Friday, June 26, 2009

Mfalme wa Muziki wa Pop atutoka,MUNGU BABA TUNAKUOMBA UILAZE ROHO YA MICHAEL JACKSON PEPON.AMINA.

Mfalme wa Muziki wa Pop atutoka,MUNGU BABA TUNAKUOMBA UILAZE ROHO YA MICHAEL JACKSON PEPON.AMINA.

Picha ya familia ya Mzee Joseph Jaskson, akiwa na watoto wake, Jackon Five, wa kwanza kushoto ni Michael Jackson, ambaye alikuwa ndiye nyota katika kundi zima la musiki wa Jackson 5.

Michael Jackson, alikuwa na umri wa miaka 50.

Los Angeles, Amerika - 26/06/09.Wapenzi wa Muziki Duniani twapigwa na wingu zito.
Picha zilizopo hapo juu, zineleza ni jinsi gani, marehemu Michael Jackson,alivyo pendwa kutokana ma kubarikiwa kipaji na Mungu.
Mzee Joseph Jackson, baba, ya Michael Jackson, alikuwa anampenda mwanae Michael ,kwa hali na mali, hapo anaonekana kwenye picha ya tano, akiwa ameshikilia moja ya CD(Album) ambayo ina picha ya Michael Jackson na ndani ya CD hiyo kuna nyimbo za Michael jackson.
Hamas yasema taifa la Israel hapana.
Damascus, Syria 26/06/09.Kiongozi wa Hamas,Khaled Mashaal, amesema Hamas, haitalitambua taifa la Israel.
Kiongozi huyo wa Hamas, Khaled Mashaal, aliyasema haya, siku ya Alkhamisi, mbele ya wanachama na wadau katika mkutano wa Hamas nchini Syria, ambapo kunawanachama na wadau wengi wa Hamas.
Hata hivyo, kiongozi huyo alikubaliana na mpango wa kuwa na mataifa mawili, ikiwa kutazingzatiwa makubaliano ya mwaka 1967 na Jerusalem mji mkuu.
Picha hpo juu, anaonekana, kiongozi wa Hamas, Khaled Mashaal, akihutubia mamia wanachama wa Hamas siku ya Alkhamis.
Serikali ya Somali kupata msaada kutoka Amerika.
Washington, Amerika - 26/06/09.Serikali ya Somalia ina karibia kupata msaada wa kijeshi kutoka serikali ya Amerika, ili kukabiliana na makundi yanayo pingana na serikali.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana,kutoka serikali ya Amerika,zina sema ya kuwa ipo haja ya kuisaidia serikali ya Somali, inyo ongozwa na Shariff Shabab.
Ili kukabiliana na hali ya hatari iliyopo nchi Somali, hasa Mogadishu, serikali ya Somalia, imetangaza hali ya hatari siku ya jumatatu katika jiji hilo.
Picha hpo juu, anaonekana, mmoja wa wapiganaji wa kundi la Al Shabab, akishambulia moja ya mitaa mjini Mogadishu.
Uturuki ipo karibu kuanza mazungumzo na muungano wa Ulaya.
Brussels, Ubeligiji - 26/06/09. Waziri mkuu wa Uturuki,Recep Tayyip Erdogan, amesema ya kuwa nchi yake, inampango wa kuanza upya mazungunzo ya kujiunga na muungano wa Ulaya.
Waziri, Recep Tayyip Erdogan, aliyasema haya, wakati alipo kuwa nchini Ubelingiji kwa mazungumzo na viongozi wa jumuia ya muungano wa nchi za Ulaya.
Hata hivyo, Uturuki imekuwa na wakati mgumu kujiunga na jumuia ya nchi za Ulaya kwa kuto kukubali kuitambua Syipras(Cyprus) na katiba yake, nakushinda kushirikiana kikamilifu na Ugiliki katika swala zima la Cyprus.
Picha hapo juu, wanaonekana, waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, akisalimiana na Olli Rehn, mkuu anaye shughulika kujiunga na Muungano wa nchi za ulaya, walipo kutana Brussels siku ya Ijumaa.
Waandamanaji na viongozi wao wawekwa karibu na kiti moto nchini Iran.
Tehran, Iran - 26/06/09.Mmoja wa viongozi wa kidini nchini Iran,Ahmad Khatami, amesema ya kuwa wale watu wote ambao wanaandamana kupinga matokeo ya uchaguzi ya juni 22, ni lazima waadhibiwe vikali.
Ayatollah, Ahmad Khatami, ambaye ni mbuge katika kamati ya wabunge teule, ameagiza kwa kusema ya kuwa viongozi waliosababisha au kusimamia maandamano lazima waadhibiwe ili wawe mfano kwa wengine.
Ayatollah, Ahmad Khatami, aliyasema hayo wakti wa swala ya Ijumaa,na kutangazwa na radio moja kwa moja.
Picha hapo juu, anaonekana, Ayatollah, Ahmad Khatami, akiwahutubia maelfu waliokusanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Tehren siku ya Ijumaa baada ya swalat Ijumaah.
Picha ya pili wanaonekana , watu walioudhulia swalat Ijuma, wakishangilia na kukubaliana na Ayatollah, Ahmad Khatami kwa yale anayo yaongea.

No comments: