Sunday, October 24, 2010

China huenda ikatumia kura yake ya veto.

China huenda ikatumia kura yake ya veto.

New York Amerika - 24/10/2010. Umoja wa Matifa umesema huenda China ikaweka kizuizi kufuatia repoti inayo sema ya kuwa risasi zilizo tumika kuwashambulia wanajeshi wa Umoja wa Mataifa ni za Kichina. Habari hizi zilipatikana wakati kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa inakutana kujadili vikwazo zidi ya serikali ya Sudan. Akiongea mwakilishi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Zhao Baogang alisema " hii repoti haina ukweli na hawaitambui na nilazima uchunguzi ufanyike kwa makini." Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa ambao wamekuwa wakishambuliwa mara kadhaa wakati kufanya doria. Umoja wa Mataifa wasimamisha zawadi kwa rais wa Ekuetioa Guinea.
New York, Amerika - 24/10/2010. Umoja wa Matifa umesimamisha zawadi yenye thamani ya $ 300,000 iliyo tarajiwa kutolewa kwa jina rais wa Ekuetoria Gunea, Obiang Nguema Mbasogo.
Kwa mujibu wa habari kutoka idara ya Umoja wa Matifa - UNESCO zinasema "uamuzi wa kusimamisha zawadi hiyo kunatokana na maombi amyayo yameletwa kupinga kuwepo kwa zawadi hiyo kutokana na rais Obiang na serikili yake walivyo itawalawa nchi na kuweka katika hali ya kimaskini." Picha hapo juu anaonekana rais wa Ekuetoria Guinea Obiang Nguema Mbasogo akiwa katika moja ya mikutano ya kimataifa.
Wikileaks yatoa nyaraka za siri kuhusu vita vya Irak.
London, Uingereza, 24/10/2010. Shirika moja la habari WikLeaks limetoa hadharani nyaraka za siri ambazo zinaelezea kiundani hali na matokeo ambayo yalitokea na hali halisi ilivyo nchini Irak tangu kunza kwa vita hadi hivi sasa.
Nyaraka hizo za siri zinaeleza "mauaji mengi ya raia yalitokea kinyume na habari zilizotolewa na serikali ya Iraq na washiriki wake."
Pia katika repoti hizo zinaeleza " baadhi ya wanawake wajawazito waliuwawa wakati walipokuwa wakikimbiziwa hosptali na ikiwa kulitokea mauaji ya liyo vunja sheria za vita wafiwa walipewa fidia ya kiasi cha $10,000."
Picha hapo juu inaonesha sehemu ambayo mauaji yalitokea kwa wingi.

No comments: