Sunday, April 5, 2009

Baraka .H.Obama atangaza kupunguzwa kwa siraha za nyuklia duniani.

Korea ya Kaskazini yarusha chombo chake angani.

Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 04/04/09.Serikali ya Korea ya Kaskazini, imetangaz rasmi yakuwa imefanikiwa kurushwa chombo chake angani saa 0029GMT na kwa sasa kinazunguka dunia.
Chombo hicho kilichorushwa katika kituo cha sayansi cha Musudan- ri, kinasemekana kilipita katika maeneo ya Japan kuelekea maeneo ya Bahari ya Pasifiki.
Kwa mujibu wa serikali ya Korea ya Kaskazini, chombo hicho nikwa ajili ya mawasiliano, na hakipo anga kwa matumizi ya kivita.
Hata hivyo, kurushwa kwa chombo hicho angani na Korea ya Kaskazini, kumeleta wasiwasi, kwa jumuiya ya kimataifa, kwani Korea ya Kaskazini, imekiuka moja ya sheria za kimataifa,kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa.
Picha hapo juu wanaonekana , baadhi ya wana nchi wa Korea ya Kaskazini, wakiangali kwa makini, chombo cha anga kilicho rushwa na walaataamu wa nchi yao.
Picha ya pili, ni ya chombo, cha kurushia mitambo angani, kikiwa tayari kurusha chombo angani, ambacho kipo angani kwa sasa, kwa mujibu wana sayansi wa anga.
Baraka .H.Obama, atangaza kupunguzwa kwa siraha za nyuklia dunia.
Prague,Chech -04/04/09. Rais wa Amerika Baraka .H. Obama, amesema serikali yake itafanya kila jitihada ili kupunguza matumizi ya nguvu za kinyuklia kwa ajili ya kutengeneza siraha, ambazo zitakuja kuleta maangamizi hapo baadaye pindipo zikipitia kwenye mikono potofu.
Rais, Baraka .H. Obama,akiwahutubia maelfu, alisema ni muhimu kwa Amerika kuanza kuongoza katika swala hili la kupunguza siraha za nyuklia, kwa ilisha wahi kutumia siraha hizo, na nilazima nchi nyingine zifuate mfano huo wa Amerika wa kupunguza siraha za nyuklia.
Rais , Obama, alisema ingawaje maangamizi hayo hayatokea wakati wa uhai wake , lakini ni lazima yaanze mara moja, na atahhakikisha serikali yake, itakuwa mstari wa mbele, kwani kwa kufanya hivyo ni kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Picha hapo juu anaonekana, rais wa Maerika , Baraka .H.Obama, akihutubia maelfu waliokuja kumlaki na kumsikiliza, akiongea kuhusu hali halisi ya mabadiliko ambayo walimwengu wanatakiwa kuyafanya ili kuokoa dunia mna mzingira yake yasiharibike, na yatunzwe kwa kizazi kijacho.
Picha ya pili wanaonekana, maelfu waliokuja kumsikiliza rais wa Amerika, Baraka Obama, badaa ya hutuba yake anaonekana rais Baraka .H.Obama, akiwasalimia wananchi kwa kuwapungia mikono.
NATO yatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa"Afghanistan bado kitendawili".
Strasbourg,Ufaransa - 03/04/09.Viongozi wa NATO wakiwa wanaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa NATO, wamekutana nchini Ufaransa, ili kujadili hali halisi ya Afghanistan na kutathmini, mafanikio ya demokrasi yanavyo endelea nchini humo.
Katika kikao hicho viongozi hao wote kwa pamoja walikubalina ni muhimu kujenga Afghanistan, na kuahakikisha hatakuwa tena kwenye mikono ya utawala wa Taliban,na mafanikio hayo yataletwa ikiwa nchi wanachama zitashirikiana kwa zati.
Vilie vile viongozi wa NATO walijadili ni jinsi gani watashirikiana na nchi nyingine ambazo siyo wanachama wa NATO, ili kuweza kuushinda ugaidi unaosumbua dunia.
Picha hapo juu, wanaonekana mawaziri wanchi za nje wakisaini kwa mara kwanza kukubali k,uanzishwa kwa NATO 4/04/1949.
Picha ya pili, anaonekana katibu wa sasa wa NATO, Jaap de Hoop Scheffer, akihutubia viongozi wa nchi wanchama wa NATO, kabla ya kuanza kikao rasmi.
Picha ya pili wanaonekana viongozi wa nchi wanchama wa NATO, wakiwa wamepiga picha kwa pamoja kabla ya kuanza mazungumzo na mjadara wa kuimarisha NATO, tangu miaka 60 ilipo anzishwa.
NATO yapata katibu mpya"Baada ya Uturuki kuridhika".
Brussel, Ubeligiji,03/04/09 - Waziri mkuu wa Denmark Anders Fogh Rasmussen, amechaguliwa kuwa katibu mkuu wa shirikisho la jumuia za nchi zinazo shirikiana kiulinzi na usalama wa nchi wanachama wa Amerika na Ulaya - NATO.
Anders Rasmussen, atachukua ofisi abayo hapo mwanzo ilikuwa ikiongozwa na Jaap Scheffer, ambaye muda wake wakuongoza unakwisha mwezi wa julai (Saba).
Hata hivyo kuchaguliwa kwake, kumekuja baada ya Uturuki, kukubaliana na nchi wanachama,kwani Uturuki ilikuwa ikitaka maelezo zaidi na uhakika kutoka kwa nchi wanchama yakuwa Anders Rasmussen, hatakuwa na msimamo aliyo weka wakati mmoja ya magazeti nchini mwake 2005 yalichapisha picha ta kumkashifu Mtume Muhammed,na hakuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.
Nabaada ya nmaelezo ya kutosha ndipo Anders Fogh Rasmussen, alichaguliwa , na anatarajiwa kuanza kazi rami mwezi wa saba 2009.
Picha hapo juu , anaonekana waziri mkuu wa Den Mark, Anders Fogh Rasmussen, akiongea katika moja ya mikutano ya kimataifa ,kujadili hali ya dunia na maendeleo yake.

No comments: