Friday, October 1, 2010

Rwanda na Uganda zakanusha madai ya repoti ya Umoja wa Mataifa.

Denzel Washington kutangaza siku yamshindi wa Nobel nchini Oslo. Oslo, Norway - 01/10/2010. Mcheza simema maarufu duniani atakuwa mtangazaji wakati wa kutoa zawadi ya Nobel Price itakayo fanyika mwaka huo Oslo. Denzel Washington ambaye amekuwa maarufu kwa kucheza sinema zenya kusisimua hisia katika jamii alisema "niheshima iliyoje kuwa mmoja wapo ya watu watakao kuwepo na kushiriki kwenye sherehe hiyo." Picha hapo juu anaonekana Denzel Washington akiwa ameshikilia zawadi aliyo shinda kuwa mshindi bora katika kucheza sinema nzuri na kusisimua. Rwanda na Uganda zakanusha madai ya repoti ya Umoja wa Mataifa.

Kigali, Rwanda - 01/10/2010. Serikali ya Rwanda na serikali ya Uganda zimepinga vikali repoti iliyo tolewa na Umoja wa Mataifa kwa kuzihusisha nchi hizo mbili katika vita na mauaji yaliyo tokea katika Demokrasi Jamuhuri ya Kongo.
Kwa mujibu wa reporti hiyo yenye kurasa 617 ilisema "majeshi ya Rwanda na Uganda yaliwauwa raia wengi wakati wa vita na hasa katika kipindi cha miaka ya 90 hadi mwisho wa miaka hiyo." Katika repoti hiyo pia nchi nyingine ambazo zilitajwa ni Burundi, Kongo na Zimbabwe.
Akiongea wakati wa kutangaza repoti hiyo kamishana wa kutetea haki za binadamu Navi Pillay alisema "katika kila jamii ya wananchi wa DR Kongo basi yupo mtu mmoja ambaye ameathirika kutokana na vita hivyo."
Picha hapo juu zinaonekana picha za bendera za Rwanda juu na ya chini ni ya Uganda nchi ambazo zinashutumiwa katika repori ya umoja wa Mataifa.
Rais wa zamani wa Pakistani aanzisha chama kipya cha siasa.
London, Uingereza - 01/10/2010. Rais wa zamani wa Pakistan na aliyekuwa amiri jeshi mkuu ameanzisha chama cha siasa.
Pervez Musharraf, alitangaza mbele ya wandishi wa habari alisema "chama hicho kitajulikana kama All Pakistan Muslim League na kitashirki katika uchaguzi ujao utakao fanyika mwaka 2013."
Aliongeza kwa kusema "ninaogopa kwani Pakistan uenda ikagawanyika kama hakutakuwa na mabadiliko ya uongozi."
Vilevile alitumia fursa hii kuomba msamaha kwa makosa yaliyo tokea wakati wa uongozi wake.
Picha hapo juu anaonekana aliyekuwa rais wa zamani wa Pakistani, Pervez Musharraf akiwasalimia wanachi waliokuja kusikiliza kuzinduliwa kwa chama kitakacho ongozwa naye.
Sherehe ya miaka 50 ya uhuru yaingia dosari nchini Nigeria.
Abuja, Nigeria - 01/10/2010. Watu wapatao wanane wamepoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa baada ya gali kulipuka katikati ya jiji la Abuja.
Mlipuko huo uliokea wakati wanachi wanajipanga kuanza kushangilia miaka 50 ya uhuru wa Nigeria.
Mlipuko huo ulitokea mbele ya viongozi wa nchi ambalo walikuja kusherehekea sikuku hiyo.
Picha hapo juu yanaonekana baadhi ya magari ambayo yamearibiwa kutokana na mlipuko na kupoteza maisha na kusababisha majeruhi.

No comments: