Mashindano ya Jumuia ya Madola ya funguliwa.
New Dheli, India - 03/10/2010. Wananchi wa India wamewakaribisha wanamichezo mbalimbali ili kushiriki mashindano ya nchi wanachama wa jumuia ya nchi zilizo kuwa koloni la Uingereza ambayo yanajulikana kama mashindano ya nchi za jumuia ya madola.
Mashindano hayo ya 19th yameanza rasmi baada ya habari za wasiwasi kuenea ya kuwa itakuwa vigumu kwa mashindano hayo kufanyika kutoakana na maandalizi yaliyo tiliwa mashaka.
Picha hapo juu wanaoneka wanamichezo wakishiriki wakati wa ufunguzi huku wakiongozwa na maonyesho yalioandaliwa kwa ajili ya ufunguzi.
Wajerumani kushangilia kumbukumbu ya muungano.

Muungano huo ulipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Ujerumani na Ulaya kwa ujumla na umekuwa ukikumbukwa na kusherekewa kila mwaka.
Picha hapo juu anaonekana Kanselar wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wengine wakiangali kwa pamoja mazingira mapya baada ya muungano huo kutokea miaka 20 iliyo pita
Athens, Greece - 03/10/2010. Serikali ya China imesema itaisaidia kikamilifu serikali ya Greek katika kujenga uchumi wake uliyo yumba.
China kuisaidia Greek kuinua Uchumi wake.


Waziri mkuu wa China Wen Jiabao alisema " China itashiriki kikamilifu katika kuisaidia Greek kujijenga upya kiuchumi ili kupunguza deni ambalo ni mzigo kwa serikali kwa kuongeza ushirikiano wa karibu na kukuza biashara kati ya nchi hizi mbil."
Picha hapo juu ni ya bendera za China nchi ambayo itashirikiana kikamilifu na serikali ya Greek ili kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Na picha inayo fuata chini ni ya Greek nchi ambayo inakabiliwa na tatizo la kiuchumi na kwa sasa itashirikiana na China kikamilifu ili kuinia uchumi wake.
No comments:
Post a Comment