Peru, imetoa adhabu ya kifungo cha miaaka 25, kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Alberto Fujimori ambaye kwa sasa anamiaka 70.
Rais huyo wa zamani, ambaye kwa sasa,alikuwa anatumika kifungo cha miaka sita baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya awali.
Hukumu hiyo ,ilitolewa baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji, utekaji nyara, na kukiuka haki za binadamu wakati alipo kuwa madarakani wakati wa miaka ya 1990s.
Hata hivyo , rais huyo wazamani amekuwa akikana mashitaka yake hayo. Picha ya hapo juu anaonekana, rais wa zamani wa Peru, akiongea enzi za utawala wake alipokuwa rais wa Peru.
Picha ya pili, anaonekana mmoja ya wapenzi na mdau wa uongozi wa rais wa zamani wa Peru,akilalamika kwa uchungu mara baada kuhukumiwa na mahakama nchini Peru.
Hali ya kisiasa nchini Thailand yaanza kuyumba tena.
Bang Kok,Thailand - 16/04/09. Waandamaji wanazidi kuandamana nchini Thailand, kudai waziri mkuu Abhisit Vejjajiva, ajiudhulu kutoka madarakani.
Waandamaji hao wapatao 300,000, waliovalia shati za rangi nyekundu, walionekana wakiwa na mabango, huku wakidai wanataka waziri wao wa zamani, Thaksi Shinawatra aliyepo ukimbizini, arudishwe madarakani.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja wa waandamanaji anaonekana akipiga kerere kudai serikali ijiudhulu.
Picha ya pili, wanaonekana waandamaji wakielekea mjini kuandamana.

No comments: