Tuesday, June 23, 2009

Urussi yatamka kushirikiana kuhusu swala la mashariki ya Katu

Wapigania uhuru kuishitaki Uingereza.

London,Uingereza - 23/06/09.Wapigania uhuru watano wa Kenya ambao walikuwa kundi la Maumau, wamefungua kesi ya mashitaka zidi ya serikali ya Uingereza kwa kuvunja haki za binadamu wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza ulipo kuwa ukitawala miaka ya 60 kurudi nyuma.
Wapigania uhuru hao ambao wanamiaka kati ta 70 na 80. wanadai ya kuwa serikali ya Uingereza inatakiwa kulipa fidia na kuomba msamahaa kwa matendo yaliyo fanywa na Uingereza wakati Inaitawala Kenya.
Msemaji wa wapigania uhuru hao, Gitu wa Kahengeri, alisema wanafanya hivyo kwa ajili ya wapigania uhuru wenzao, wa kundi la Mau mau ambao walipoteza maisha kwa ajili mya kutetea uhuru.
Hata hivyo serikali ya Uingereza, imedai ya hali halisi ilipewa serikali ya Kenya baada ya kupata uhuru.
Picha hapo juu, ni ya bendera ya Kenya, nchi ambayo ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza hadi ilipo pata uhuru 1963.
Picha pili, wanaonekana, baadhi ya wapigania uhuru wa mau mau wakiwa chini ya ulinzi, ambao wengi wao walipoteza maisha wakati wa kutetea uhuru wa nchi yao
Urussi yatamka kushirikiana na Misri kuhusu swala la Mashariki ya Kati.
Kairo, Misri-23/06/09.Rasi wa Urussi, Dmitri Medvedev, yupo nchini Misri kwa ziara ya kiserikali. Katika ziara hiyo, rais,Medvedev, amekutana na rais wa Misri, Hosni Mubaraka, kuzungumzia swala zima la mashariki ya kati. Picha hapo juu, wanaonekana marais wa Urussi na Misri wakiwa katika mazungumzo, wakati rais,Dmitri Medvedevwa Urussi alipo kutana na rais, Hosni Mubaraka wa Misri. Israel ya mwachia kiongozi wa Hamas.
Jerusalem,Israel- 23/06/09.Serikali ya Israel imemwachia huru spika bunge wa Hamas bwana, Abdul Aziz Dweik, baada ya kukaa miaka mitatu jela kwa kuso la kujihusisha na kundi hilo ambalo linamshikilia, Gilat Shalit.
Pichani hapo juu, anaoneka bwana, Abdul Aziz Dweik, akitolewa pingu na polisi kabla ya kuwa huru.
Picha pili anaonekana,Abdul Aziz Dweik, akitabasamu kabla ya kutoka kizimbani kuelekea nyumbani.

2 comments:

Anonymous said...

I want not approve on it. I regard as precise post. Especially the title-deed attracted me to study the sound story.

Anonymous said...

Nice brief and this enter helped me alot in my college assignement. Gratefulness you on your information.