Mbrazili nyota asajiliwa kwa kitita kinene.
Madrid, Uispania - 09/06/09.Timu ya Real Madrid,imemsajili mchezaji nyota wa Brazil, Kaka, kwa kitita cha $ 94.05million na kuvunja rekodi ya dunia.
Kaka, ambaye alikuwa mchezaji wa, AC Milan, amevunja rekodi ya iliyo wekwa na, Zinedin Zidane, aliposajiliwa na mwaka 2001.
Hata kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya soka, wanasema bado Zinedine Zidane, anaweka rekodi ya kuwa mchezaji aliye nunuliwa kwa Euro 73million na Kaka Euoro 63, kwa kuzingatia mzunguko wa mabadiliko ya pesa ( Fedha).
Picha hapo juu anaonekana, Kaka , akiongea na waandishi wa habari, muda baada ya kumaliza kufanya uangalizi wa afya mapema jana.
Jose Emanuel Barroso,achaguliwa tena kuwa rais wa Muungano wa Ulaya.
Brussel, Belgium - 09/06/09.Muungano wa Ulaya,umemchagua tena, Jose Emanuel Barroso, kwa mara nyingine kuwa rais wa muungano huo kwa kipindi kingine cha miaaka mitano.
Niger Delta, Nigeria - 09/06/09.Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Nigeria, wataendelea kusukuma na kusisitiza kutaka kupata haki na ukweli kuhusu kifo cha aliyekuwa kiongozi wa kuteteta mazingira, Ken Saro Wiwa, aliye uwawa mwaka 10/11/1995, licha ya kampuni ya Shell kukubali kulipa malipo ya dola za Kimarekani 15.5 million kwa familia zilizopinga kuwepo kwa Shell katika jimbo la, Niger Delta, kwa madai ya kuchafua mazingira.
No comments:
Post a Comment