Monday, June 8, 2009

Rais wa Gabon hatupo nae tena.

Waandishi wahabari, 2 wa Amerika wahukumiwa kwenda jela miaaka 12 kila mtu.

Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 08/06/09. Hakama nchini Korae ya Kaskazini imewahukumu, waandishi wa habari raia wa Amerika miaka 12 jela , baada ya kuwakuta na hatia ya kosa la kuingia katika maeno ya Korea ya Kaskazini kinyume cha sheria. Waandisha hao wa habari, Laura Ling na Euna Lee, walikamatwa mnamo Machi 17/2007, ana askari wa ulinzi wa mipaka wa Korea ya Kaskazini.
Kufuatia hukumu hiyo, serikali ya Amerika ,imesema haikuridhishwa na kitendo hicho cha Korea ya Kaskazini, na itafanya kila jitihada kuhakikisha waandishi hao Laura na Euna,waachaliwe.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Korea ya Kaskazini,nchi ambayo imekuwa na mvutano mkubwa na Amerika kwa miaaka mingi tangu miaaka ya hamsini.
Picha ya pili wanaonekana, Laula Ling na Euna Lee, waandishi wa habari walio hukumiwa kifungo cha miaa 12 kila mtu na serikali ya Korea ya Kaskazini.
Rais wa Gabon hatupo naye tena.
Libreville, Gabao - 08/06/09.Serikali ya Gabon,imetangaza yakuwa rais wa Gabon Omar Bongo amefariki dunia nchi, Uispania Barcelona.
Kwa mujibu wa habari kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Gabon, zilisema ya kuwa, alifariki jumatatu ya leo saa nane machana katika Hospital ya Quiron.
Rasi, Omar Bongo aliyekuwa na miaka 73, alikuwa anajulikana kama rais wa maisha wa Gabon. ameitawala Gabon kwa muda wa miaaka 41, na kuwa kiongozi aliyetawala kwa muda mrefu katika bara la Afrika.
Picha hapo juu anaonekana rais , Omar Bongo , enzi za uhai wake, akiwa anatafakari kwa makini.
Picha ya pili anaonekana, rais, Omar Bongo, enzi za uhai wake,akikagua gwaride la heshima nchini Ufaransa, alipo tembelea nchin hiyo.
Picha ya tatu, anaonekana rais, Omar Bongo, akiwa na rais wa Ufaransa, Nikolas Sarkozy, wakati rais wa Ufaransa alipo tembelea nchini Gabaon.
Uchaguzi wa Lebanon, waleta hafuaheni.
Beirut, Lebanon - 8/06/09. Matokeo ya uchaguzi uliofanyika nchini Lebanon,yamekipa ushindi mkubwa chama kinacho ongozwa na mtoto aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon, hayati Rafiki Hariri, Saad Hariri kwa kupata viti 71 kati ya viti 128 katika bunge la Lebanon.
Kushinda kwa chama hicho 14 March,kinampa uwezo, Saad Hariri na chama chake kuongoza Lebanon na.
Hata hivyo chama kilichokuwa kinaupinzani mkubwa na 14 March, cha Hezbollah, kimepata viti 57, katika bunge hilo, jambo ambalo litaleta wakati mgumu kwa chama cha 14 March kupitisha baadhi ya maamuzi katika bunge hilo.
Ushindi huo wa chama cha 14 March, umepokelewa na nchi za Ulaya na Amerika kwa unafuu mkubwa, kwani uhusiano wa nchi hizo na Hezbollah siyo mzuri.
Picha hapo juu ,ni picha ya bendera ya ya Lebanon, nchi ambayo imekuwa katika hali ya mashaka kwa muda, hasa kwa baadhi ya viongozi wa siasa kuuwawa.
Picha ya pili anaonekana mmoja ya wananchi wa Lebanon, akijipongeza mara baada ya kujua ya kuwa chama chake kipata kura bungeni.

No comments: