Monday, June 15, 2009

Ahmadinejad, achaguliwa tena kuwa rais,matokeo ya uchaguzi yaleta sakata Iran.

Muda si mrefu,Waingereza kupata ukweli kuhusu vita vya Irak.

London, Uingereza, 15/06/09. Waziri mkuu wa Uingereza,ametangaza ya kuwa serikali itafanya uchunguzi kwa makini kuhusu kuhusika kwa Uingereza katika vita vya Irak, vilivyo fanyi miaka sita iliyo pita.
Vita hivyo,vilivyoanza mwaka mapema 2003 na kumng'oa rais wa Irak, Saddam Hussein, vimekuwa vikileta joto ya jiwe kwa serikali ya, Gordon Brown na aliye mwachia ofisi, waziri mkuu mstaafaafu, Tony Brair.
Picha hapo juu, anaonekana,waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, ambaye amekuwa na wakati mgumu kutoka kwa wapinzani kudai kuwepo kwa uchunguzi wa Uingereza kuhusika kwa nchi hiyo katika vita vya Irak.
Picha ya pili wanaonekana, wanajeshi wa Uingereza wakiwa wakiwa katika mapambano katika kumng'oa Saddam Hussein.
Ahmadinejad,achaguliwa tena kuwa rais, matokeo ya uchaguzi yaleta sakata Iran.
Tehran, Iran - 15/06/09. Kamati inayosimamia uchaguzi wa Iran, nchini Iran imetangaza ya kuwa rais Mahamoud Ahmadinejad, kuwa mshindi kwa kupata kura kiasi cha 62% zidi ya mpinzani wake Mir Hossein Mousavi, katika kinyanganyiro cha kugombea kiti cha urais wa Iran.
Hata hivyo, baada ya matangazo ya ushindi wa rais, Mahmoud Ahamadinejad,mpinzani wake, Mir Hoeesin Mousavi, amesema yakuwa uchaguzi umekuwa batili na amekata rufaa, kutokubaliana na matokea hayo.
Kufuatia, malalamiko hayo, wasimamizi wa uchaguzi huo, wamesema wanafanya uchaguzi, watautangaza baada ya siku kumi.
Picha hapo juu, anaonekana, ras Mahmoud Ahmadinejad, ambaye amechaguliwa kuwa rais wa Iran kwa mara nyingine tena.
Picha ya pili wanaonekana,wadau wa rais Mir Hossein Mousavi, wa cha upinzani, wakiandamana kuelekea kwanye uwanja wa ukumbozi kupinga matokea ya uchaguzi huo.
Majeshi ya NATO na Amerika yapata Generalali mpya.
Kabul, Afghanistan, 15/06/09. Jeneralali Stanley Mc Chrystal,ambaye aliteuliwa kuwa wa mkuu wa majeshi ya Amerika na NATO, nchini Afghanistan,katika kupambana na kundi la Taliban.
Jeneralali, Stanley MacChrystal, amechukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa majeshi hayo, Generalali, David McKiernan, ambaye aliachishwa kazi, baada ya kutokea makosa ya wakati wa uongozi wake.
Picha hapo juu, anaonekana, Generalali, Stanley McChrystal, akiongea na rais, Baraka Obama,mara baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa majeshi hayo.
Mashariki ya kati bado fumbo kwa jumuia ya kimataifa.
Jerusalem, Israel - 15/06/09. Waziri mkuu wa Israel, Menyamin Netanyahu,amesema ya kuwa kuwepo kwa taifa la Wapalestina,ni muhimu kwa usalama na amani wa eneo zima la mashariki ya kati.
Akisisitiza mkazo wa kuwepo kwa taifa la Wapalestina,waziri mkuu wa Israel, Benyamini Netanyahu, alisema ya kuwa hii yote itafanikiwa, ikiwa Wapelestina, wataitambua Israel ni taifa, ,swala la wakimbizi,kutofanya mashambulizi kwa Wanchi wa Israel, na kuzuia au kuwapokonya siraha wale wote wanao shiriki katika ugaidi.
Hata hivyo,serikali ya Palestina,imesema yakuwa hotuba ya waziri mkuu wa I srael, Benyamini Netanyahu, ni kikwazo kikubwa cha kuleta amani na usalama katika eneo zima la Mashariki ya Kati, hawaoni kama wana mshiriki katika swala la amani na usalama wa eneo hilo.
Picha ya hapo juu anaonekana, rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, ambaye uongozi wake umekuwa unapata ushirikiano wa karibu na serikali za Amerika na Ulaya katika swala la kuleta amani kati ya Waisrael na Wapalestina.
Picha ya pili, anaonekna waziri mkuu wa Israel , Benyamini Netanyahu, akihutubia jana taifa na jumui ya kimataifa kuhusu sera ya serikali yake katika maswala ya mambo ya nchi za nje.

No comments: