Monday, April 27, 2009

Mafua ya nguruwe yaiweka dunia njia panda.

Mafua ya nguruwe yaiweka dunia njia panda.

Mexico City,Mexico 27/04/09.Mlipuko wa ugonjwa wa mafua ya nguruwe, umeiweka dunia katikahali ya taadhali, baada ya watu wapatao 149 kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo, na wengine kwa mamia kuugua kutokana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa waziri wa afya wa Mexico, Jose Angel Cordova, serikali ya Mexico kwa kushirikiana na shirika la afya ulimwenguni WHO, zinajitahidi kuzuia ugonjwa huo usienee na tiba yake inatolewa mara moja pindipo atakapo patikana mgonjwa.
Picha hapo juu wanaonekana abiria wakiwa katika treni, anaonekana mmoja ya askari akigawa dhana za kukingia mdomo kwa abiria waliomo ndani ya treni.
Picha ya pili, wanaonekana, askari wakiwa katika kwata , huku wakiwa wamevaa midononi na puani dhana za kukinga ugonjwa usiwakumbe wakati wakiwa kazini.
Mashindano ya siraha,huenda yaka anza Mashariki ya Kati.
Dubai, UAE - 27/04/09. Serikali ya UAE, imeongeza uwezo wake wa kijeshi,kwa kununua zana za kijeshi ili kuongeaz uwezo wake wa kijeshi, kufuatana na wakati.
Kwa mujibu wa ripoti zilizo tolewa na shirika la kimataifa linalo shughulikia, maswala ya amani na zana za kivita (SIPRI - Stockholm International Peace Research), limesema ya kuwa UAE, kwa muda wa miaaka isiyo pungua kumi, UAE imepanda kuwa nchi ya 15 duniani kwa kununu siraha na teknolojia za kivita.
Kufuatia hali hii, shirika hilo, linasema kunaweza kuleta mashindano ya zana za kivita katika eneo la Mashariki ya Kati.
Picha hapo juu, ni moja ya gwaride la wanajeshi wa UAE, wakiwa katika moja ya sherehe za kitaifa,na kwa upande wa kushoto ni moja ya siraha ambazo UAE, inazo katika himaya yake.
Picha ya pili, linaoneka bomu likiwa linatoka kwenya mtutu, kuelekea lilipo lengewa wakati wa mazoezi ya kivita.
ANC ya pata ushindi kwa mara nyingine tena "Tayari kuongoza serikali".
Johannesburg,Afrika ya Kusini - 27/07/09. Matokeo ya uchaguzi mkuu, ulifanyika Afrika ya Kusini, kumeipa chama tawala cha ANC ushindi kwa mara ya tatu tangu kukomeshwa kwa utawala wa wazungu wachache.
Ingawaje katika uchaguzi huo, chama cha ANC, hakikuweza kupata vingi wa viti katika bunge ambavyo vingewezesha ANC kuweza kubadilisha katiba ya nchi.
Katika uchaguzi huo,ANC ilipata 65% sawa na viti katika bunge 264 kati ya viti 400,vilivyopo katika bunge.
Picha hapo juu, inaonekana bendera ya Afrika ya Kusini, nchi ambayo ilikuwa chini ya utawala wa wazungu wachache kwa kipindi kirefu.
Picha ya pili,ni ya chama tawala ANC,chama ambacho kilikuwa mstari wa mbele, katika kupinga ubaguzi wa rangi na kupigania haki za Waafrika wa Kusini waliokuwa wakikandamizwa na serikali ya makabulu.

No comments: