Tuesday, June 16, 2009

Rais wa zamani wa Amerika atembelea Gaza.

Wananchi wa Niger, kupiga kura ya maoni ya hatma ya urais. Niamey, Niger 16/06/09. Maelfu ya wanchi Niger, wameandamana kudai ya kuwa rais,Mamadou Tandja, aliyepo madarakani,asibadilishe katiba, ili aweze kugombea tena kiti cha uchaguzi kwa mara ya tatu. Maandamano hayo, nayamefanywa kufatia kupangwa tarehe ya kupiga kura ya maoni 4/Agusti,ikiwa kama rais Mamadou Tandaja ataweza endelea kugombea kiti cha uraisi. Rasi, Mamadou Tandja, anatarajiwa kumaliza muda wake wakuongoza nchi hivi karibuni. Picha hapo juu, anaonekana, rais Mamadou Tandja, akiwa katika moja ya mikutano ya kimataifa.

Makamu wa rais wa Kongo DRC, afunguliwa mashitaka.
Hague, Holland - 16/06/09. Mahakama inayo shughulikia kesi za kimataifa za jinai na maafa yanayo sabaishwa na vita, imemfungulia kesi makamu wa rais wa Kongo (DRC), Jean - Pierre Bemba, ya kuhusika na vita nchini Kongo na kusababisha kuvunjwa kwa haki za binadamu wakati wa vita vilivyo tokea kati ya mwishoni mwa mwaka 2002 hadai mwanzoni mwa mwaka 2003
Kwa mujibu wa mwanasheria wa mahakama alidai ya kuwa Jean Piere Bemba, alikuwa ana fahamu yote yaliyo tokea.
Hata hivyo mwanasheria anayemtete bwana, Bemba , amesema yakuwa, mteja wake hakuhusika na wala alikuwa hajui nini kilichokuwa kinaendelea, hii ni yote ninakuja kutokana na mrindimo wa siasa.
Rais wa zamani wa Amerika,atembelea Gaza.
Gaza,Ukingo wa mto Magharibi - 16/06/09.Rais wa zamani wa Amerika, Jimmy Carter,ametembela maeneo yaliyo shambuliwa na Israel mwishoni mwa 2008 na mapema mwaka huu 2009, na kusema yakuwa imestua saana.
Bwana, Carter, alisema ya kuwa mstuko huo, unaonyesha ni jinsi gani, Wapalestina wanavyo fanywa kama siwatu, na kuagiza ya kuwa kuna haja ya Wapalestina kupata haki kama watu wengine.
Picha hapo juu, wanaonekana, rais wa zamani wa Amerika, Jimmy Carter,na kiongozi wa Hamas,Ismail Haniyeh,kulia wakitembea kuelekea ofisini, kabla ya kuongea na waandishi wa habari.
Picha ya pili, wanaonekana, rais wazamani wa Amerika, Jimmy Carter kushoto na kulia kiongozi wa Hamas, Ismail Haniayeh, wakiongea na waandishi wa habari.
Kamati yaamua kura kuhesabiwa upya.
Tehran, Iran - 16/06/09.Kamati iliyo simamia uchaguzi wa urais wa Iran,imetangaza yakuwa watatizama kiundani na kuanza kuziehesabu kura upya.
Hata hivyo, Mir Hussein Mousavi, ambaye ameshindwa katika uchaguzi huu, ametaka kura zipigwe upya, swala ambalo kamati iliyo simamia uchaguzi imelikataa.
Mvutano huo wa matokeo ya kura,yameleta wasiwasi wa kisiasa nchini Iran, jambo ambalo linaufanya uongozi wa Iran, chini ya Ayatollah Ali Khamenei kuwa na wakati mgumu.
Picha hapo juu, ni picha ya rais,Mahamoud Ahamdinejad katikati, akiwasiri nyumbani,baada ya kukatiza ziara yake ya kikazi nchini Urussi.
Picha ya pili, anaonekana, Ayatollah Ali Khamenei, ambaye uongozi mkuu wa Iran,ambaye Iran inategemea uwezo wake.

No comments: