Michezo ya 19 ya jumuia ya Madola yamalizika nchini India.

Katika mashindano hayo Australia ambayo imeondoka na medali nyingi za dhahabu zipatazo 74, ikifatiwa na Uingereza.
Akiongea wakati wa kufunga mashindano hayo rais wa michezo hiyo Mike Fennell alisema "michezo yote imekwisha vizuri na kila aliyeshiriki alifurahi japo kulikuwa na matatizo ya hapa na pale."
Picha hapo juu anaonekana mmoja ya watumbijazi akifanya vitu vyake wakati wa kufunga mashindano ya nchi ya jumuia ya Madola ya liyo fanyika nchini India
Picha ya pili wanaonekana washiriki na wanamichezo walioshiriki mashindano ya nchi wanachama wa jumuia ya Madola wakiwa uwanjani tayari kwa ufungaji wa michezo ya hiyo.
Venezuela ya saini mkataba na Urussi kujenga mitambo ya nguvu za kinyuklia

Mkataba huo uilisainiwa na waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Nikolaus Maduro na rais wa mambo ya kinyuklia wa Urussi Sergie Kiriyenko.
Makataba huo kati ya serikali ya Urussi na Venezuela ulishuhudiwa na viongozi wa serikali zote mbili Hugo Chavez wa Venezuela na Dmitry Medvedev.
Mara ya kusaini mkataba, rais wa Urusi alisema "Venezuela ni mshiriki mkubwa wa Urussi katika nyanja za kimaendeleo."
Picha hapo juu anaonekana rais wa Venezuela Hugo Chavez kushoto akiwa na rais wa Urussi Dmitry Medvedev kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo ya kiserikali.
Barabara ndefu duniani ya kamilika kuchimbwa

Uchimbaji huo amabo ulianza miaka 15 iliyopita ulimalizika leo kwa kuunganisha barabara hiyo na barabara ambayo iliyopo Gottard Base.
Barabara hiyo itaunganisha kusini na kaskazini mwa Ulaya kiusafiri hasa ule wa mizigo mikubwa.
Picha hapo juu anaonekana mmoja ya wafanyakazi akiwa kazini kuanza ujenzi wa reli itakayo tumika kubebea mizigo.
No comments:
Post a Comment