Thursday, October 7, 2010

Askofu Dasmond Tutu astaafu kazi za kiofisi.

Askofu Desmond Tutu astaafu kazi zote za kiofisi.

Cape Town, Afrika ya Kusini - 07/10/2010. Askofu, kiongozi, mtetezi, mpigania haki za binandamu na mmoja wa vionngozi walio pinga ubaguzi wa rangi nicni Afrika ya Kusini wakati wa serikali ya kibaguzi ya makaburu wa Afrika ya Kusini ametangaza kujiudhulu kazi zote za kiofisi.
Askofu Desmond Tutu aliyasema hayo wakati akiazimisha siku ya kuzaliwa kwake leo ambapo anatimiza miaka 79.
Askofu Desmond Tutu alisema "Kuanzia sasa nitakuwa karibu na mke wangu, familia yangu kwa muda wote na kupumzika huku nikiangalia michezo, na wakati huo nikitoa husia kwa wanangun wajukuu na vijukuu."
Picha hapo juu anaonekana, Askofu Desmond Tutu akiwa anaongoza maombi kabla ya kufikiwa wakati wa kustaafu kazi zake zote za kiofisi.

No comments: