Saturday, October 30, 2010

Mizigo inayo sadikiwa kuwa na bomu yapatikana

Mizigo inayo sadikiwa kuwa na bomu yapatikana. Dubai, UAE - 30/10/2010. Makachero wa UAE na makachero wa kimataifa wa nchi za Uingereza na Amerika wamefanikiwa kuukamata mizigo ambao inasadikiwa ilikuwa ndani ya ndege tayari kuelekea Amerika. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "mizigo hiyo ilikuwa imetokea nchini Yamen. Mizigo hiyo likutwa na aina fulani ya unga PETN ambao unasadikiwa ungetumika kuleta madhara." Picha hao juu inaonekana moja ya ndege ya kubebea mzigo ikiwa inafanyiwa ukaguzi mara ya habari kupatikana ya kuwa kuna moja ya ndege za kubebea mizigo imebeba mzigo wenye bomu.

Makampuni ya ulinzi ya watu binafsi yaongezewa muda kukaa nchini Afghanistan.
Kabul,Afghanistan - 30/10/2010. Serikali ya Afghanistani imekubali kuongeza muda wa kuwepo kwa makampuni ya ulinzi ya kibinafsi.
Kwa mujibu wa habari za apo hawali makampuni yote wa kiulinzi yaliyopo nchini Afghanistani yalitakiwa kuondoka ifikapo mwisho wa Desemba 2010 lakini yameongezewa muda hadi kufikia mwezi Machi 2011.
Uamuzi wa kufuta mkataba na makampuni ya kiulinzi yaliyopo nchini Afghanistan ulitolewa serikali na kutangazwa rasmi na rais Karzai.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Afghanistan Hamid Karzai akiwa mazungukwa na walinzi ambao baadhi yao wameajiliwa na makampuini ya ulinzi ya watu binafsi.
Picha ya pili anaonekana mmoja wa walinzi wa makampuni ya ulinzi ya watu binafsi akikatiza katika shamba moja nchini Afghanistan wakati wa akiwa kazini.
Aliyekuwa rais wa Argentina azikwa kijijini kwao
Santa Cruz,Argentina - 30/10/2010. Aliyekuwa rais wa Argentina Nestor Kirchner azikwa nyumbani kwao alikozaliwa Rio Gallegos.
Rais huyo ambaye alikuwa mume wa rais wa sasa Bi Cristina Kirchner, alikuwa kiongozi aliye simamia na kufanya kazi bila kuchoka ili kuleta maendeleo ya Argentina.
Picha hapo juu anaonekana marehemu Nestor Kirchner ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 60.
Picha ya pili wanaonekana rais wa Argentina Bi Cristina Kirchner kushoto akiwa na marehemu mume wake Nestor Kirchner enzi za uhai wake.
Picha ya tatu wanaonekana baadhi ya Waargentina wakisindikiza gari lililo mbeba marehemu Nestor Kirchner kuelekea kijiji kwao kwa mazishi.

No comments: