Mkuu wa Taliban, atangaza hali ya hatari kwa Amerika.
Washington,Amerika - 01/04/09 - Serikali ya Amerika imetangaz itatoa zawadi ya dola za Kiamerika $ 5 million, kwa mtu atakaye toa habari wapi alipo kiongozi wa Taliban, Baitullah Mehsud, ambaye ametangaza kuwa kundi lake litashambulia Amerika na kuishangaza dunia.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana, zinasema yakuwa kiongozi huyo wa Taliban, alisema ya kuwa kundi lake ndili lililo husika na ulipuaji wa kituo cha polisi mjini Rahore, siku ya jumatatu.
Baitatullah Mehsud, anashukiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistani Bi Benazir Bhutto, na mashambulizi yaliyo tokea katika hotela ya Marriot iliyopo Islamabad.
Na inaaminika anauhusiano wa karibu na kundi la Al Qaeda.
Picha hapo juu ni ya, Baitullah Mehsud, ambaye anatafutwa akiwa hai au amefariki na serikali ya Amerika kwa kuwekewa zawadi ya US dola $ million 5 kwa mtu atakaye toa habari zake ili akamatwe.
Hatimaye Israel yapata waziri mkuu mpya.
Jerusalem, Israel - 01/04/09.Benyamin Netanyahu, ameapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Israel, baada ya kupata baraka kutoka kwa bunge la nchi hiyo.
London,Uingereza - 01/04/09.Rais wa Amrika Baraka Obama, ameanza ziara katika nchi za Ulaya na ataudhulia mkutano wa kiuchuni ambao umeandaliwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Doha,Katar - 31/03/09.Viongozi Latini Amerika na viongozi wa jumuia nchi wanachama wa nchi za Kiaarabu,wamekutana ili kujadili maendeleo na ushirikiano wakaribu.
No comments:
Post a Comment