Sunday, March 20, 2011

Mashambulizi nchini Libya ya zidi kupamba moto.

Mashambulizi nchini Libya ya zidi kupamba moto.

Paris, Ufaransa - 20/03/20. Jeshi la Ufaransa kwa kushirikiana na washiriki wake wanaenedelea na mashambulizi kwa kutumia jeshi la anga ilikuzuia jeshi la Muammar Gaddafi.
Mashambulizi hayo ambayo yameshachukua siku mbili yameanza kuchukupicha tofauti baada ya maafa kutokea na kuleta hisia tofauti.
Akiongea kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alisema " vita vilivyo anzishwa na nchi za Magharibi na washirika wake vitakuwa na maafa makubwa kwa jamii nzima ya kimataifa na itachukua muda mrefu kuliko walivyo dhania."
Mmoja wa mkuu wa jeshi la Amerika Admiral Mike Mullen amesema "mashambulizi nchini Libya hayana maana ya kumtoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo."
Wakati huo huo jumuia ya nchi za Kiarabu imelaumu mashambulizi yaliyo fanywa na Ufaransa na washiriki wake, akiongea katibu mkuu wa jumuia hiyo Amr Mussa alisema "majeshi ya Ufaransa na washiriki wake yanafanya kinyume na makubaliano ambayo ni kulizuia jeshi la Libya lisitumie jeshi la anga, lakini sasa mashambulizi yanaelekea kuleta maafa kwa raia."
Mashambulizi nchini Libya yameanza baada ya Umoja wa matifa kupigakura na kukubali kuingilia kati matatizo ya wenyewe kwa wenye kati ya watu wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi na ya wapinzani wake.

No comments: