Monday, October 11, 2010

Swala la amani kati ya Waizrael na Wapalestina laingia sura mpya.

Swala la amani kati ya Waizrael na Wapalestina la chukua sura mpya.

Jerusalem, Israel - 11/10/2010. Waziri mkuu wa Izrael amewataka viongozi wa Kipalestina kukubali na kutambua ya kuwa Izrael in taifa la Mayahudi.
Binyamin Netanyahu, aliyasema hayo wakati alipo kuwa aki hutubia bunge la Izrael Knesset
Waziri mkuu Netanyahu alisema "kulitambua taifa la Izrael ni nguzo muhimu katika swala zima la mazungumzo ya amani."
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Wapalestina alisema "Wapalestina hawakubaliani masharti hayo na wanataka ili mazungumzo yaendelee ni lazima serikali ya Izrael isimamishe ujenzi wa nyumba zake katika maeneo inayo yakali."
Picha hapo juu ni ya bendera ya Izrael ambao viongozi wa serikali wanataka Wapalestina walitambue Taifa la Waizrael.
Picha ya pili ni ya bendera ya Wapalestina, ambapo wanataka Izrael isimamishe ujenzi ili mazungumzo ya amani yaendelee.
Serikali ya Hungari kukataifisha kampuni iliyo husika na janga la sumu.
Budapest Hunguri - 11/10/2010. Polisi nchini Hungari wamemkamata na kuweka kizuizini mkuu wa kampuni ya kuzalisha vyuma kwa kosa la kupasuka kwa bwawa lenya maji yaliyo changanyika na sumu hivi karibuni.
Msemaji wa serikali Anna Nagy aliema " Zoltan Bakony ambaye ni mkuuwa kampuni hiyo alikamatwa hivi karibuni."
Akiongea mbele za waandishi wa habari ,waziri mkuuwa Hungari Viktor Orban alisema "kampuni hiyo inatakiwa kuwa chini ya serikali kwa kutokana na matatizo yaliyo tokea ya kuaribu mazingira na makazi wa wana vijiji."
Kufuatia mafuriko hayo watu wapatao saba walipoteza maisha yao na wengi zaidi ya 150 kujeruhiwa vibaya.
Bwawa hilo lililo pasuka lipo km 160 magharibi mwa mji wa Budapest lilifianya mji mzima kuwa na rangi nyekundu sumu ambayo huenda ikaleta madhara makubwa kiafya katika jamii.
Mgogoro wa China na Japan mawaziri wakutana.
Hanoi, Vietnam - 11/01/2010. Mawaziri wa ulinzi wa serikali za China na Japan wamekutana kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mzozo baada ya serikali ya Japan kumkamata rais wa China Zhan Qixiong.
Mzozo huo ulizidi kuwa mkubwa mara baada ya serikali ya Japan kukataa kumwanchia huru raia huyo wa China ambaye alikuwa kiongozi wakati meli ya uvuvi ya China inlipo gongana na boti ya ulinzi ya Kijapan.
Msemaji wa serikali ya China Liang Guanglie alisema " mazungumzo ya maafisa hao wawili wa serikali zote yaliendelea viziri na kuna matumaini ya kuwa mgogoro huu utakwisha hivi karibuni."
Picha hapo juu hapo juu inaonekana meli ya uvuvi ya Kichina ambayo ilikuwa chanzo cha mgogoro kati ya China na Japan.

No comments: