Sunday, June 7, 2009

Kuba ilikuwa na makachero wake nchini Amerika.

Washington, Amerika - 05/06/09.Wastaafu wawili bibi na bwana,Myres wanashitakiwa na serikali ya Amerika kwa kosa la kufanya ukachero kwa niaanba ya serikali ya Kuba , wakati walipo kuwa wafanyakazi wa serikali ya Amerika.
Kwa mujibu wa idara ya mahakama, ina yo shughulikia kesi hiyo,zinasema, bibi Myres 71 na bwana Myres 72, walianza kazi hiyo mnamo wa mwaka ya 1979, walisha pewa tunzo na serikali ya Kuba mwaka 1995.
Bwana Myres na mke wake walikuwa wakisafiri na kukutana na makachero wa Kuba nchini Mexico, kila wakati.
Picha hapo juu,anaonekana rais wa zamani wa Kuba, Fidel Castro, ambaye wakati wa utawala wake uhusiana wa Kuba na Amerika, ulikuwa wa mashaka makubwa.
Picha ya pili,ni ya bendera ya Amerika, nchi ambayo kwa muda mrefu imekuwa haina uhuusiana mzuri na Kuba.

No comments: