Thursday, April 23, 2009

Hali ya ukame nchini Kenya huenda ikaleta maafa kwa jamii"UN"

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Amerika lawamani. Washington, Amerika 23/04/09.Aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Condoleezza Rice,inesemekana ndiye aliyetia sahii kuanza kutumika kwa njia ambazo zilikwenda kinyume na haki za binadamu wakati watuhumiwa waliokamatwa kama wahujumu na watu hatari kwa Amerika wakati wa mahijiano katika gereza la Guantanamo Bay. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana, zinasema Bi Rice, alitia sahii ruhusa hiyo mwaka 2002, wakati akiwa mshauri wa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Picha hpo juu, anaonekana, Bi Condeelezza Rice, akiongea katika moja ya vikao wakati alipo kuwa akifanya kazi katika ofisi ya mambo ya ndani ya Amerika. Wahisani wakubali kuisaidia Somalia. Brussels, Ubeligiji - 23/04/09. Kundi la waihisani wamekubaliana kwa pamoja watachanga kiasi cha US$250 million, ili kuisadia Somalia kujenga na kurudisha hali ya kiusalama nchini humo. Wahisani hao walikubali kwa pamoja kutoa mchango huo,kwa kufuatia ombi la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano kuzungumzia hali halisi ya Somalia, hasa kufuatia kuku kwa uharamia. Picha hapo juu wanaonekana, rais wa Somalia, Sheikh Sharif Ahmed ,na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, wakati wa mkutano huo uliofanyika nchini Ubeligiji na wahisani na Umoja wa Mataifa. Uhusiano wa Amerika na Venezuela kuanza upya. Caracas, Venezuela - 19/04/09. Serikali ya Venezuela, imesema ya kuwa itafungua ofisi zake za kibalozi nchini Amerika, ikiwa ni ishara ya kuonyesha yakuwa Venezuela inahitaji kushirikiana na Amerika. Hayo yalizungumzwa na rais wa Venezuela , Hugo Chavez, wakati alipo kutana na rais wa Amerika, Baraka Obama,kwenye mkutano, ulio zishirikisha nchi zililizopo katika bara la Amerika nchi Trinidad na Tobago. Uhusiano wa Venezuela, haukuwa mzuri wakati wa kipindi cha utawala wa rais George Bush, hata kufikia, kufungwa kwa ofisi zote za kibalozi kati ya nchi hizi. Pcha hapo juu ,anaonekana , rais wa Amerika Baraka Obama na rais wa Venezuela, Hugo Chavez, wakiwa wameshikana mikono, wakta rais Hugo Chavez, alipo kuwa akimkabidhi rais Baraka Obama kitabu cha historia ya Watu wa Latini Amerika na maisha yao hadi hivi leo. Picha hapo juu, wanaonekana marais , Hugo Chavez kuliana rais, Baraka Obama kushoto wakiwa mwameshikana mkono wakati walipo kutana nchini Trinidad na Tobago ili kuzungumzia hali ya kiuchumi ya Amerika. Algeria yalaumiwa na Morocco kwa kutaka kuvuruga amani. Rabat, Morocco - 19/04/09. Serikali ya Morocco imeilaumu serikali ya Algeria, kwa kusaidia wapiganaji wa POLISARIO, kuingia karibu na mpaka wa Morocco na kufanya mashambulizi ambayo ayakuleta madhara. Kwa mujibu wa habari zilizo toka ofisi za mambo nchi za nje za Morocco, zilisema wapiganaji hao walipiga risasi ovyo hewani. POLISARIO, ni kundi lililopo kusini magharibi mwa Morocco linalo pigania kujitenga na Morocco. Picha hapo juu ni ramani ya Afrika ya Kaskazini Magharibi,na kusini mwa ramani hiyo, kunaonekana,eneo la Sahara ya Magharibi, ni eneo ambalo kwa muda mrefu linamvutano na mgogoro mkubwa huko kaskazini magharibi mwa bara la Afrika. Hali ya ukame nchini Kenya huenda ikaleta maafa kwa jamii."UN".

Nairobi, Kenya 18/04/09. Hali ya ukame inayo endelea nchini Kenya, imefika hali mbaya, kwa mujibu wa maseami wa shirika linalo shughulikia vyakula Duniani ( WFP - World Food Progamme), Gabrielle Menezes alisema, kufuatia ukame huo, Kenya itakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula,ambapo msaada wa vyakulua hutaitajika.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Kenya nchi ambayo hali ya ukame nchini humo inatishia jamii.
Picha ya pili wanaonekana wa kina mama wakiwametua kupumzika, baada ya kutembea kwa muda mrefu kutoka kutafuta ridhiki.
Wazimbabwe washerekea siku ya uhuru chini ya serikali ya muungano madarakani.

Harare, Zimbabwe - 17/04/09. Viongozi wa vyama pinzani nchini Zimbabwe,Robert Mugabe wa NAZU PF na Morgan Tsvangirai wa MDC, wamechelekea kwa pamoja siku ya uhuru wa Zimbabwe hivi karibuni, tangu kuanzishwa kwa serikali ya muungano.

Sherehe hiyo ambayo ili udhuliwa na viongozi wote wa serikali na baadhi mabalozi huwa inaadhimishwa kila tarehe 17/04/09 ya kila mwaka.

Katika sherehe hiyo, rais,Robert Mugabe , aliwataka wananchi waungane kwa pamoja, kujenga nchi na kuulunda nchi yao

Picha hapo juu ni ya bendera ya Zimbabwe, nchi ambayo ulipata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.

No comments: