Tuesday, October 26, 2010

Tarik Aziz ahukumiwa kifo na mahakama kuu nchini Irak.

Tarik Aziz ahukumiwa kifo na mahakama kuu nchini Irak.

Baghdad, Irak 26/10/2010. Mahakama kuu nchini Irak imemuhukumu adhabu ya kifo aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na naibu waziri mkuu wakati wa utawala wa rais Saddam Hussein.
Hukumu hiyo ilitolewa kwa Tarik Aziz ambaye alikuwa msemaji mkuu wa serikali ya Irak katika shughuli zote za kimataifa.
Tarik Aziz 74, alikuwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wakati wa utawala wa rais Saddam Hussein kutoka katika madhehebu ya Kikrisru
Picha hapo juu anaonekanaTarik Aziz enzi zake kama waziri wa mambo ya nchi za nje wa Irak akihutubia moja ya mkuutano mkuu wa umoja wa Mataifa.
Picha ya pili anaonekana Tarik Aziz akikaribishwa na hayati Papa John Paul II wakati alipo kwenda kumtembe Vatikani kwa mazungumzo.

No comments: