Wednesday, June 10, 2009

Sudan kuzalisha mafuta kutoka kwenye mimea.

Sudan kuzalisha mafuta kutoka kwenya mimea. Khartoum, Sudan - 10/06/09. Serikali ya Sudan imezindua rasm mmea utakao tumika katika kutengenezea mafuta ya kuendeshea mitambo. Akizindua mmea huo, rais wa Sudana, Omar Al Bashir, alisema ya kuwa serikali yake itafanya kilanjia mradi huo udumu kwa utaipatia Sudan, pesa za kigeni na kuta ajira. Kwa mujibu wa uongozi wa kampuni hiyo ya Kenana, imesema ya kuwa mtambo huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha mafuta lita 200 million , yatakayo toka kwenye mimea hiyo baada ya miaka miwili. Picha ya hapo juu, ni ya bendera ya serikali ya Sudan, nchi ambayo imegundua mimea itakayo toa zao halisi la mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo. Hali halisi ya maisha kuisaida Taliban kukua. Ismabad, Pakistan - 10/06/09. Wachunguzi wa mambo ya kiusalma nchini Pakistan, wanasema ya kuwa kundi la Taliban, linazidi kukua kila mwaka. Hii inakuja kutokana na hali halisi ya eneo hili,kiimani,mila na desturi na hasa swala usalama wa wanchi waliowengi nchini Pakistan na hivyo wanchi wengi kujikuta kuingia katika kundi la Taliban kwa nguvu au kwa hiyari yao. Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu, ambao wamesimama khuku wakiota jua,katika kambi moja ya wakimbizi, baada ya kukimbia vita vinavyoendelea kati ya Taliban na majeshi ya serikali.

No comments: