Thursday, October 14, 2010

Kazi ya uokoaji yamalizika salama nchini Chile

Kazi ya uokoaji yamalizika salama nchini Chile.

Atacama, Chile 14/10/2010. Waokoaji wamefanikisha kazi ya kuwaokoa wafanyakzi 33 waliokuwa wamekwama kutoka katika migodi iliyopo kwenye jangwa la Atacama baada ya kukwama ndani ya machimbo ya migodi kwa zaidi ya miezi miwili .
Akiongea mara ya kumalizika uokoaji rais wa Chile Sebastian Pinera, alisema "kwama ra nyingine tena tumekuwa tumezaliwa upya na sisi Wachile tumeuonyesha ulimwengu ya kuwa tuko pamoja katika kila hali."
Akiongea mmoja wa waokolewa Luis Urzua alisema " tulikuwa na imani na tulikuwa tunapigania kwa ajili ya familia zetu na tumefanikiwa kutoka tukiwa hai kutokana na ushirikiano tuliokuwa nao kwa wakti wote tulipo kuwa chini ya ardhi."
Pia shughuli za uokoaji zilishuhudiwa na rais wa Bolivia Evo Morares ambaye alikuja kumuunga mkono rais mwenzake wa Chile na kumpokea mmoja wa watu waliokuwa wamekwama chini ya ardhi alikuwa ni raia wa Bolivia.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Bolivia Evo Morares akiongea huku akimtizama rais wa Chile Sebastian Pinera wakati alipo kwenda kumuunga mkono shughuli za uokoaji zilipo anza.
Picha ya pili anaonekana rais wa Chile Sebastian Pinera, akitangaza rasmi kuanza shughuli za uokoaji huku akitazamwa na wananchi ambao walikuwa wanangoja kwa hamu kuwaona ngugu zao wakiwa hai.
Picha ya tatu anaonekana rais wa Chile akikumbatiana na Florencio Avalos ambaye alikuwa wa kwanza kuokolewa kutoka kwenya migodi iliyo bomoka na kuwazuia wasiweze kutoka yeye pamoja na wenzake.
Picha ya nne, anaonekana Carlos Mamani Soliz akiwa amepiga magoti kushukuru Mungu, mara baada ya kukombolewa kutoka ndani ya machimbo ya migodi ambayo ilibomoka wakati walipokuwa kazini.
Rais wa Iran afanya ziara ya kiserikali nchini Lebanon.
Beiruti, Lebanon-14/10/2010. Rais wa Iran amewahutubia maelfu ya Walebanoni kwa nyakati tofauti tangu kuanza kwa ziara yake ya kiseikali nchini humo. Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad katika hotuba zake aliwasifu wananchi wa Lebanon kwa kusema "ujasiri wane wa kutokukubali kuonewa na ndiyo imekuwa changamoto katika eneo zima la Mashariki ya Kati."
Pia rais huyo aliongezea kwa kusema "Iran itasimama bega kwa bega na Lebanon ikiwa kutatokea matatizo yaina yoyote."
Hata hivyo serikali ya Amerika na Izrael zimekiaani kitendo cha rais wa Iran kufanya ziara nchini Lebanon kwa kusema "sijambo muafaka."
Mahmoud Ahamadinejad yupo nchini Lebanon katika kuendeleza na kukuza ushirikiano wa Karibu na nchi hiyo ambapo nchi hizo mbili zilitiliana sahii mikataba ya ushirikiano kibiashara, kilimo na katika nyanja mafuta.
Picha ya kwanza ni ya rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad akiwa mbele ya bendera za Iran na Lebanon.
Picha ya pili wanaonekana watu waliokuja kumsikiliza rais wa Iran wakati alipo kuwa akihutubia katika moja ya mikutano wakati wa ziara yake nchini Lebanon.
Mamia waandamana kupinga kuteuliwa Kim Jong-Un
Seoul, Korea ya Kusini - 14/01/2010. Mamia ya watu wameandamana katika jiji la Seoul kupinga kitendo cha kiongozi wa serikali ya Korea ya Kaskazini kumteua mtoto wake kushika madaraka yake.
Katika maandamano hayo mmoja wa waandamanaji amabye mwanaye alitekwa mwaka 1971 alisema "dunia imeshangazwa na kitendo cha kiongozi wa Korea ya Kaskazini kupanga kumrisisha mwanae madaraka kinyume na demokrasi.
Picha hapo juu anaonekana mmoja ya watu waliokimbia kutoka Korea ya Kaskazini akiwa ameshikiria kitu mkononi kutopia picha iliyo chorwa ya Kim Jong-Un,ambaye inaaminika tachukua madaraka kutoka kwa babayake Kim Jong Il.
Viongozi wakutana kupata majibu ya chanzo cha kifo cha raia wa Uingereza.
London Uingereza - 14/10/2010. Waziri Mkuu wa Uingereza amekutana na Mkuu wa Majeshi wa Amerika anayesimamia vita vya Afghanistan ili kupata muafaka kuhusu kifo cha raia mmoja wa Uingereza.
Waziri Mkuu David Cameron alikutana na Kamanda David Petraeus katika ofisi ya waziri mkuu zilizopo jijini London.
Kifo cha Mwingereza Linda Norgrove 36 kilitokea wakati wa harakati za kutaka kumkomboa kutoka mikononi mwa wateka nyara waliomteke. Natokea kuuwawa kwa Mwingereza huyo kumekuwa na habari tofauti kuhusu kifo chake.
Picha hpo juu anaonekana marehemu bi Linda Norgrove ambaye alipoteza maisha wakati wa jitihada za kutaka kumwokoa.

No comments: