Friday, March 25, 2011

NATO kuongoza mapambano zidi ya Libya.

NATO kuongoza mapambano zidi ya Libya.

Brussels,Ubeligiji - 25/03/2011. Jumuia ya ulinzi na shirikisho la kijeshi la nchi wanachama wa
NATO zimekubaliana kuchukua majukumu na kuongoza vita zidi ya kiongozi wa Libya.
Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen aliongea na waandishi wa habari baada ya kikao cha viongozi hao kuamua kuchukua jukumu hilo kutoka kwa serikali ya Amerika.
Anders Fogh Rasmussen alisema " NATO itachukuwa majukumu yote ya kuhakikisha ya kuwa amri iliyo wekwa na umoja wa mataifa ya kumzuia kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kutumia jeshi la anga katika mashabulizi zidi ya wapinzani wake."
NATO ilianza mashabulizi nchi Libya baada ya kamati ya usalama ya umoja wa mataifa kupiga kura kumzuai kiongozi wa Libya kutumia jeshi la anga.
Wimbi la mageuzi ya kisiasa la aanza nchini Syria.
Daraa, Syria - 25/03/2011. Maafias wa usalama nchini Syria wamewashambulia waandamanaji ambao wanataka serikali ifanya mageuzi ya kisiasa.
Waandamanaji hao ambao waliandamana katika mji wa Daraa, walikutana na police na maafisa usalama wakati wakiwa njiani kuelekea kwenye ofosi za serikali.
Rais wa Syria Bashar al Assad ametangaza kuachiwa kwa wale wote walio kamatwa.
Maandamano yanayofanyikannchini Syria ni moja ya wimbi la mageuzi ambayo yana vuma katika bara la Kiarabu na nchi za Kiarabu pia.

No comments: