Monday, June 29, 2009

Kamati ya uchaguzi Iran, rais,Mahmoud Ahmadinejad,badao ni mshindi.

Chaji za simu kuwa za aina moja kiviwango. Brussels, Ubeligiji - 29/06/09. Kampuni zilazo shughulikia, utengenezaji wa simu, zimekubaliana kwa pamoja kuanza kutengeneza chaji za aina moja, kwa ajili ya matumizi ya simu zote. Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya ofisi inayaoshughulikia, maswala ya mawasialiano katika nchi za jumuia ya Ulaya, zimesema ya kuwa kampuni za Nokia ,Motorola, Sumsung, Sony Ericsson., Apple,na LG, ambazo zina tengeneza simu na kutukiwa na wakazi wa Ulaya, zimekubaliana na kamati ya mawasiliano kwa kukubaliana kutengeneza chaji zitakazo tumika kwa kiwango kimoja. Kwa mujibu, wa habari hizi , kuanza kutumika kwa chaji hizi mpya, kuaanza mapema mwakani. Picha hpo juu, zimnaonekana, aina tofauti za chaji , ambazo hutumika kwa simu tofauti,na huwa zinaleta matatizo kwa watumiaji wa simu katika nchi Ulaya. Millionea ahukumiwa kwenda jera miaka 13 nchini Urussi. Moscow, Urussi, -29/06/09. Mahakama mjini Moscow, imemuhukumu, milionea Boris Berezovsky kwenda jela miaka 13, baada ya kukutwa na hatia ya kulaghai kwa kujipatia kiasi cha $million kutoka kwa kampuni ya Avtovaz. Boris Berezovsky,alihukumiwa, wakati yeyemwenyewe hakuwepo mahakamani. Mtuhumiwa huyo, Boris Berezovsky, anaishi ukimbizini nchi Uingereza. Picha hapo juu, anaonekana, Boris Berezovsky,akiingia ndani ya gari, ambapo kuonekana kwake huwa nadra saana.

Kamati ya uchaguzi Iran,rais, Mahmoud Ahmadinejad bado ni mshindi.
Tehran, Iran - 29/06/09. Kamati inayosimamia uchaguzi nchini Iran, imetoa matokeo ya kura zilizo hesabiwa upya na kusema ya kuwa rais, Mahmoud Ahmadinejad, mchaguliwa, ameshinda kwa kura nyingi na kusisitiza ya kuwa hata kura ambazo zimehesabiwa hivi sasa bado zina mpa kura nyingi rais.
Kura hizo za asilimia kumi,ambazo ndizo zilizodaiwa kuwa hazikuhesibiwa na kuleta utata.
Hata hivyo, wapinza ambao walikuwa wanagombea kiti hicho cha urais, waligomea uchaguzi kwa kudai ya kuwa kulikuwa na matatizo ya kura katika mahesabu yake.
Picha hapo juu, anaonekna rais, wa Iran, Mohmoud Ahmadinejed, akiongea katika moja ya mikutana , mara baada ya kutangazwa matokeao ya uchaguzi na kumpa ushindi mkubwa.
Picha ya pili wanaonekana, baadhi ya watu wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi, kwa madai ya kuwa kura zao hazikuhesibiwa.
Rais aomba ukimbizi,baada ya mapinduzi.
Honduras,Tegucigalpa - 29/06/09.Rais mpya aliyeapishwa nchini Honduras, Roberto Micheletti, kuchukua nafasi ya rais, Manuel Zelaya, ambaye yupo ukimbizini Kosta Rica.
Kufuatiwa kupinduliwa kwa rais, Emanuel Zelaya, baada ya rais huyo, kukataa kumrudisha kazini amir jeshi mkuu, ambaye alimfukuza kazi.
Kupinduliwa kwa, rais wa Honduras, Emanuel Zelaya, kumelaniwa na umoja wa mataifa.
Picha hapo juu, anaonekana, rais Emanuel Zeyala, ambaye yupo ukimbizini Kosta Rica.
Picha ya pili, anonekana, rais mpya wa Homduras, Micheletti, akiapishwa kuwa rais wa Honduras.
Picha ya tatu,kinaonekana , kifaru cha jeshi kikiwa mbele ya ikulu,kulinda serikali mpya ya rais, Robert Michelitti.
Aliyetikisa wawekezaji kutumikia kifungo miaka 150.
New York, Amerika - 29/06/09. Mahakama ya jijini, New York , imemuhukumu miaka 150 kwenda jela,Bernard Madoff,aliyekuwa mwenyekitia wa Nasdaq soko la wawekezaji na wabadishaji lililopo jijini New York.
Hukumu hiyo, ilitolewa na jaji Danny Chin, baada ya Bernadr Madoff, kukili kosa lake, la kuwatapeli mamia ya wawekezaji, wakiwepo watu mashuhuri kutoka ,Hollywood, wastaafu,na wafanya biashara wengine.
Kutolewa kwa hukumu hiyo, kunaaminika kutajaribu kupunguza jazba au machungu waliokuwa nayo wale wote waliotapeliwa na Bernard Madoff.
Pichani hapo juu, anaonekna Bernard Madoff, akielekea mahakamani ,huku paparazzi wakiwa kazini kupata picha za kumbukumbu.

No comments: